Hoja: la muhimu zaidi ni heshima kwa sheria, na kwa vile Katiba ni sheria mama, basi heshima husika iwe kwenye sheria zilizomo kwenye katiba.
Hali ilivyo sasa: ni kweli katiba iliyopo ina mapungufu mengi. Na ni kweli kuwa mapungufu hayo yanaathiri maeneo mbalimbali hususan haki za kisiasa/kidemokrasia.
Katiba yote ya sasa ina mapungufu?: Hapana. Kuna sheria nyingi tu katika katiba ya sasa ambazo ni mwafaka. Tatizo ni kwamba heshima kwa sheria ni changamoto kubwa kwa Watanzania. Kwahiyo hata sheria hizo "nzuri" zaishia kuonekana "mbaya" kwa sababu zinapuuzwa
Case study: kwa mujibu wa maelezo ya Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilifoji majina wa wabunge 19 wa viti maalum wa chama hicho. Kufoji ni kosa la jinai. Hadi muda huu Chadema hawajafungua mashtaka dhidi ya tume ya Taifa ya Uchaguzi kutokana na forgery hiyo.
Tatizo lipo wapi? Ukisikiliza mjadala kuhusu Katiba mpya, focus ipo kwa watawala. Nguvu kubwa za Rais, Tume ya uchaguzi kutokuwa huru, nk. Lakini pengine kwa makusudi au kutojua, hakuna mjadala kuhusu "mapungufu ya watawaliwa." Mfano hai hapa ni huo wa NEC kuvunja sheria lakini wahanga wa uvunjifu huo wa sheria, Chadema hajachukua hatua za kisheria. Sasa hapo tatizo si katiba bali ni kupuuza sheria inayoweza kutoa haki stahili.
Logic ya wakati huo kwa Chadema: zama za Mwendazake, ingekuwa sawa na kupoteza muda kwa Chadema kwenda mahakamani kudai haki yao.
Logic ya sasa: huhitaji kuwa na upeo mkubwa wa kinachoendelea Tanzania kubaini kuwa zama zimebadilika haswa. Japo utaambiwa "kutenguliwa hukumu ya Mbowe na Mdude kuachiwa huru ni suala la kimahakama," ukweli wa wazi ni kuwa haya yasingewezekana katika zama za Mwendazake.
Kwa maana hiyo: kwa vile mazingira yaliyopo ni rafiki kudai haki, angalau kwa kigezo cha kesi hizo mbili, kwanini Chadema wasiiburuze mahakamani Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kosa la kufoji majina 19 ya wabunge wa viti maalum?
Katiba mpya inaingiaje hapa?: Naam kuna haja ya marekebisho ya sheria mbalimbali kandamizi. Endapo mabadiliko hayo ni lazima yafanyike kwa njia ya Katiba mpya, ni sawa. Endapo badala ya katiba mpya tunaweza kufanya marekebisho tu ya katiba, ni sawa pia. However, iwe ni marekebisho ya katiba au ujio wa katiba mpya, kasumba ya kupuuza sheria itafanya marekebisho ya katiba/katiba mpya kuwa tatizo kama ilivyo sasa.
Kama alivyosema Askofu Bagonza kuwa wanaovunja Katiba hii wanaweza pia kuvunja katiba mpya, nami nahitimisha kuwa wanaopuuzia kudai haki zao kipindi hiki cha "katiba yenye mapungufu" wanaweza pia kupuuzia kudai haki zao katika zama za "Katiba mpya."
Na mwisho kabisa, kama hatuwezi kuheshimiana sie wenyewe katika mjadala huu muhimu kwa mustakabali wa taifa letu, hiyo katiba mpya itaheshimiwa vipi maana asiye na heshima kwa mtu ana nafasi kubwa ya kutokuwa na heshima kwa kitu/vitu (eg Katiba).
Mfano hai wa "kukoseana heshima" ni pale nguli wa sheria Prof Issa Shivji alipotoa angalizo kuhusu katiba mpya na kutanabaisha kuwa sio mwarobaini wa kutatua changamoto mbalimbali, baadhi ya "wasiopenda mawazo tofauti na yao" wamedai profesa huyo anazeeka vibaya. Wengine wameenda mbali na kumtusi kuwa "nafasi za u-DC zimejaa."
