CBT na KCJE zieleze tani elfu 50 za salfa ya unga ziko wapi?

CBT na KCJE zieleze tani elfu 50 za salfa ya unga ziko wapi?

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
Mnamo mwezi Aprili 2026 Umoja wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Korosho nchini (KCJE) na Bodi ya Korosho Tanzania walieleza kuwa wanatarajia kusambaza zaidi ya tani elfu 50 za Viuatilifu vya unga (Sulphur) msimu wa kilimo 2026/2027 kwa wakulima wa korosho nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa tarehe 26 Aprili 2026 Mkoani Mtwara, ilizinukuu KCJE na CBT zikieleza kuwa tayari kulikuwa na viuatilifu ambavyo vipo nchini huku vingine vikiwa vinatarajiwa kuendelea kuingia, ikiwa ni pamoja na tani elfu 30 za Salfa ya Unga.

Hata hivyo, taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali wakiwepo wakulima wa Korosho zinaeleza kuwa mpaka sasa kiasi cha viuatilifu viliyofika hasa Salfa ya unga ni vichache ilikinganishwa na maelezo yaliyokuwa yametolewa awali.

Maswali ya kujiuliza ni je, ni kweli kulikuwa Salfa ya unga iliyokuwa imebaki? Ilikuwa kiasi gani? Ilisambazwa wapi? Kuna kiasi gani ambacho kimeingizwa nchini mpaka sasa? Kiasi ambacho hakijaagizwa fedha zake ziko wapi?
 
Ukiwa Mkulima wa hayo mazao sijui wanaita ya Kimkakati ukawa 100% unategemea inputs za bure kutoka Kwenye hivyo vyama vya ushirika na bodi utahangaika na kufeli kabisa. Hivyo vyama vya ushirika wanawaza makato yao tu
 
Hili jambo linafikirisha sana, na cha kushangaza ni kwamba kwa mara ya kwanza wabunge wa miko inayolima Korosho wamekaa kimya huku wakijua madudu yanayoendelea kwenye issue nzima ya uagizaji wa pembeje msimu 2026/2027.

Na ndio maana kuwa kuna tuhuma za wabunge wenye ushawishi katika mikoa ya korosho kuhongwa kiasi cha fedha na Bodi ya Korosho Tanzania, ili wanyamaze mambo yapite ikiwa ni sehemu ya CBT kujisafisha kutokana na mambo mbalimbali ya ubadhiri yanayoendelea kuripotiwa.

Bodi ya Korosho inauelewa mpango mzima, lakini haiwezi kutoka hadharani kusema chochote kuhusu pembejeo kwa sababu ukweli wanaujua juu ya data halisi na zile za kupikwa wanazozitagaza mara kwa mara wakishirikiana na KCJE.
 
Mhe.Rais Dkt.Samia ikimpendeza afanye uchunguzi kupitia vyombo vyake mbalimbali atabaini ukweli wa madudu mengi yanayoendelea ndani ya CBT yakianzia kwa Mkurugenzi Mkuu, Bodi ya Wakurugenzi, baadhi ya watendaji hasa kwenye idara za Kilimo,Ubanguaji,Manunuzi nk.

Mkurugenzi Mkuu ameiweka Bodi ya Wakurugenzi mfukoni, hakuna anayeweza kumueleza au kumkanya kwa sababu anajua namna ya kula nao, ndio maana kumekuwa na madudu yasiyoelezeka kwa sababu hakuna wa kuyakeme.
 
Bodi ya Korosho Tanzania ndiyo inayosimama badala ya Serikalini, ndiyo Taasisi iliyopewa mamlaka ya kisheria ya kusimamia sekta ya Korsho nchini, lakini cha kushangaza ni kwamba KCJE ndio inatoa takwimu za uagizaji wa pembejeo ambazo hazipo CBT.

Kama kuna shida au ubadhirifu wowote kwenye uagizaji na usambazaji wa pembejeo, basi CBT inatakiwa kuwa ya kwanza kuwajibika kwa sababu ndiyo iliyotoa fedha za Serikali na kuwapa KCJE kwa ajili ya uagizaji na usambazaji wa pembejeo msimu 2026/2027.

