Case study: Waliosoma english medium ni "wazuri" kuliko waliosoma shule za kawaida


Na ndio hicho kinachotuponza wengi, mazingira.
Mimi nimesoma hizo hizo shule za ikungu igeni, Mseko, Shelui, Ntwike kwa elimu ya msingi (Baba alikua mwalimu).
Ni zile shule ambazo yaani mtu unapelekwa tu kama hatua ya ukuaji, hata kufaulu kwenda sekondari ni kama ajali, hujui ukimaliza la saba ni hatua gani inafuata. Matokeo yakitoka unaambiwa unatakiwa kwenda sekondari.

Nilibahatika kupenda kusoma vitabu vya kiingereza series fulani ya oxford ilikua na hadithi za akina Abdul kuanzia kitabu cha kwanza hadi cha sita. Na baada ya hapo nikawa napenda kujisomea vingine vya kiingereza kwa sababu nilikua na weza kwenda maktaba na kuchukua vitabu nnavyotaka. Kana kwamba haitoshi nilikua nasilikiza BBC english japo naokota neno mojamoja lakini kadri muda ulivyozidi kwenda nikawa napata kuelewa na kupata baadhi ya misamiati na maana ya maneno mengi ya kiingereza.

Hadi leo hii, vitabu ni eneo linalotumia vizuri kipato changu na sijawahi kujuta.
Shule zina umuhimu mkubwa sana kwenye suala la kiingereza kwa mtoto, lakini mazingira anayokutana nayo mtoto yana mchango mkubwa zaidi kumjengea mtoto huo uwezo.
 
Maendeleo ya Tanganyika hayawezi kuja kwa sababu ya kuongea kingereza. Kama umefikiri hivyo basi umekosea sana Hakuna kitu chenye nguvu kama lugha Mama sababu ni hii angalia mastaa kama Ronaldo anapewa tuzo ya dunia ila aliongea kireno.. raisi wa Brazil akiwa south Africa aliongea lugha ya Nyumbani Haya China VP... kwahiyo lugha ya kiswahili tumeipotezea dhamani sisi wenyewe Nina imani itafika wakati lugha Hii itatumika mpaka kwenye usahili
 
Kwa muktadha huu mwana wa Ngabu, kinachozingatiwa hapa ni fluent(I am not sure of the word) in speaking na wingi wa misamiati, haiangaliwi grammar, intonation wala tenses.

Kwa hiyo wakenya kwa kigezo kwamba it is their nation language, hatutakiwi kushangaa wakiwa fluent in speaking with a lot vocabularies.
 
Binafsi sijavutiwa hata kidogo na uwezo wa Wakenya wa kuongea Kiingereza. Sasa sijui wewe mwenzangu kilichokuvutia ni nini hadi uwamwagie sifa kihivyo?
kaka with all the minor grudges between us and kenyans(our neighbours ),i give them some credit in mastering the english language.nadhani kwa ukanda huu wa EA wanashika #1 .baadhi ya vipanga wanaosifika kujua sana kizungu nchini kenya ni prof p.l.o Lumumba(unaweza ukam-google).siku moja nilimuona akifanyiwa mahojiano na jeff koinange ktk kipindi chake the bench.jeff pamoja na kuishi kwake miaka mingi abroad na kufanya kazi CNN alimgwaya jamaa vile alivyo kuwa anazungumza.hiki ni moja ya kionjo cha p.l.o lumumba ktk english,ukisha soma nitaomba wewe au mdau yoyote wa lugha atuambie kama hiki kizungu ni sahihi au laa,cause saa zingine baadhi ya watu huwa wanamkosoa :
Forwarded by WANGARI KIHARA
“In promulgating your esoteric cogitations or
articulating your superficial sentimentalities,
and amicable philosophical or psychological
observations, beware of platitudinous
ponderosa. Let your conversational
communications possess a compacted
conciseness, a clarified comprehensibility, a
coalescent cogency, and a concatenated
consistency. Eschew obfuscation and all
conglomerations of flatulent garrulity, jejune
rabblement, and asinine affectations. Let your
extemporaneous descanting and
unpremeditated expatiations have intelligibility
and voracious vivacity without rodomontade or
thrasonical bombast. Sedulously avoid all
polysyllabic profundity, pompous prolificacy,
and vain vapid verbosity.
In short what Lumumba was telling his fellow
commissioners in the review team is: “Be brief
and don’t use big words!!!!” . maneno haya yanapatikana hapa :
kenyananalyst.wordpress.com/2006/05/17/plo-lumumba-yawa/
 
Kwa nini umhurumie mkuu?,
Mbona mimi naona amepiga English ya kufa mtu!?, sema tu maneno mengi sijaelewa.
 
Reactions: HMS
Actually, I have captured no theme in this article.
 
Kwa nini umhurumie mkuu?,
Mbona mimi naona amepiga English ya kufa mtu!?, sema tu maneno mengi sijaelewa.

