CCM, Angelina Mabula na Stanslaus Mabula, hizo nyumba zilizouzwa na Jiji la Mwanza zinaenda kuwa ajenda ya kwanza ya wapinzani. Mtatikiswa!

CCM, Angelina Mabula na Stanslaus Mabula, hizo nyumba zilizouzwa na Jiji la Mwanza zinaenda kuwa ajenda ya kwanza ya wapinzani. Mtatikiswa!

Kuna uozo au hakuna? Maana naona unazunguka tuu wala hujibu unachoulizwa..
Mara mgao, mara serikali yote imeoza, mara sijui nini..!! JIbu hoja acha longolongo
Unataka nijibu ishu ni kwamba tumeuza hivyo vichuguu viwili kwa bei nusu na order imetoka juu.... Haya unataka nini kingine.
 
Airport hiyo muda si mrefu inafumuliwa, mnajenga airport ndani mnaweka choo Cha shimo, aliyechora airport hajawahi kuchora airport yoyote zaidi ya ramani za vyoo vya manispaa, haijui hata Heathrow Airport anayosema aliigizia ramani, eti anadanlodi ramani ya jengo la airport, nyanoko
Na nyie mmeanza kujenga nini? Kila siku maneno tu ya kiswahili na huyo mkuu wa mkoa amekutana na watoto wa mjini zaidi yake.
 
Rais Samia amefungulia mikutano ya hadhara, na katika majiji ambayo Chadema wanajiwinda kuyadhibiti ni Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam. Wanatafuta ajenda nzito za kutikisa na kuwashika wananchi.

Arusha walifanya tukio, Sasa hivi wote wananyea debe, angalau wanaarusha wanaelewa hatua zimechukuliwa.

Kwa Jiji la Mwanza, Mkurugenzi wa Jiji na maafisa ardhi nao hawajachelewa kuwapa wapinzani ajenda.

Kuna habari kwamba Jiji la mwanza limeuza nyumba zake katikati ya Jiji kwa bei ya kutupa, bila kufuata taratibu.

Maeneo hayo yameuzwa wakati machinga mjini hawana maeneo ya biashara, wameenda kutupwa igoma nyamongolo huko ambako hakuna wateja, na kiloleli, na bila kuzingatia maelekezo ya Rais ya ubia kati ya sekta binafsi na Serikali, kiasi kwamba wangeongea na taasisi yoyote ile au mtu binafsi, akawekeza, wakawa wanakula faida, na eneo likabali lao.

Ni kwamba, wanamwanza wameibiwa.

Stanslaus Mabula, wewe ndio mbunge wa Nyamagana, bila shaka unalijua Jimbo linakuwaga la moto, hasa ukizingatia "sponsor kafa".

Angelina Mabula, wewe ndio Waziri wa hiyo ardhi ya serikali iliyouzwa, na uhamishaji miliki usingefanyika bila kupitia Ofisi za ardhi. Na sijui kwa nini kama mamlaka ya serikali inapotaka kuuza ardhi isitakiwe kupata Kibali Cha Waziri wa Ardhi au Waziri Mkuu! Au Rais! Uwepo udhibiti.

Mna kazi moja tu, kuirudisha ardhi hiyo, hatutaki Rais aanze kupata shida kupata kura za Mwanza wakati alishanyoosha mapito yake kwa miradi mikubwa ya maendeleo.

Ni hapohapo mwanza machinga aliyekuwa anauza ndizi, Jiji lilimwaga ndizi zake na kumpiga, Leo Jiji Lina ardhi hapohapo katikati ya mji linaiuza!

Njia moja tu, kurejesha hizo nyumba, na Kila Afisa aliyehusika apelekwe mahakamani, wanamwanza wataridhika wakiwaona wahusika wanapanda kizimbani, na kupelekwa gereza la Butimba.
Kama hoja ni hizi ikulu mtaisikia kwenye radio
 
Ishu ni mgao mkurugenzi alimpa mkuu wa mkoa gawio kidogo, sasa mkuu wa mkoa akakataa kuchukua akijua viwanja hivyo viwili vimeuzwa kwa bei kubwa zaidi kumbe ni bilion moja tu, sasa mkuu wa mkoa ndio akatata kumwaga mboga, na mkurugenzi akasema na yeye atamwaga ugali tena na kuufukia kwa kueleza uozo wote wa hili zee linaloitwa adamu malima
Duh! Kumbe hela ya mauzo wamegawana? Mh Mpango lishughulikie hili.
 
Na nyie mmeanza kujenga nini? Kila siku maneno tu ya kiswahili na huyo mkuu wa mkoa amekutana na watoto wa mjini zaidi yake.
Sasa Malima kazaliwa Dar, wewe umekulia milimani huko unajiita mtoto wa mjini?

Mtoto wa Waziri, tena wa fedha, Ofisi ya msajili wa hazina ilikuwa chini yake, alishakuwa Waziri, anajua taratibu zote za mali za serikali.
 
Kuna uozo au hakuna? Maana naona unazunguka tuu wala hujibu unachoulizwa..
Mara mgao, mara serikali yote imeoza, mara sijui nini..!! JIbu hoja acha longolongo
Inaonekana ozo upo, ndio maana Adam Malima alitaka apewe chochote ili kuficha huo uozo, bahati mbaya akakataa kwa kudhani kuna pesa mingi zaidi ya aliyotaka kupewa.

The best thing about this ni kwamba, inaonekana Malima kwa kudhani amekataa pesa aliyopewa atakuwa amejiweka kwenye nafasi nzuri, kumbe kuna wahusika wengine juu ambao watatakiwa kuhusishwa kwenye hili suala.
 
Hakika mkuu na mambo ndio yapo hivi hapa ofisini.
 
Unataka nijibu ishu ni kwamba tumeuza hivyo vichuguu viwili kwa bei nusu na order imetoka juu.... Haya unataka nini kingine.
Mnakiri mmeuza kwa nusu bei, na huyo wa juu mtasema ni nani, maana maafisa ardhi kwa Sasa Kila wakiuza kiwanja ca serikali wanasema amenunua ridhiwani kikwete na ndiye kawapa order, Kila mmoja atatoa hesabu yake
 
Back
Top Bottom