Sasa unaweza kujiuliza, inawezekanaje Serikalini kupitia CBT itoe mabilioni ya fedha za pembejeo, alafu kusiwe na ufuatiliaji na utoaji wa taarifa kuhusu mwenendo wa uagizaji na usambazi wa pembejeo?

Je kama Pembejeo zipo, au zimechelewa kwa sababu ambazo zinaelezeka, ni kwanini CBT inatuhumiwa kuwa iliwahonga baadhi ya wabunge na wakuu wa Wilaya zinazolima Korosho ili kuzima kelele za wakulima waliokuwa wanalalamikia ukosekanaji wa Salfa ya unga?je ilikuwa inataka kuficha nini?

Ndio maani bado tunasisitiza kuwa kuna haja ya Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kwanza kuivunja Bodi ya Wakurugenzi ya CBT, kumuwajiisha Mkurugenzi Mkuu wa CBT, kuivunja KCJE na shughuli zote za uagizaji na usambazaji zifanywe na Bodi ya Korosho Tanzania baada ya kuchaguliwa kwa Bodi mpya ya Wakurugenzi na kuajiriwa Mkurugenzi Mkuu mwingine kwa sababu aliyekuwepo sasa ameshindwa kuisimamia Taasisi.
 
BODI YA KOROSHO HAIWEZI KUKWEPA LAWAMA UHABA WA SALFA YA UNGA

Aprili 2026 Umoja wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Korosho nchini (KCJE) na Bodi ya Korosho Tanzani walitangaza kuanza kusambaza zaidi ya tani 51 za Viuatilifu vya unga (Sulphur) msimu wa kilimo 2026/2027 kwa wakulima wa korosho nchini.

Katika taarifa rasmi, CBT na KCJE walieleleza mbele ya vyombo vya habari kuwa tayari kulikuwa na tani elfu 16 za Salfa ya Unga ambauo iko nchini, na kiasi kingine kitaagizwa.

Hata hivyo wakulima wa Korosho katika Wilaya za Tandahi,Newala,Masasi,Tunduru, Nachengwea na Ruangwa,wanaeleza kuwa mpaka sasa kiasi cha ni vichache ilikinganishwa na maelezo yanayotolewa na Bodi ya Korosho Tanzania.

Vilevile inaelezwa kuwa kuna udanganyifu mkubwa unaofanywa katika mpango huo wa uagizaji na usambazaji wa viuatilifu hivyo, huku taarifa zikisema kuwa viongozi wa Bodi ya Korosho ya KCJA wapo nyuma ya mpango huo muovu.

Kulikuwa Salfa ya unga iliyokuwa imebaki?ilikuwa kiasi gani?ilisambazwa wapi?Kuna kiasi gani ambacho kimeingizwa nchini mpaka sasa?ni kiasi gani ambacho hakijaagizwa mpaka sasa?kitaagizwa lini wakati muda unaisha? fedha zake ziko wapi?
 
Nikiwa kama mdau wa sekta ya Korosho hapa nchini, ambaye nimezaliwa na kulelewa kwa zao hili la Korosho, kwa maoni yangu tunapaswa kuheshimu hatua kubwa inayopigwa katika kusimamiwa na kuendelezwa kwa zao hili, ambalo limekuwa likitumika na baadhi ya watu vibaya kwa maslahi yao binafsi ili kuvuruga mipango na mikakati iliyopo bila kuangalia kwa upande mwingine ambao kumekuwa na jitihada kubwa katika kuboresha maslahi ya wakulima.

Nitakuwa mchoyo wa Fadhila nisipoandika maoni haya kwa kueleza kwa uchache ambayo nayafahamu yaliyosaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa baadhi ya kero ambazo zilikuwa zinawakabili wakulima wetu, kwa kipindi cha zaidi ya miaka minne, tumeshuhudia kwa kiasi kikubwa kuondoka kwa kilio cha wakulima wa zao la korosho ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa pembejeo kwa wakati, vifungashio kwa wakati na hata malipo yao kwa kwa wakati.

