Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUTOKA CASSIUS CLAY 1964 HADI KARIM MANDONGA 2022
Kuishi kwingi kuona mengi.
Sikumjua Mandonga hadi alipopigwa na Shabani Kaoneka na kuona taarifa zake mitandaoni.
Hapo ndipo nilipomfahamu Mandonga na kuanza kuona vituko vyake nje ya ulingo.
Mashaallah ni bingwa wa tambo.
Hakika mdomo haumkatai bwana wake.
Utapenda kumsikia akizungumza na kwa hakika utatishika.
Utakuwa na uhakika kuwa mpinzani wake havuki duru ya kwanza au kajitahidi duru ya pili atakuwa yuko chini anahema anasikiliza mwamuzi akimuhesabia…moja, mbili, tatu…
Nikamkumbuka Muhammad Ali 1964 wakati huo akijulikana kama Cassius Clay.
Mwaka wa 1964 nina miaka 12 na nikimpenda sana Muhammad Ali wakati huo anajitayarisha na pigano la kuwania mkanda wa dunia uzito wa juu dhidi ya Sonny Liston.
Cassius Clay yuko katika vyombo vya habari kila uchao anatoa maneno makali, makali na kejeli dhidi ya Sonny Liston.
Liston ndiyo bingwa wa dunia amevaa mkanda wa uzito wa juu lakini hamwezi Clay kwa mdomo.
Pambano hili likavutia watu ulimwengu mzima na hapo ndipo Muhammad Ali akaanza kufahamika.
Clay akajulikana kwa haraka kama alivyojulikana Mandonga.
Kuna watu ndani ya Marekani wakamchukia Muhammad Ali kwa ule mdomo wake wakataka siku ya pambano ifike domo la Cassius Clay lifungwe kwa ngumi nzito za Liston; kama vile wako waliotamani Mandonga afungwe mdomo wake na Shabani Kaoneka.
Kile alichoonyesha Cassius Clay Miami Beach katika pambano lake na Sonny Liston lilishangaza wengi, ilikuwa, ‘’Fly like a butterfly and sting like a bee.’’
''Ruka kama kipepeo na uma kama nyuki.''
Naam Cassius Clay alipepea.
Katika ulingo Liston anamkimbiza Cassius Clay na hamfikii wala hampati.
Kilichobakia ni historia.
Allah ni mwema sana.
Nilikuwa naandika kitabu cha maisha ya mwimbaji Sal Davis.
Tuko London mwanzo wa kitabu mwaka ni 1963 Sal Davis kaacha shule Manchester amekwenda London na amekuwa mwanamuziki kijana wa kusifika akifanya show Soho sehemu maarufu kwa mengi hapo mjini.
Sal Davis kijana kutoka Makadara Mombasa mbali ya kupiga muziki usiku vilevile kaajiriwa na BBC kama mtangazaji akifanya kipindi cha michezo, ‘’Sports This Week.’’
Sal Davis akaniambia kuwa alikwenda kumfanyia mahojiano Cassius Clay alipokwenda London kupigana na Henry Cooper.
Hii ilimpa nafasi yeye kuonana na Muhammad Ali na kushuhudia vibweka vyake kwa karibu.
Clay wasaidizi wake wakimwita ‘’Champ,’’ ingawa alikuwa hata huo mkanda bado hajauvaa na yeye akiitika kama kweli ndiye bingwa wa dunia ingawa bingwa mwenyewe alikuwa Sonny Liston.
Hii ilikuwa mwaka wa 1963.
Mandonga sijui kama mwenyewe alikuwa anafahamu kuwa kwa yale majigambo yake alikuwa anapita barabara aliyopita Muhammad Ali miaka 58 iliyopita wakati anaanza ngumi. zake.
Lakini masikini Mandonga hakuweza kutimiza yale aliyotimiza Cassius Clay siku alipokutana na Sonny Liston Miami Beach, Florida.
Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.
Mandonga bado unayo nafasi.
Shabiki wake mmoja kaandika mtandaoni anasema, ‘’Mandonga sisi washabiki wako tuko na wewe mpaka watakapokuua.’’
How cruel.