Case study kuhusiana na mjadala wa Katiba Mpya

Hii nchi ina wasomi wengi sana, wataendesha hao.
Katiba ina sura mbili ya kisheria na kisiasa.

Huwezi kuitenganisha katiba na siasa kutengeneza katiba siyo Caesarean Section procedure kwamba unahitaji technocrats.

Wanasiasa ndiyo chimbuko la mabadiliko mengi ya mifumo ya kiutawala siyo hao wasomi wako au unataka kusema wanasiasa siyo wasomi ?
 
Mchango mzuri asante sana kiongozi kwa maono mazuri juu ya maendeleo ya taifa letu kwa ujumla.

Nilikuwa napenda kuchangia mjadala huu kwa kutowa mawazo kuwa ni kwa asilimia ngapi ya watanzania wenye uwelewa juu ya sheria mbali mbali zilizomo kwenye katiba ?.

Kwa mawazo yangu tu madogo naona kuwa kundi kubwa la Taifa letu halina uwelewa mkubwa kuhusu katiba na wachache ndio wenyeuwelewa na ndio walio soma katiba na kuiyelewa.

Mfano unaweza ukafanya mkusanyo mdogo wa takwimu humu humu ndani ya JF kuwa ni wangapi tunaelewa kusu katiba na sheria zipi zipo imara na nisheria zipi ni dhaifu na zinapaswa kufanyiwa mabadiliko.

Hili ndiyo linalo leta ukakasi na kufanya swala la kudai katiba mpya kuwa zito zaidi.

Ningependa kusema kuwa kama kungekuwa na uwezekano wowote ule wa watu kuweza kueleweshwa juu ya katiba na kukawa na uchambuzi wa sheria zilizo imara na sheria zilizo dhaifu basi mungano ungekuwa mkubwa na sauti ingesikika.

Haya ni mawazo yangu tu wa dau wa jukwaa naamini akuna kinacho shindikana chini ya hili jua maadamu uhai upo. Asante mwasilisha mada.
 
Ninapata shaka sana kuhusu katiba..

Preamble ya katiba yasema watu wote ni sawa ajabu ukiingia ndani ya katiba hii kuna watu wana "kinga" hata wakitenda uovu hii kweli itakua na mantiki??

Tukienda ndani zaidi uhuru wa kutoa maoni unaruhusiwa pia kuanzisha mkusanyiko ..

Ajabu ni kuwa kuna watu hapo hapo walikataza, wanakataza na wataendelea kukataza uhuru wa kutoa maoni na kufanya kusanyiko kujadili masuala mbali mbali...

Hawa wanaoivunja katiba huku wakijua hawana cha kupoteza wala cha kuwafanya bila kuibadili miaka nenda rudi si itakuwa madhila kwa waliowaajiri na ndio walipa kodi?
 
Shida mahakama hazipo huru, Ndugai kajiwekea kinga utamfanya nini? hao wabunge taasisi ya urais inahusika moja kwa moja, Mwendazake hayupo lakini wateule wake akina Mnganga bado wapo.
 
Katiba kutoka kwa mwanasiasa ni ile inayompa favour yeye kwanza

So ukimkaribisha mwanasiasa akutengenezee katiba, tegemea mivutano isiyo na maana(kila mtu atatetea kinachompa favour)
 
Sheria inasema maamuzi ya tume yanaweza kupingwa mahakamani? Au umesahau kuwa matokeo ya uchaguzi hayawezi kupingwa mahakamani?
 
Hata mahakama zitakuwa huru zitaanza kutenga haki
 
Nakushangaa chadema ni chama cha siasa nimetoa kauli hawahusiki na hiyo barua ya wabunge 19,na imetoa hukumu kama chama kuwafukuza walio forge,kaa kwenye kiti jiuulize vizuri nani mwingine inatakiwa kuchukua hatua dhidi ya fojali hiyo.
 
Chahali chadema wamejaa majukumu kwa kuwafukuza uanachama na kutoa kauli kuwa hawahusiki na hiyo barua,wamefoji na kulidanganya bunge,chadema hapo ni shahidi shahidi ataendaje kufungua kesi
 
Binadamu yoyote ni mwanasiasa.
Katiba kutoka kwa mwanasiasa ni ile inayompa favour yeye kwanza

So ukimkaribisha mwanasiasa akutengenezee katiba, tegemea mivutano isiyo na maana(kila mtu atatetea kinachompa favour)
 
Mzalendo anaweza kujenga airport kijijini kwake huku akiwaacha mamilioni ya watu bila maji safi ya kunywa?
Kazi ya kupiga ramli huiwezi, kaa kwa kutulia,

Kumbukumbu ya Magufuli ni chachu kwa viongozi wazalendo wajao

NB: tusiharibu mada ya katiba tafwadhari.
 
Katiba sio kipaumbele cha wanannchi walio wengi wa Tanzania .

Kama wao wanataka katiba mpya waunde ya kwao na waitumie wao kama wao .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…