GE2025 Catherine Joachim Aibuka Mshindi wa Ubunge Tanzania Bara Katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi CCM

GE2025 Catherine Joachim Aibuka Mshindi wa Ubunge Tanzania Bara Katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Wazazi CCM

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Jumuiya ya wazazi ya chama Cha Mapinduzi (CCM) imetangaza matokeo ya uchaguzi wa wabunge na wa wakilishi wa Jumuiya hiyo huku Catherine Joachim akijinyakulia ushindi kwa nafasi ya ubunge Tanzania Bara kwa kujizolea kura 597 akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Khadija Shabani aliyepata kura 94.

Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
‎
‎Kwa upande na nafasi ya viti maalum wazazi Zanzibar aliyeshinda ni Najma Murtaza Giga aliyepata kura 591 kati ya kura 710 zilizopigwa na kuwabwaga wapinzani wake sita waliokuwa wanagombania nafasi hiyo.
‎
‎Kwa upande wa nafasi ya uwakilishi Zanzibar walioshinda ni Aza January Joseph aliyepata kura 350 akifuatiwa na Salama Abbas Juma aliyepata kura 330 na kuwabwaga wenzao sita ambao waliambulia kura zilizosalia.
‎
‎Akitangaza matokeo hayo Naibu katibu mkuu wa CCM, John Mongella amesema matokeo hayo ni ya awali hivyo walioshinda kwenye uchaguzi huo waendelee kusubiri maamuzi ya vikao vya juu vya chama ambavyo ndivyo vyenye maamuzi ya mwisho.
 
Back
Top Bottom