The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 20,242
- 45,930
Now now now now, namaanisha nilimaliza kusoma vitabu fulani vya Chase.
Ningevipata vyote probably ningeweza kuvimaliza, lakini sikubahatika kuvipata vyote. Chase had that page turning style ambayo nilikuwa naipenda sana, it is addictive.
Sasa mtu kama wewe una vitabu hivyo, kama una watoto hapo nyumbani, wanaanza kuona mazingira ya vitabu nyumbani (although some of the Chase covers are not exactly child friendly, but in any case I am referring to books in general).
Kwa mtoto mdadisi, yale mazingira ya nyumbani yanaweza kuwa stimulant kubwa ya kujua lugha kuliko hata shuleni.
Mimi nakumbuka nilivyokuwa mdogo nilikuwa nasoma mpaka Engineering plans zilizokuwa nyumbani, sasa hapo mtu unaanza kupata udadisi kuhusu hizi plans zinasomwaje, hivi vialama vina maana gani etc kabla hujajua trigonometry.
Ndiyo maana naona umuhimu wa kuhoji hii dhana ya kutafsiri "watoto wanaoenda english medium wanajua zaidi kiingereza" kumaanisha kwamba english medium schools zinawapa advantage ya kujua zaidi kiingereza.
Obviously kufundishwa kwa kiingereza kunachangia, lakini kwa kiwango gani? Na kiwango gani kinachangiwa na mazingira ya nyumbani?
Inawezekana mtu kwao wana Time Magazine subscription, akiwa bored anajisomea, anajenga msamiati na uelewa wa Kiingereza, halafu akija kuonekana anajua, sifa zinaenda kwenye english medium school.
Na ndio hicho kinachotuponza wengi, mazingira.
Mimi nimesoma hizo hizo shule za ikungu igeni, Mseko, Shelui, Ntwike kwa elimu ya msingi (Baba alikua mwalimu).
Ni zile shule ambazo yaani mtu unapelekwa tu kama hatua ya ukuaji, hata kufaulu kwenda sekondari ni kama ajali, hujui ukimaliza la saba ni hatua gani inafuata. Matokeo yakitoka unaambiwa unatakiwa kwenda sekondari.
Nilibahatika kupenda kusoma vitabu vya kiingereza series fulani ya oxford ilikua na hadithi za akina Abdul kuanzia kitabu cha kwanza hadi cha sita. Na baada ya hapo nikawa napenda kujisomea vingine vya kiingereza kwa sababu nilikua na weza kwenda maktaba na kuchukua vitabu nnavyotaka. Kana kwamba haitoshi nilikua nasilikiza BBC english japo naokota neno mojamoja lakini kadri muda ulivyozidi kwenda nikawa napata kuelewa na kupata baadhi ya misamiati na maana ya maneno mengi ya kiingereza.
Hadi leo hii, vitabu ni eneo linalotumia vizuri kipato changu na sijawahi kujuta.
Shule zina umuhimu mkubwa sana kwenye suala la kiingereza kwa mtoto, lakini mazingira anayokutana nayo mtoto yana mchango mkubwa zaidi kumjengea mtoto huo uwezo.