Kingereza chake ni kizuri lakini sicho ambacho natives wanachokiongea kwenye maisha yao, sasa ukiongea hivo kwa mtu anaejua lugha ndo anakuona kama umeandika sivo, lakini ujumbe unafika na unaeleweka. kwa mfano kusema nataka kutapika, utasema I want to vomit, ni kweli sahihi lakini hilo neon vomit hasa linatumika hospital kwa daktari huko, lakini natives wenyewe hawasemi hivo bali wanasema I want to throw up, au I want to puke. kuna mifano mingi sn. sasa hapo juu hicho kingereza kinaeleweka vizuri lakini sio kinachoongelewa, sijui unanielewa mkuu. we maneno mengi hujaelewa maana haupo fluent. kwa mfano kwenye Kiswahili zamani mshkaji ilikua ni demu yaan king'asti au totoz ndo anaitwa mshkaji, lakini sikuhz mshkaji ni msela wako au m2 wa karibu yaan unaelewana nae ile ile, umenisoma, sasa akaja mtu ambae ndo hajui Kiswahili kivile hlf akaita mwanamke mhkaji hajakosea sema sasa hv Kiswahili kipo next levo mshkaji sio demu ila ni mtu msela unaemkubali awe man au demu wote mzuka. jamaa mie nimechoka kukuelewesha, yaan km hujaelewa basi mkuu.
 


Naomba nifungue dictionary, then tuanze neno baada ya neno, usikute prof alibabaisha tu...
 

PLO namjua. Hatumii vocab ngumu kihivyo. Ila naelewa kwa nini watu wanaona kama anatumia vocab ngumu.
 

Ni kweli wanaangalia kilicho kichwani kupitia hiyo lugha ya Kiingereza. Na ni dhahiri wale wa English-Medium wanaconfidence na wanaweza kujielezea vizuri kupitia hiyo lugha. Asikuambie mtu hata vocational insitutions kama VETA wamefahamu hilo kupitia feedback za waajiri na sasa wengi wanaona lost opportunities kwa sababu ya kutoweza kujielezea vizuri.
 
Nyani Ngabu, asante kwa video, ntaisikiliza baadaye naona network sasa hivi inasuasua.
Lakini, hivi vocab ngumu ni mpaka ziweje?

Mfano mtu anakuandikia hivi "...may your day be panctuated with arevanchism whose magniloquence can only be theatropistically analysed by the use of a reminiscent excarbation. I hope you dont mind my apostacy. I know your arquistic impedance might not engulf this kind of debanched pedagogy because of it's repuginatious tolecentrim..." hapa atakuwa ametumia maneno magumu au?

CC ​ Kiranga.
 

Kwanza kabisa, sijawahi kukutana na mtu anayeongea hivyo. Hata kwenye PMQ kwenye House of Commons huwa hawazungumzi hivyo. Hata kwenye kesi pale Old Bailey huwa hawatumii misamiati kama hiyo.

Mara nyingi utakuta maneno kama hayo yapo kwenye maandishi tu. Na mengi ya hayo maneno huwa ni ya zamani kiasi cha matumizi yake katika jamii kupungua. Na ukichunguza zaidi unaweza hata kukuta huyo mwandishi si mzungumzaji wa Kiingereza kama lugha yake ya kwanza, hivyo kunakuwa hulka fulani ya kujionyesha na wewe unaijua misamiati migumu (isiyotumika mara kwa mara) ya Kiingereza (si unajua tena Kiingereza ni ishara hadhi, elimu, akili, na sifa zingine ziendanazo).

Lakini kwa mtu ambaye anapenda kujisomea mambo mbalimbali zikiwemo kamusi, maneno kama hayo wala si mageni. Na siku hizi mambo ya mtandao yamesaidia sana. Unaweza kujiunga na tovuti za kamusi mbalimbali za Kiingereza ambazo huwa zina 'vocabulary quizzes' kwa ajili ya mazoezi ya kuongeza na kuimarisha msamiati.

Halafu, ukichunguza kwa makini zaidi unaweza kukuta mwandishi kayalundika lundika (pleonasm) tu hayo maneno mpaka kapoteza hata mantiki kabisa. Lakini kwa vile kuna dhana ya kwamba hayo ni maneno magumu, ni watu wachache sana watakaoweza au watakaokuwa na muda wa kuangalia matumizi pamoja na miundo ya kisarufi kama ni sahihi.

Ushawahi kukutana na mtu yeyote anayejibu maswali ya mtihani kwa kutumia maneno kama hayo?
 
Kiukweli nashukuru Mungu na wazazi kupita english medium,ZINA MCHANGO MKUBWA SANA,
however mtu ukiwa determined haijalishi umesoma wapi
 
Sasa mkuu naanza kujifunza kitu;

Sasa hapa tofauti ya maneno haya na yale ya Lumumba ni ipi?
 
Naanza kijufunza kwamba kwamba mtu anaweza akatumia maneno ambayo hayatumiki katika kuzungumza, aidha ni ya kizamani mno na anaweza akawa ameyarundika kiasi kwamba hayaleti maana.

Umesema yale maneno ya Lumumba ni ya kawaida tu, nataka kujua umeyatofautishaje na haya yangu?
Tofauti ni maneno yenyewe vipi?
Unaanza kujifunza nini?



Tofauti iliyopo ni maneno yenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…