Evarist Chahali,
..hoja yako ni nzuri, lakini naona umeichanganya na mfano mbaya ulipoleta suala la Chadema kutokwenda mahakamani kuhusiana na waliokuwa wanachama wao kujipeleka bungeni.
..mimi nadhani ungekuwa sahihi kama ungewashinikiza wabunge 19 ni kwanini wanahudhuria bungeni wakati chama chao kimewafukuza uanachama.
..Yuko mbunge mmoja alikiri bungeni kwamba amefukuzwa uanachama, na kitu cha kushangaza Naibu Spika akamkatiza hotuba yake na kumuelekeza afute kauli kuwa amefukuzwa uanachama.
..Pia wanaoweza kwenda mahakamani sio Chadema peke yao. Hata wabunge 19, Tume ya uchaguzi, Ofisi ya Spika, Msajili wa vyama vya siasa, wanayo dhima ya kulipeleka suala hili mahakamani ili liamuliwe kisheria.
..Kuhusu Chadema kutokwenda mahakamani inawezekana ni kutokana na UZOEFU wao na mahakama zetu. Kuna matukio mengi ya mahakama kuwaonea Chadema ama kwa kuwatia hatiani kwa makosa ya kubambikiwa, au kuamua mashauri kwa namna ya kukikandamiza chama hicho.
..Ni maoni yangu kwamba mhimili wa mahakama nao unapaswa kuhojiwa kama umekuwa ukitenda HAKI wakati wote. Kuna umuhimu wa mhimili huo kujitathmini utendaji wake na maadili yake.
..Naamini utendaji mbovu wa mahakama zetu ambazo zinashirikiana na wavunja sheria, na katiba, na hali hiyo imepelekea wananchi kukata tamaa kutafuta haki zao mahakamani.