Mchango huu kwa kiasi kikubwa umechangiwa na kuanzishwa kwa Taasisi ya Korosho Cooperative Joint Enterprise Limited (KCJE), ambayo ni Taasisi iliyosajiliwa na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania chini ya kifungu cha 33 cha Sheria ya Vyama vya Ushirika Sura ya 211 Pamoja na marekebisho yake ya Mwaka 2025 na Kanuni zake za mwaka 2015.

Pamoja na mambo mengine Taasisi hii imekuwa ikifanya shughuli kubwa ya kuratibu na kusimamia ununuzi na usambaji wa pembejeo, kuratibu na kusimamia usambazaji mfumo wa Mizani za kidijitali kwenye Vyama vikuu vya Ushirika, na kuratibu na kusimamia ununuzi wa magunia kwenye vyama hivyo pia, na taasisi hii tangu ianzishwe ina takribani miaka minne tu, lakini tumeona mabadiliko makubwa ambayo pia yamechangia kuongezeka kwa uzalishaji wa zao hilo kutoka tani 240,000 hadi tani 618,000.

Nikiiyaelekeza maoni yangu kwa upande wa suala la usambazaji pembejeo, kutokana na taarifa za uhakika nilizonazo ni kuwa tayari zaidi ya tani 15,000 za Salfa ya Unga zimeshasambazwa kwa wakulima wa Korosho nchini, huku usambazaji huo ukiwa unaendelea.

Salfa hiyo ya unga ilisambazwa kutokana na kuwa na tani 16,000 zilizokuwa zimebaki msimu 2025/2026, baadae KCJE iliagiza tani 10,000 na kumaliza kiasi kingine cha tani 5,000, huku viuatilifu vya maji lita milioni 2 vikipokelewa pamoja na salfa hizo mwaka huu.

Kuhusu Viuatilifu vya maji, ni kuwa tayari zaidi ya lita milioni 3.2 zimesambazwa kwa wakulima msimu 2026/2027, ambayo ni mara mbili zaidi ya kiasi cha lita milioni 1.5 zilizokuwa zimekusudiwa kusambazwa awali.

KCJE ililazimika kuongeza kiasi hicho cha viuatilifu vya Maji, baada ya kuona kutakuwa na ucheleweshaji wa salfa ya Unga kutokana na mzozo uliokuwa unaendelea katika nchi za mashariki ya kati ambako ndipo salfa ya unga inapotokea, ambao ulisababisha bei kuongezeka maradufu.

Kwa hiyo inawezekana kabisa kukawa na changamoto za hapa na pale katika mchakato mzima wa uagizaji na usambazaji wa pembejeo msimu 2026/2027 lakini KCJE imejitahidi sana katika kuhakikisha kuwa wakulima wanafikiwa na pembejeo hususan za maji ambazo kulikuwa na bakaa ya wastani wa lita milioni 7, katika msimu uliopita, na kusaidia kuwafikia wakulima kwa wakati hali ambayo imepunguza usumbufu kwa kiasi kikubwa, na ikumbukwe kuwa nchi yetu haina kiwanda cha kuzalisha pembejeo zinazotumika na zao hili, hivyo jitihada za watendaji ndio zilizotumika ili kukabiliana na changamoto hizo, kwani wengi wetu tunafahamu yanayoendelea huko mashariki ya kati.

Ni vema pia kujua kuwa tangu KCJE ianze kuagiza pembejeo, kumekuwa na mtiririko mzuri wa ongezeko la viuatilifu vinavyowafikia wakulima wa korosho nchini tena kwa wakati, hivyo kuongeza uzalishaji.

Takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha misimu mitano kuanzia 2021/2022 hadi 2025/2026, jumla ya lita 11,002,730 za viuatilifu vya maji zimesambazwa, huku sulphur ya unga ikifikia tani 153,291.

