Case Close: Aishi Manula ni Tanzania One, Case Starts: Namba moja Afrika

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Itoshe kusema kwamba ndani ya misimu hii mitano huyu ndio golikipa bora kwa Tanzania. Kumlinganisha na golie wengine ni kumkosea heshima tu. Tusisubiri mpaka Rais Samia amtolee tamko. Hii kesi tunaifunga na faili tunalitupa makumbusho.

Tunafungua faili jipya tunasema Aishi Manula anatosha kuwa goli kipa namba moja Afrika. Onyango wa Mamelod anasubiri. Sote tumeona save za hatari alizofanya Congo na ile game ya Al Ahl. Leo mechi ya Libya ametufunga midomo kabisa.

Bishoo AirManula hongera sana
 
Binafsi miaka miwili iliyopita nilikuwa simkubali Aishi Manula kutokana na mapungufu yake ktk kulilinda lango,

Lakini kiukweli ameimprove sana hivi karibuni, amekuwa nguzo muhimu ktk idara ya goalkeeping kuanzia Simba mpaka Starz.
Yale mapungufu yake hasa katika udakaji mipira ya juu, kuzicheza krosi, kona na fouls yamepungua kwa kiasi kikubwa sana

Na katika michuano ya CAF-CL mpaka mzunguko wa mechi nne unaisha ni magolikipa wawili tu waliocheza dakika nyingi zenye clean sheet, Ahmed Reda Tagnaouti wa Wydad Casablanca ya Morroco alipo Msuva na Aishi Salum Manula.

Kongole sana AirManula
 
Ungetuwekea stats zao hapa mkuu ili tuone nani zaidi kuliko kuleta maneno matupu.

Weka stats tuwalinganishe.
 
Manara anasema ye ndie kamjenga Manula alimwambia awe anatokea mipira
 
Tanzania One hutoka Simba mara nyingi (kama sio mara Zote), hili lilishaandikwa hivyo.
 
Sio huyu aliyetunguliwa kizembe na Prison akataka kubondwa na mashabiki,sio huyu anayetunguliwa mita 40, lile ni pazia
 
Naunga mkono hoja Air Manula ni Tz one,refer ile save aliyoifany game ya Simba vs al ahly dakik za mwsho huy jamaa ni fundi kweny masual ya goalkeeping!
 
Ulaya ipi kwa kimo kile, sema azidishe mazoezi ili hata apate timu hapo Afrika Kusini.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
Acheni ulimbukeni Africa kusini kuna team moja tu ambayo ni Mamelod nyingine zinazidiwa mafanikio na Simba kwenye Mpira wa Africa .Ungesema Egypty ,Tunisia na Morocco
 
Acheni ulimbukeni Africa kusini Luna team moja tu ambayo ni Mamelod nyingine zinazidiwa mafanikio na Sumba kwenye Mpira wa Africa .Ungesema Egypty ,Tunisia na Morocco
Acha wenge soma ukiwa umetuliza msambwanda vizuri, mwenyewe umekiri Afrika kusini kuna timu imeizidi Simba ndio aende huko sasa, hapo nilisema .. hata apate timu Africa Kusini, nikiimanisha anaweza kwenda pengine palipo na mafanikio zaidi ya Bongo.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…