KERO CCBRT Hospital hailipi wafanyakazi kwa wakati

KERO CCBRT Hospital hailipi wafanyakazi kwa wakati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Shytown

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2025
Posts
1,196
Reaction score
2,236
Kwa sababu hii ni taasis inayofanya Biashara, sina haja ya kuivua Nguo, Itoshe kusema; Kulipa wafanyakazi Mishahara katikati ya mwezi unaofuata sio sawa kabisa!.

Kama mnafirisika bora mtangaze, Serikali iwashike Mkono. Na kama mmeshindwa kusimamia mapato na matumizi, ombeni Serikali iwaletee wataalamu wa fedha

Msitangulize visingizio kuwa wafadhili wamepungua, kwani sio kweli kwamba; mapato hayatoshi hata kulipa mishahara ya wafanyakazi ambayo ni kipaumbele cha juu kabisa.

Lakini pia Inaonekana kunakitu hakipo sawa kwenye kusimamia mapato na matumizi kwa huu uongozi mpya kwani, uongozi wa awali uliomaliza muda wake ulifanya kazi kwa weledi bila hizi changamoto ikiwemo wafanyakazi kupanda madaraja pamoja na kuwa wafadhili walikuwa wana sua sua..... Ila hawa waliokasimishwa, wamefanya CCBRT ni shamba la bibi.
 
Uwa najisahau kabisa kwamba CCBRT ni private.
 
Bro hiyo ni taasisi binafsi, mapato yake hutokana na wafadhili na malipo ya wagonjwa.

Hata muhimbili, usifikiri vi elfu mbili mnavyolipa kupata dozi ya material, ndio vinalipa mishahara, hospitari za umma zote, bila ruzuku ya serikali kwa 80%, haziwezi kujiendesha
 
Wakati wanalipa kwa wakati mbona ukutulingishia sasa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Bro hiyo ni taasisi binafsi, mapato yake hutokana na wafadhili na malipo ya wagonjwa,
Hata muhimbili, usifikiri vi elfu mbili mnavyolipa kupata dozi ya material, ndio vinalipa mishahara, hospitari za umma zote, bila ruzuku ya serikali kwa 80%, haziwezi kujiendesha

Hivi unajua takriban 1/4 ya Hospitali za ngazi ya juu ni za private na zinalipa vizuri kwa kutegemea usimamizi makini wa mapato na matumizi (bila ufadhili wowote) Zingine zimefikia hata kuanzisha vyuo nk

Kwa Hospitali kama Muhimbili kwa sasa wagonjwa wanatumia Bima kwa takriban 60, na waliobaki wanalipa cash, japo najua wapo wale ambao hawana uwezo au magonjwa yenye msamaha. Inamaana kama Bima ya wote ingeshika kasi watu kama 90% wakawa na Bima; Serikali ingebakiza mchango wake pale pengine 20-30% ambao bado ni mkubwa sana
Ile ya kutegemea Serikali kwa 80% haipo tena; Kwa sasa wanajiendesha kwa mapato yao na wanategemea Serikali zaidi kwa Capital investment (Kununua vifaa tiba ambavyo havikuwepo nk) na kuchangia yale magonjwa yenye msamaha na wale wasiokuwa na uwezo ILA vifaa vikisha kuwepo ni jukumu la Hospitali kuviendesha.
Angalizo: Wagonjwa hawalipi vicent kama unavyofikiri; Siku ukilaza mgonjwa pale wiki moja ukalipa cash....ukija hapa utaandika vingine.....
 
Kwa sababu hii ni taasis inayofanya Biashara, sina haja ya kuivua Nguo. Itoshe kusema; Kulipa wafanyakazi Mishahara katikati ya mwezi unaofuata sio sawa kabisa!.

Kama mnafirisika bora mtangaze, Serikali iwashike Mkono. Na kama mmeshindwa kusimamia mapato na matumizi, ombeni Serikali iwaletee wataalamu wa fedha
Msitangulize visingizio kuwa wafadhili wamepungua, kwani sio kweli kwamba mapato hayatoshi hata kulipa mishahara ya wafanyakazi ambayo ni kipaumbele cha juu kabisa...

Lakini pia Inaonekana kunakitu hakipo sawa kwenye kusimamia mapato na matumizi kwa huu uongozi mpya kwani, uongozi wa awali uliomaliza muda wake ulifanya kazi kwa weledi bila hizi changamoto ikiwemo wafanyakazi kupanda madaraja pamoja na kuwa wafadhili walikuwa wachache pia
Pole sana, pesa inaonekana ipo lakini inaliwa na viongozi wa juu, posho perdm na safari za mara kwa mara. Vilevile wanachota pesa na kuendesha miradi yao binafsi.
 
UKWELI TUNATIA AIBU KWA WAZUNGU WALIOTUACHIA MRADI...
BADALA YA KUTAFUTA SOLUTION YA CHANGAMOTO, KUCHA KUTWA NI VISINGIZIO KUWA WADHAMINI WAMEPUNGUA.
SASA WADHAMINI WAKIPUNGUA, YALE MARUPURUPU MLIKUWA MNAJILIPA NA VIKAO VYA KILA KUKICHA VYA KUJILIPA MAMILIONI, NA SAFARI ZA MARA KWA MARA SI MPUNGUZE?
Hospitali nyingine kubwa za Binafsi zimefikia kuwaendeleza wafanyakazi wao ngazi ya Diploma, degree nk bure na hawana ufadhili wowote nyie bado unaongelea kulipa wafanyakazi?
Natamani kuanzia mwezi ujao (wa tano) kusiwe na hii changamoto ya kuitia aibu taasisi yenu yenye jina kubwa na linaloheshimika.
 
Back
Top Bottom