Katika msimu wa 2021/2022, zilisambazwa lita 1,497,354 za viuatilifu vya maji na tani 13,562 za sulphur ya unga. Kiasi hicho kiliongezeka katika msimu wa 2022/2023 hadi lita 2,683,682 za viuatilifu na tani 15,014 za sulphur.
Msimu wa 2023/2024 ulirekodi usambazaji wa lita 1,989,238 za viuatilifu vya maji na tani 39,275 za sulphur, kabla ya kuongezeka zaidi mwaka 2024/2025 ambapo lita 2,689,581 za viuatilifu na tani 41,263 za sulphur zilisambazwa.

Katika msimu wa 2025/2026, jumla ya lita 2,142,875 za viuatilifu vya maji zilisambazwa, huku sulphur ya unga ikifikia kiwango cha juu cha tani 44,177.

Ongezeko hilo la usambazaji wa sulphur linaonesha kuendelea kwa jitihada za kuhakikisha wakulima wanapata pembejeo muhimu kwa wakati, jambo linalolenga kudhibiti visumbufu na magonjwa ya mikorosho na hatimaye kuongeza uzalishaji wa korosho ghafi.

Nimalizie kwa kuomba wadau wote wanaouhisika kwenye mnyororo wa Sekta ya Korosho nchini, kuunga mkono juhudi zinazofanywa na KCJE katika kukuza na kuendeleza zao la Korosho na pale kunapotokea changamoto basi kuomba ufafanuzi kutoka kwa vyanzo sahihi ili kupata taarifa sahihi kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika.

Na kama kuna mtu yoyote mwenye jambo na ushauri wowote kwa ajili ya kuboresha zaidi, ni vyema ajitokeze hadharani au kuwasiliana na watendaji wa taasisi hiyo ili kushauri naamini KCJE itakuwa tayari kupokea na kufanyia kazi ushauri wowote badala ya kujificha.
Asante.
 
Mnamo mwezi Aprili 2026 Umoja wa Pamoja wa Vyama Vikuu vya Korosho nchini (KCJE) na Bodi ya Korosho Tanzani walieleza kuwa wanatarajia kusambaza zaidi ya tani elfu 50 za Viuatilifu vya unga (Sulphur) msimu wa kilimo 2026/2027 kwa wakulima wa korosho nchini.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa tarehe 26 Aprili 2026 Mkoani Mtwara, ilizinukuu KCJE na CBT zikieleza kuwa tayari kulikuwa na viuatili ambavyo vipo nchini huku vingine vikiwa vinatarajiwa kuendelea kuingia, ikiwa ni pamoja na tani elfu 30 za Salfa ya Unga.

Hata hivyo, taarifa kutoka katika vyanzo mbalimbali wakiwepo wakulima wa Korosho zinaeleza kuwa mpaka sasa kiasi cha viuatilifu viliyofika hasa Salfa ya unga ni vichache ilikinganishwa na maelezo yaliyokuwa yametolewa awali.

Maswali ya kujiuliza ni je, ni kweli kulikuwa Salfa ya unga iliyokuwa imebaki? Ilikuwa kiasi gani? Ilisambazwa wapi? Kuna kiasi gani ambacho kimeingizwa nchini mpaka sasa? Kiasi ambacho hakijaagizwa fedha zake ziko wapi?
MADAI YA KUFUNGWA KWA KIZUIZI CHA MKURANGA ILI KUPITISHA KOROSHO KIHOLELA

Kuna taarifa zinaeleza kuwa mwanzoni mwa mwaka 2026, Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania akishirikiana na Mkurugenzi Mkuu walitumia nafasi zao kuagiza kufungwa kwa Kizuizi cha Mkuranga Mkoani Pwani, ambacho kilikuwa kimewekwa na Bodi ya Korosho Tanzania kwa lengo la kudhibiti usafirishaji wa korosho zilizobanguliwa bila vibali na bila kulipiwa tozo zinazozotambulika kisheria.

Inadaiwa kuwa Mwenyekiti alimwelekeza Mkurugenzi Mkuu kufunga kizuizi hicho kwa madai kwamba maafisa waliokuwa wanasimamia walikuwa wakila rushwa kupitisha mizigo ya wafanyabiashara jambo ambalo lilihitaji kufanyiwa uchunguzi.

