CCM 2022 na uchaguzi wake inarudi mikononi mwa matajiri, wananchi masikini ondokeni haraka wenye chama wanarudi

CCM 2022 na uchaguzi wake inarudi mikononi mwa matajiri, wananchi masikini ondokeni haraka wenye chama wanarudi

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Nimefurahi uchaguzi unaendelea ndani ya CCM ni hatari tupu, wale matajiri waliowekwa kando na Mh Mwendazake, sasa wanarudi Kwa kasi kasi ya 4G.

Ninaikumbuka sana CCM ya kabla ya Magufuli, ilivyokuwa tulip kuwa na macho tunakumbuka wenyeviti wa CCM mikoani walikuwa wafanyabiashara wakubwa sana ambao utajiri wao ulikuwa na shaka kubwa, wapo waliokuwa wauza madawa ya kulevya, wapo waliofanya biashara ila hawakulipa Kodi kabisa, nawakumbuka wengi hakika wale ambao tulikuwa tukifatilia habari za siasa tuliona kilichoendelea nchini Tanzania.

Fagio la chuma lilipitishwa na Mh Rais Magufuli Kwa kweli lilikuwa fagio hasa, Leo hii fedha zinaanza kununua madaraka tena. Je, nchi na CCM mnajitafakari?

Enyi nyinyi wenye kadi za CCM na hamna maisha jitafakarini wapi mnaenda?

Majizi yaliyofurushwa yanarudi Kwa kasi.
 
Hakikisha unaishi katika Mungu, Mtafute Mungu

Amtegemeaye Mwanadamu amelaaniwa
 
CCM hii ya Kinana!
CCM hii ya Nape!
CCM hii ya Makamba!

CCM hii ya Wanamtandao imeishajitambulisha Rasmi!

Ni kifo cha CCM pekee ndio kitawakomboa watanzania!

Mungu Sio Asumane!
 
CCM hii ya Kinana!
CCM hii ya Nape!
CCM hii ya Makamba!

CCM hii ya Wanamtandao imeishajitambulisha Rasmi!

Ni kifo cha CCM pekee ndio kitawakomboa watanzania!

Mungu Sio Asumane!
Chama chetu
 
Magufuli ndiye aliyebariki coming back ya Rostam Aziz na kwenda kuzinduwa Taifa gesi.

Mwendakuzimu ni Mwizi aliyetaka kuiba peke yake, hana utakatifu huo mnaompachika.
 
Muumba wa mbingu na nchi, sikia kuomba kwetu. Hiki chama kipoteze juu ya sura ya nchi yetu tukufu, hatukitaki TENA tumekichoka wametutesa wanao.

Wametupiga upofu wa maana hatuoni wala hatuna nguvu tena watanzania. Tuinue, tusaidie baba kwa njia zako mwenyewe wewe wajua. We have surrendered to you our Lord.
 
CCM hii ya Kinana!
CCM hii ya Nape!
CCM hii ya Makamba...
Wananchi tuamke sasa. Kwa uchaguzi huu mambo yako peupe. CCM si chama cha kutetea wananchi bali ni chama cha wafanyabiashara matajiri na kiko kwa ajili ya kutetea matajiri.

Tunahitaji viongozi makini pamoja na NGO kwenda vijijini kuwafundisha watu juu ya mustakabali wa nchi hii.NGos zisijikite mijini tu bali ziende kwa wananchi kuelimisha juu ya hatma ya nchi hii.
 
Katiba mpya ndio suluhisho la haya yote!
Tukiwa na katiba bora hatutangojea kiongozi wa kuja kuwafagia mafisadi bali katiba tu itaweka misingi ya kuchuja na kupata viongozi waadilifu tangu ndani ya vgyama hadi serikalini!
 
Back
Top Bottom