Case study kuhusiana na mjadala wa Katiba Mpya

Kujenga sanamu la mwendazake sio upotevu wa pesa za umma?
Raisi ni alama ya nchi, kutumia pesa ya umma kujenga sanamu yake ni kutaka akumbukwe,

Ingekuwa tunatumia pesa ya umma kutaka kujenga sanamu la mjomba wako au bibi yako, ndo yangekua matumizi mabaya ya pesa

Maana hakuna cha maana wameifanyia hii nchi,

NB: tusiharibu mada ya katiba tafwadhari.
 
Amefeli, ameleta suala la Chadema makusudi ili kuthibitisha mahaba aliyonayo kwa "mama" na huo mfano wake mbovu ndio umeharibu kabisa uhalisia/mantiki ya hiki alichoandika, juu kule nimeshamuonesha ni kwa namna gani Chadema hawastahili kuingizwa kwenye hili andiko lake, badala yake watawala wa nchi hii ndio wahusika wakuu.
 

..Mfano wa chama kikuu cha upinzani hapa Tz kutokuwa na imani na mahakama zetu ni uthibitisho wa ulazima wa marekebisho makubwa ya katiba na sheria za nchi yetu.

..Kwa kifupi ni kwamba sheria na taratibu zetu zinawalinda zaidi watawala wanaopoka haki na kuliko wananchi wanaotafuta haki.
 
Na kwa upande wa wananchi inakuwa wepesi sana kuchukuliwa hatua za kisheria wakati viongozi wa nchi hulindwa hata kama wakivunja sheria makusudi, naona huyu jamaa kaja hapa kuitetea hii Katiba mbovu iliyopo "kisayansi fulani", apuuzwe.
 
Mtoa mada anajichanganya sana kuanzia suala la kuheshimu katiba na sheria za nchi pamoja na hiyo case study yake.

Kwanza ungetueleza Ni akina nani hasa ambao hawaheshimu katiba na sheria za nchi yetu?

Kwa akili za kipropaganda unataka kutuaminisha katiba na sheria ya Nchi haziheshimiwi na Chadema hivyo hata hitaji la katiba mpya Ni sawa na bure kwasababu ya Chadema yenyewe imeshindwa kutokwenda mahakamani kwaajili ya kufungua kesi ya kufoji kwa wabunge 19 kwako unaona ni sawq na kushindwa kuheshimu katiba na sheria Nchi kwa Chadema, mtego wako kwa Chadema umejaribu kuuweka hapo.

Udhaifu wa mada yako uko hapa kwamba wakati wa utawala wa JPM unaamini Chadema kutokwenda mahakamani kufungua kesi ya kufoji dhidi ya wabunge 19 kwako Ni sahihi Ila kutokana na Mbowe na wezake na watu mbalimbali kuachiwa katika utawala wa mama Samia Saluhu unadai Chadema haiko sahihi kutokwenda mahakamani.

Nataka kukumbusha Chadema haimini kwa mtu ( Kama unavyotaka watanzania wamuamini mama samia?) inaamini kwenye katiba na sheria zetu za Nchi Sasa Ni ujinga kuitaka Chadema iweke Imani kwa mtu badala ya katiba na sheria za Nchi.

Chadema haimini tena kwenda mahakaman kwasababu katiba na sheria bado ni zilezile zilizotumika kukandamiza haki za watu na hazijabadilishwa mpaka hivi Sasa hivyo Chadema inaamini Nchi haiwezi endeshewa kwa hisani ya mtu Kama ulivyotaka kutuaminisha Bali kwa kufuata katiba na sheria zetu za Nchi.

Watanzania (Chadema) wanataka katiba mpya ambayo itaifanya bunge na mahakama zetu ziwe huru na sio kuongozwa kwa utashi wa aliyeko madarakani kwa wakati huo.

Mtoa mada unaonekana una Imani na mtu na sio katiba na sheria zetu
 
Akikumbukwa inamsaidia nini bibi yako asiye na maji safi ya kunywa kijijini kwako au dada yako anayedanga miaka mitano sasa kwa kukosa ajira?
 
Na kwa upande wa wananchi inakuwa wepesi sana kuchukuliwa hatua za kisheria wakati viongozi wa nchi hulindwa hata kama wakivunja sheria makusudi, naona huyu jamaa kaja hapa kuitetea hii Katiba mbovu iliyopo "kisayansi fulani", apuuzwe.