Katika misimu ya Korosho 2024/2025 na 2025/2026, inadaiwa kuwa Mwenyekiti alikuwa akitumia baadhi ya vijana kununua na kusafirisha korosho zilizobanguliwa bila kuwa na vibali vinavyotolewa na Bodi ya Korosho Tanzania ambayo anaisimamia yeye.

Inadaiwa kuwa kupitia watu hao, mizigo ya korosho yenye uzito kati ya kilo 500 hadi kilo 800, na wakati mwingine kufikia takribani tani 1.5, kila siku ilikuwa ikisafirishwa bila kufuata taratibu zinazohitajika.

Zipo taratibu zinazotakiwa kutumika katika usafirishaji wa korosho zilizobanguliwa, ambapo msafirishaji anapaswa kulipa tozo zinazohusika, ikiwemo tozo ya Halmashauri inayokadiriwa kuwa shilingi 300 kwa kila kilo, na kuwasilisha risiti husika kama sehemu ya nyaraka za kuombea kibali kutoka Bodi ya Korosho Tanzania.

Hata hivyo, inasemekana kuwa utaratibu huo haukuzingatiwa katika mizigo iliyosafirishwa kutoka Mtwara Kwenda Dar Es Salaam, hali ambayo inawezekana kuwa imesababisha upotevu wa mapato ya Serikali za Mitaa na Serikali kwa ujumla, pamoja na kuathiri usawa wa ushindani miongoni mwa wafanyabiashara wanaofuata taratibu zilizowekwa.

Kuhusu kizuizi cha Mkuranga ni kwamba, kabla ya kufungwa kulikuwa na maafisa wa Bodi ya Korosho Tanzania waliokuwa wakifanya kazi katika eneo hilo kwa kushirikiana na maafisa wa Polisi wa Wilaya ya Mkuranga katika ukaguzi wa mizigo inayopita katika eneo hilo.

Inadaiwa kuwa katika utekelezaji wa majukumu yao, maafisa hao walikuwa wakikamata mizigo ya korosho iliyokutwa haina vibali vinavyohitajika na kuchukua hatua stahiki, ikiwemo kutoza faini kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu za Bodi ya Korosho Tanzania.

Hata hivyo baadhi ya mizigo iliyokamatwa ilikuwa ikihusishwa na watu waliokuwa wakifanya kazi kwa niaba ya Mwenyekiti, na baada ya taarifa za kukamatwa kwa mizigo hiyo kuwafikia wahusika, inadaiwa kuwa Mwenyekiti alichukua hatua za kuagiza kufungwa kwa kizuizi hicho, jambo ambalo liliondoa utaratibu wa udhibiti uliokuwa umewekwa ili kuzuia usafirishaji wa korosho bila vibali.

Kwa kuzingatia uzito wa madai hayo, yafuatayo yanahitaji kufanyiwa uchunguzi na mamlaka husika:

Uthibitisho wa umiliki wa mizigo ya korosho iliyokamatwa katika Kizuizi cha Mkuranga na maeneo mengine.

Rekodi za vibali vya usafirishaji vilivyotolewa na Bodi ya Korosho Tanzania katika misimu ya 2024/2025 na 2025/2026.

Rekodi za malipo ya tozo za Halmashauri na Serikali zinazohusiana na mizigo hiyo.

Rekodi za mizigo iliyokamatwa na kutozwa faini katika Kizuizi cha Mkuranga.

Taarifa za maafisa wa Bodi na Polisi waliokuwa wakifanya kazi katika kizuizi hicho.

Maelekezo au mawasiliano yaliyotolewa kuhusu kufungwa kwa Kizuizi cha Mkuranga, ikiwemo sababu rasmi za uamuzi huo.

Uhusiano kati ya Mwenyekiti na watu waliodaiwa kununua au kusafirisha korosho kwa niaba yake.

