- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Baada ya Lissu kunyimwa funguo za Mikocheni ameamua kususa nafasi yake imezibwa rasmi na Catherine Ruge, Wasalimie sana ACT Wazalendo.
- Tunachokijua
- Catherine Ruge Ni Mwanasiasa ambaye amewahi kuwa Mbunge wa viti Maalum Serengeti, kupitia CHEDEMA mwaka 2017 hadi 2020.
Freeman Mbowe ni Mwanasiasa na Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, CHADEMA
Kumekuwa na taarifa zinasambaa mtandaoni kuwa Catherine Ruge amepewa nafasi ya Tundu Lissu ambayo ni Makamu Mwenyekiti Bara kupitia CHADEMA. Tazama hapa, hapa na hapa
Je, ni kweli ni upi?
Jamiicheck imebaini Taarifa inayosambazwa kuwa Catherine Ruge ameziba nafasi ya Tundu Lissu ambayo ni Makamu Mwenyekiti bara si ya kweli, kwa sababu kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) huchaguliwa, na si kuteuliwa.
Kulingana na Katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006, toleo la mwaka 2020, Kifungu cha 6.3.1 kinaeleza kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA huchaguliwa na Mkutano Mkuu wa Taifa wa CHADEMA.
Uchaguzi huu hufanywa kwa njia ya kidemokrasia, ambapo wajumbe wa mkutano huo hupiga kura kuchagua viongozi wa chama, ikiwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti.
Makamu Mwenyekiti ni sehemu ya safu ya uongozi wa kitaifa wa CHADEMA, akimsaidia Mwenyekiti katika majukumu yake. Katiba imeweka utaratibu wa wazi wa uchaguzi wa viongozi wa ngazi za juu wa chama kupitia chombo kikuu cha maamuzi cha chama cha CHADEMA, yaani Mkutano Mkuu.
Aidha, JamiiCheck imepita kwenye kurasa rasmi za CHADEMA na Tundu Lissu na kuthibitisha hakuna sehemu yoyote ambayo kuna taarifa inayoeleza Makamu Mwenyekiti Bara amejiuzulu nafasi yake au kuondolewa kwenye wadhifa huo ili nafasi hiyo izibwe na Chatherine Ruge kama ilivyodaiwa.
Pia, Katiba ya CHADEMA kifungu cha 6.3.4 kinaeleza kuwa kukoma kwa uongozi kutakuwa kwa sababu za, kujiuzulu, kiongozi kuachishwa uongozi au kufukuzwa uanachama, Kushindwa kutumiza majukumu au kufariki, Kitu ambacho hakijathibitishwa kutoke Kwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA aliyepo.
Vivyo hivyo, Lissu, ameonekana akiwasili Tanzania leo 11 Septemba 2024 akitokea nje ya nchi na aliweza kujibu maswali ya waandishi wa habari waliomuuliza alipokuwa uwanja wa ndege, pia Wakati wa Mkutano wa CHADEMA kwenye Ofisi za CHADEMA Mikocheni alionekana kuendelea na shughuli za chama kama Kawaida.