CBE wagoma

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,947
Reaction score
4,470
Kwa taarifa nilizo pata sasa hivi wanafunzi wa CBE-Dar wamegoma kuanzia sasa.
Wanagomea matokeo ya supplementary wamefli vibaya mno kwa hiyo wamechukua uamuzi wa kugoma
 
Hivi Mitihani walifanyia Sanaa Pub ama maana nakuwa kama sielewi elewi... Wamefeli kwa kugoma ama wamegoma baada ya kufeli...

Wachukue mfano wa FOE [CoET] pale UDSM, wenzao masomo yakiwa yamebana wanaanzisha Kunji tu ili mitihani isifanyike kwa wakati uliopangwa...
 
Wamegoma baada ya kufeli wanadai wamefelishwa.
Chuo kimeomba kipewe wiki 2 kushughulikia madai yao.
 
Hivi CBE nacho ni chuo katika vyuo. Mabishoo wote wanaofeli o-level na A-level ndo kimbilio lao pale, sasa unategemea nini? Watu wengi pale wamefoji vyeti tu. Kuna mtoto wa uncle yangu alipata Div 0 form 4. Nikashangaa yuko CBE anafanya Diploma, hapo ndo nikakoma mwenyewe. Kumuuliza imekuwaje akaniambia mbona tuko wengi tuu..nikaachwa mdomo wazi. Hivyo kufeli CBE si kitu cha ajabu pale hakuna elimu ni ubraza men tu na usista du.

Nashauri vyetu vyao vihakikiwe na Necta kabla ya kuruhusiwa kuingia madarani.
 

Mnyama hapo unaongea kwani mara zote nifikapo pale watu wanafanya mambo yao tu na hakuna sign yeyote ya seriousness kwenye masoma.

hao walimu nawapongeza kwa kuwakamata tena, na huu ujinga wakila ukamatwapo umeonewa umeanza lini ? na kwa nini uonewe wewe tu na si wengine? tusichanganye biashara na elimu ¨ EDUCATION IS NOT A BUSINESS¨ tunakoelekea tanzania/vyuo naona vinageuza elimu kuwa biashara.

mimi ni lecturer na naona seriousness ya wanafunzi wa sasa. ni tofauti kabisaaa na tulivyokuwa sisi six/seven years back at UD.

nawakilisha
 


Ni kwamba pale sasa amepelekwa mkuu wa chuo mpya ambaye yupo serious na academics, na amefanya safishasafisha ya kutosha ikiwemo kuajiri walimu wapya na walimu vihiyo kibao kutimuliwa. Sasa shule imeanza kuwa shule hasa na ndio maana unaona supp zimezagaa. Mimi nafikiri wasilegeza kamba maana CBE ni chuo kikubwa ambacho kiliharibiwa na wahuni tu kwa kukifanya kijiwe cha watu walioshindwa shule sehemu zingine. We need bold people as the new CBE principal is doing.
 
Hakuna mwalimu anaependa mwanafunzi wake afeli hata kama yupo labda kwa chuki binafsi yap aweza felisha lakini sio mass failure. Uwezo wa wanafunzi hapo CBE ni wa wasiwasi hasa ukichukulia pesa inaongea pale huna pesa hupati addmission kwa hiyo haya ndio tungetarajia kama kuna uongozi imara unaofata sheria kama uliopo sasa. Hongera uongozi wa chuo kwa kuwa serious sasa maana hao jamaa wanaopasishwa bila kugonga vitu ndio wakipata uongozi wanaingia mikataba ya kutumaliza afathali mmalizane nao hapohapo. Ubishoo wapi na wapi na shule nendeni FOE mkaone vijana walivyotingwa wanaonesha userious ktk masomo japo shule yao ni ngumu na vifaa ni duni. Ingekuwa ni hawa FOE ndio wanachukua hayo masomo yenu hapo CBE ni Nyumba tu(A) na sio mgomo. Lakini msijali watawabeba tu pesa si mnayo na wazazi wenu ndio wako ktk system
 
Wachukue mfano wa FOE [CoET] pale UDSM, wenzao masomo yakiwa yamebana wanaanzisha Kunji tu ili mitihani isifanyike kwa wakati uliopangwa...

Mkuu, FOE vijana walikuwa hawagomi kwa kuwa shule imekuwa ngumu. Bahati mbaya sana issues zilikuwa zinatokea wakati mitihani imekaribia.

Habari ya wanaCBE kukamatwa inanikumbusha kipindi flani faculty ya Laws pale UD kulikuwa na ubishoo mwingi sana na dean aliyekuwepo alikuwa serious ile mbaya na watu wakawa wanapewa discos na sup kama kawa until when walipogundua kwamba kuwa lawyer lazima uingie darasani.

Lazima ifike wakati vyuo vyetu viheshimiwe na isiwe kimbilio la waliofeli secondary na vyuo vingine
 

Umenikumbusha mbali sana kuhusu kunji, kuna wakati jamaa walianzisha mgomo kwa kisingizio cha vyoo vichafu, ilikuwa 4 days kabla ya mitihani na lengo hasa ni kupata muda wa kujiandaa maana jamaa walikuwa wananpekeshwa lecture inaisha leo mtihani unaanza kesho. sasa hawa CBE wanatia timu uwanjani, halafu mpira umeisha wamepigwa bao ndio wanagomea mechi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…