Kufanyika kwa uchunguzi wa kina ili kubaini kama kulikuwa na mgongano wa maslahi, matumizi mabaya ya madaraka au ukiukwaji wa taratibu za biashara ya korosho.


Hata hivyo kwa kuwa madai yaliyotajwa hapo juu ni mazito na yanahusu uadilifu wa uongozi, usimamizi wa Sekta ya Korosho na ulinzi wa mapato ya Serikali,yanapaswa kuchunguzwa na kuthibitishwa kwa ushahidi wa nyaraka, kumbukumbu za biashara, taarifa za maafisa waliohusika na uchunguzi huru wa mamlaka husika kabla ya kufikia hitimisho kuhusu uwajibikaji wa mtu yeyote.

Kwa hiyo, ni jukumu la mamlaka yenye dhamana ifanye uchunguzi wa kina na wa haki kuhusu madai haya, hususan kuhusu umiliki wa mizigo, vibali, malipo ya tozo, mizigo iliyokamatwa na mazingira ya kufungwa kwa Kizuizi cha Mkuranga, ili kubaini ukweli na kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria na taratibu.
 
CBT kupitia Mkurugenzi wake Mkuu inamhujumu Rais Dkt.Samia ambaye amejitolea kwa dhati kuendeleza sekta ya Korosho nchini kwa kuboresha mazingira ya Kilimo na Masoko ambavyo vimeonesha tija kubwa kwa wakulima wa Korosho tangu aingie madarakani.

Ubadhirifu ambao umekuwa ukitajwa katika mradi wa Kongani la Viwanda Halmashauri ya Mji Nanyamba, matumizi mabaya ya Ofisi, ugawaji wa Tenda usiofuata taratibu za manunuzi, usimamizi mbovu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Korosho nk. ni miongoni mwa mambo yanayorejesha nyuma kwa makusudi juhudi za Mhe.Rais Dkt.Samia.

Wakati Serikali kupitia Wizara ya Kilimo ikijitahidi kupeleka fedha CBT kwa ajili ya usimamizi wa Tasnia ya Korosho nchini, Mkurugenzi Mkuu akishirikiana na watendaji wasiozidi wawili tu ndio wenye sauti ya mwisho katika mambo yote yanayohusu Taasisi hiyo ya umma.

Jambo la kushangaza ni kuwa Bodi ya Wakurugenzi ambayo kimsingi ndio ilitakiwa isimamie utendaji, nayo imewekwa mfukoni na Mkurugenzi Mkuu, hivyo bodi hiyo kuwa kama geresha tu lakini kimsingi haifanyi kazi yoyote mpaka Mkurugenzi aridhie.

Wakati flani miaka ya 2000-2025 baadhi ya wafanyakazi waadilifu walijaribu kwashirikisha wabunge kujua madudu yaliyokuwa yanaendelea, ili wawasaidie kupaza sauti hata Bungeni, lakini wabunge hao waliishia kuwazunguka na kurudi kwa Mkurugenzi kuchota fedha huku wafanyakazi wakifanyiwa uonevu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuhamishwa vituo vya kazi.

Siku ikiundwa tume ya kuchunguza madudu ya CBT, alafu ikachunguza kutaka kujua uhamisho wa wafanyakazi uliofanywa katika kipindi cha miaka 6 iliyoipita, itagundua madudu ya kutisha na uonevu mkubwa uliofanywa kwa wafanyakazi hao kwa sababu tu walikuwa against Mkurugenzi mkuu ambaye hataki watu wanaojua wala kumpinga isipokuwa wale machawa ndio wanaokula maisha ndani ya CBT.

Sasa katika hali kama hiyo, tunawezaje kusema Taasisi inaunga mkono juhudi za Mhe.Rais wakati hakuna inachotekeleza kwa maslahi ya wakulima na badala yake kila kitu kinafanyika kwa maslahi ya Mkurugenzi mkuu na timu yake?

Tunajua wakati huu Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan anaomboleza msiba wa mwenza wake aliyefariki hivi karibuni, lakini ni dhahiri kuwa vyombo vyake vya ushauri vinaendelea na kazi na vitakuwa vinakusanya hizi taarifa na ipo siku tu CBT itakombolewa.