..hatakiwi kupuuzwa, vinginevyo anaweza kuleta madhara kwa jamii.

..ukimpatia majibu mazuri unatoa elimu kwa wasomaji ambao wangeweza kuwa mislead na alichokiandika.
 
Akikumbukwa inamsaidia nini bibi yako asiye na maji safi ya kunywa kijijini kwako au dada yako anayedanga miaka mitano sasa kwa kukosa ajira?
Kazi ya kupiga ramli huiwezi, kaa kwa kutulia,

Kumbukumbu ya Magufuli ni chachu kwa viongozi wazalendo wajao

NB: tusiharibu mada ya katiba tafwadhari.
 
Rufaa ya hao wabunge 19 ilishaamuliwa na baraza kuu la chadema?!
 
Katiba ni suala la Kitaifa linalogusa kila nyanja , case study yako kujikita Chadema tu inaondoa uhalali wa uzi wako
 
Kosa kubwa sana wanalofanya watu wanaodai katiba mpya ni kutilia mkazo kipengele kimoja kama ndicho katiba nzima i.e. tume huru ya uchaguzi. Mimi ni mmoja wa watu wanaoamini kabisa kuwa Tanzania inahitaji katina mpya haraka iwezekanavyo (iwe haraka lakini tusi-compromize uzuri wa katiba). Kwa nini tunahitaji katiba mpya? Tunahitaji katiba mpya kwa sabanu system yetu ya utawala imekuwa-failer na imetufanya kusonga mbele kwa kusuasua sana. Kila akija rais mpya anakuja na ahadi nzuri lakini anapoondoka anakuwa ameshachokwa na anayekuja anakuwa akama anaanza upya. Waungwana wanasema kurudia kufanya jambo lile lile kwa namna ile ile huku ukitegemea matokeo tofauti ni kama wendawazimu. Sisi tumekuwa kama wendawazimu. Kila rais anajaribu njia yake ya utendaji lakini hali haibadiliki. Ebu angalia muundo wa serikali, ebu angalia madaraka ya rais, hebu angalia utendaji na uwajibikaji wa kila mteule wa rais. Just ni impossible kuwa na positive results. Tanzania ni kubwa sana, kutegemea rais awe ndiye alfa na omega ni kama kutegemea rais awe na uwezo wa Mungu. Kwa hiyo kwangu mimi katiba mpya ni suala la utendaji na maendeleo kuliko tume huru ya uchaguzi. Nipe katiba mpya yenye muundo mzuri wa utalawa na acha tume ya uchaguzi jinsi ilivyo, nitakubali. Kwa nini tusikopi aina na muundo wa utawala kutoka klwa nchi zilizopiga hatua?
 
Akili inaanza kurudi
 
Yaani unaandika as if hujui kuwa system nzima imecollude kuwaingiza hao wanawake 19 bungeni!

Halafu kitendo cha kusema kuwa unawaelewa CHADEMA kutofungua shauri hilo mahakamani enzi za mwendazake ila unawashangaa sasa kwa nini hawafanyi hivyo wakati zama zimebadilika ni ushahidi wa Wazi kuwa unatambua kuwa Mahakama haziko huru zinaingiliwa. Kama ziko huru kwa nini zisijisimamie imara kila mtawala mwingine anayoingia madarakani!.

Mbele ya huyu mama ambaye ameshatangaza kupiga marufuku neno "kwiyo"tangu akiwa makamu wa raisi, mtawala anayeamini rais hakosei, mtawala anayeteua watu walionunuliwa na yeye anajua walinunuliwa, mtawala anayepiga marufuku mikutano ya siasa kinyume cha sheria kama mtangulizi wake, UNA IMANI NAYE HATOINGILIA MAHAKAMA KATIKA SHAURI HILI AMBALO LITAITIA AIBU HATA SERIKALI YAKE AMBAYO INAENDELEA KUWALIPA MSHAHARA WALE WABUNGE?
 
..hatakiwi kupuuzwa, vinginevyo anaweza kuleta madhara kwa jamii.

..ukimpatia majibu mazuri unatoa elimu kwa wasomaji ambao wangeweza kuwa mislead na alichokiandika.
Noted.
 
Mkuu watu wengine wanajipendekeza kutafta uteuzi.

Waganga njaa sio wa kuwasikiliza.
 
Mwana kitengo just sit and not be corrected
 
Hiyo mijadala iendeshwe na nani sasa ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…