I stand to be corrected 🙏
Mengi yamesemwa kwa nini katiba mpya na kwa nini katiba mpya ni hitajio la wengi:
1. Case ya wabunge 19 inahusu tuhuma za forgery. Forgery ni jinai. Polisi na hata TAKUKURU wanawajibika kuchukua hatua dhidi ya tuhuma zozote za jinai bila ku msubiri mlalamikaji.
Bunge, Tume ya Uchaguzi na Msajili wa vyama vya siasa vyombo vya umma watuhumiwa wakuu wa kadhia hii, kwa dhamana yao kutoka kwa wananchi, walipaswa kujibu tuhuma za Chadema zilizowasililishwa kwao kwa maandishi kuhusiana na ubatili wa wabunge hao.
Ofisi hizi si mali binafsi.
2. Kwamba ilikuwa sawa Chadema kutokwenda kulalamika mahakamani kipindi cha mwendazake ila si sawa kutokwenda kulalamika sasa kwa sababu hiki kipindi ni cha Samia?
Kwa nini kufungamanisha hivi mihimili na serikali? Kufungamanishwa huku ni ukiukwaji wa katiba. Mhalifu katika hili ni rais madarakani anayepaswa kuilinda na kuiheshimu katiba. Kwa mujibu wa katiba hii hata asipoilinda wala kuiheshimu hakuna cha kumfanya.
Kama JPM alikuwa akivunja katiba kwa mujibu wa katiba nini kitamfanya Samia asifanye hivyo hivyo? Ni vipi mlalamikaji ategemee haki kwenye mfumo kama huu na hasa mtuhumiwa anapokuwa ni serikali?
(Mzee Kingunge ni katika watu ya 7 walioiandika katiba tuliyo nayo 1977.)
Kumbuka rais si mtu bali ni taasisi. JPM kaondoka lakini taasisi ya urais ni ile ile. Bila shaka ndiyo sababu ya kauli hizi: Samia = JPM na Kazi iendelee. Yaani pori jipya nyani wale wale.
Timu inayomzunguka Samia ni ile ile iliyokuwa ikimzunguka JPM. Bila ya shaka nia yao ya kuendeleza yote ya JPM bila yeye kuwepo iko pale pale kwa maneno na vitendo.
Zama za katiba mbovu ni zile zile hakuna kilocho badilika.
3. Kwamba kwa vile Mdude kaachiwa au kesi ya kina Mbowe hatimaye wamepewa ushindi hivyo ndiyo viwe vigezo vya kuwa sasa kuna nia njema ya Rais? Kwamba kwa sababu hiyo na mahakama nazo ndiyo zimeanza sasa kutenda haki? Inatosha hiyo kweli kumshawishi mtu na akili zake?
Kwanini masuala ya mahakamani yategemee utashi wa rais?
Tuna uhakika gani kuwa huyu ataacha mahakama kuwa huru kama hata yule hakuwahi kukiri kuwa alikuwa akiziingilia mahakama? Huyu naye akiwa anaziingilia mahakama tutamwajibisha vipi?
Tunahitaji katiba yenye kuweka usawa na adhabu za wazi kwa kila mvunja katiba bila ya kujali cheo.
Tunataka katiba iliyo wazi kwenye usawa, uhuru, haki, demokrasia na utawala bora. Katiba itakayo tufanya:
1. Sote kuwa sawa mbele ya sheria
2. Kusiwe na kubambikiziana kesi
3. Tuwe na viongozi wenye tija watokanao na ridhaa yetu
4. Tuweze kumwajibisha yeyote asiyekidhi matarajio yetu na kwa wakati
5. Kuiendesha nchi katika hali ya makubaliano
6.Nk.
Hata hivyo nisiache kuweka kipande hiki:
Hii ikiwa ni kwa sababu mleta mada unajulikana kwa mchango wako kwenye kusukuma jitihada za kupatikana kwa katiba mpya.
Kulikoni ndugu mjumbe chighafla leo, hujui kwa nini katiba iliyopo inashindikana kusiimamiwa isivunjwe?!