As-salamu alaykum
 
UZEMBE WA FRANCIS ALFRED MKURUGENZI MKUU BODI YA KOROSHO TANZANIA MZIGO KWA WAKULIMA WA KOROSHO

Takribani miaka 8 sasa Idara ya Kilimo inayosimamia pamoja na masuala mengine ununuzi na usambazaji wa pembejeo za wakulima kwa miaka yote hiyo imekuwa ikisimamiwa na mtumishi wa mkataba huku Mkurugenzi wa Idara hiyo akiwa amehamishiwa Tawi la Morogoro tangu mwaka 2018.

Pamoja na kwamba wakati Bw. Francis Alfred wakati anateuliwa kushika nafasi ya Mkurugenzi Mkuu alikuta Mkurugenzi wa Kilimo yupo Morogoro, alipaswa kumrudisha Makao Makuu ili asimamie Idara ya Kilimo lakini hakufanya hivyo na hakuwai kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo.

Kutokana na Idara ya Kilimo kukosa Mkurugenzi wa kuisimamia leo hii wakulima wa Korosho wanadaiwa shilingi Bilioni 468 gharama za pembejeo ambazo walikuwa wakitumia huku wakielezwa ni pembejeo za ruzuku hivyo ni bure kutoka kwa
serikali yao.

Hii ilidhihirika kupitia katika mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa Korosho tarehe 27 Agosti 2026 mkoani Morogoro.

Mkurugenzi Mkuu aliwasilisha taarifa ya utekelezaji na kueleza kuwa kila mkulima anatakiwa kukatwa shilingi 250 kwa kila kilo kwa miaka 3 mfururizo mpaka kumaliza deni hilo.

Suala hili limebua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau hasa wakulima wakipinga kukatwa fedha hizo wakati walikuwa wanajua pembejeo walizokuwa wanapata ni za ruzuku.

Pamoja na uwasilishaji wa taarifa ya deni hilo, Naibu Katibu Mkuu aliyeiwasilisha wizara katika mkutano huo alionesha kustushwa na taarifa hiyo kwakuwa hata wizara haikuwa na taarifa ya deni hilo.

Vile vile hata wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi nao walionesha kutokuwa na taarifa ya deni hilo kupitia vikao vyao vya kawaida.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kwa muda mrefu pembejeo hizo zilikuwa zinanunuliwa bila kufuata utaratibu na kusambazwa kiholela bila usimamizi dhabiti.

Pembejeo nyingi zimekuwa zikiibiwa na mpaka kuuzwa nje ya nchi jirani kwa sababu ya kukosa usimamizi.

Aidha, kumekuwepo na taarifa za wizi wa pembejeo hizo kupitia mifumo na kuna kesi nyingi karibia kila wilaya zikishirikisha watumishi na viongozi wa Ushirika.

Hivi karibuni Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongoro alimwagiza Mkurugenzi Mkuu Bw. Francis Alfred kuhakikisha anaweka mpango wa kupulizia korosho za wakulima ili kupunguza matumizi hole ya viuhatilifu kwa wakulima.

Hata hivyo maagizo hayo hakuwahi kuyatekeleza kwasababu hakuwahi kuwa na Mkurugenzi wa Idara ya kilimo badala yake amekuwa akimtumia mfanyakazi wa makataba bw. Juma Yusuph ambaye hana uwezo wa kusimamia Idara hiyo hata kusimamia usabazaji wa pembejeo hizo.

Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba mfanyakazi huyu wa mkataba ndiye amekuwa Mwenyekiti wa Tenda wa Bodi tangu wakati Bodi inanunua pembejeo hizo.

Kwa ujumla huu ni uzembe wa Mkurugenzi Mkuu kwa kushindwa kumrudisha Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo hadi amestaafu mwezi Julai mwaka huu 2026.

Pamoja na kustaafu kwa Bw. Silomba aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo, bado Mkurugenzi Mkuu hajachukuwa hatua zozote kumpata Mkurugenzi mwingine kwakuwa anataka kumfanya huyu Bw. Juma Yusuph kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo wakati hana sifa ya kuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo.

Kwanini hawezi kuteua Maafisa waandamizi waliyopo Idara hiyo ambao mmoja wapo anaweza kukaimu nafasi hiyo au hata kuomba kwa katibu Mkuu Utumishi katika ofisi ya Rais kuhamishia hapo Mkurugenzi anayeweza kusimamia Idara hiyo ili kupunguza hasara kwa wakulima na Serikali kwa ujumla?

Taarifa za CAG zinaonesha Bodi imeshindwa kusimamia ununuzi wa pembejeo kwa muda mrefu ambapo unakuta lita moja mfano ni elfu 5 kwa tenda aliyoshinda lakini wakati wa kuwasilisha lita hiyo baada ya manunuzi inaonesha elfu 10 huku zikitolewa sababu nyingi mara ohoo gharama zilipanda kwasababu ya mgogoro wa Mashariki ya Kati na sababu kikao.

Badala ya Bodi kusimamia ripoti ya tenda aliyoshinda inapokea na kuendelea kuongeza deni mpaka hii leo bilioni 468 ni mzigo kwa mkulima.

Hivyo jumla ya tozo kwa kila kilo mnadani itakuwa shilingi 608 msimu huu 2026/2027 badala ya 468 ya msimu 2025/2026. Hii ina maana kwamba bei ya mkulima inaenda kupungua kwasababu kila shilingi inayoongezeka kwa mnunuzi anapungua kwa bei ya mkulima.

Bei ya mkulima ikipungua maanake uzalishaji unaenda kupungua na hatimaye kushindwa kufikia uzalishaji wa tani milioni 1 kwa mwaka 2030.

Katika hili Mkurugenzi Mkuu Bw. Francis Alfred hana budi kuwajibika kwa uzembe, matumuzi mabaya ya madaraka mpaka hakashindwa kumrudisha makao makuu Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo mpaka Serikali ikapata hasara ya ongezeke gharama za pembejeo tofauti na uhalisia wake.

Ngoja tusubiri kauli ya Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kama wakulima hawa waendelee kupata hasara na serikali kwa ujumla au achukuliwe hatua huyu Mkurugenzi Mkuu ambaye anaonekana kuleta mazoea kutokana na miaka 8 aliyokaa katika cheo hicho huku bila kuwa na faida yoyote.
 
CCM MTWARA SASA HAINA IMANI NA BODI YA KOROSHO TANZANIA

Baada ya malalamiko ya muda mrefu juu ya utendaji na usimamizi wa CBT, hatimaye sasa Mwenyeki wa chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mtwara mwalimu Said Nyengedi ameeleza kuwa hana imani na bodi ya korosho kufuatia kukamatwa kwa tani 136 za korosho chafu.

Mwalimu Nyengedi ameyasema hayo September 25,2026 akiwa kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa huo (RCC) huku jambo ambalo limeibua mijadala kutoka kwa wananchi na wadau wa tasnia ya Korosho nchini.

Wananchi hao wanahoji kama imefikia hatua hata Chama Tawala halina imani tena na Taasisi hiyo ya umma, inakuwaje Mkurugenzi wake mtendaji na Bodi ya Wakurugenzi waendelee kuwepo kwenye nafasi zao?

Kwa tuhuma hizi nzito kutoka kiongozi wa CCM Mkoa ambao ndipo yalipo makao makuu ya CBT, ni dhahiri sasa kuwa Mkurugenzi Mkuu Ndg.Francis Alfred na Bodi ya Wakurugenzi wanapaswa kuachia ngazi ili watu wengine wenye weledi wachukua majukumu hayo.

Wakati tuhuma zinatolewa ilionekana ni fitina,uongo,uzushi na hadi kufikia baadi ya watumishi kutengwa wakihisiwa kuwa wao ndio wanatoa taarifa hizo, sasa awamu hii mtoa taarifa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa, tuone kama na yeye atatengwa na Alfred.
 
Back
Top Bottom