CCM asanteni sana kwa hii dancing style

CCM asanteni sana kwa hii dancing style

Tunawadhukuru kwa kweli mmetuonyesha dancing style ya kufua mtu. Yunaifanyia mazoezi na tutakutana rena ulingoni 2020.
Umeandika haraka mnoo "Tunawadhukuru,Yunaifanyia kazi,rena!!!!......punguza munkari..ila tumekuelewa
 
Kuna picha kubwa sana imeonekana,
1: CCM ya sasa haijui Siasa na figisu za Siasa, watu walikuwa wanajua CCM wanaiba lakini sio kwa Kiwango na ubabe wa aina hii, huu sasa sio wizi bali ni ujambazi, wizi wa kutumia nguvu

2: pamoja na jitihada anazojaribu kutuonyesha mtukufu Rais, bado watu hawamwelewi na hakubaliki, kwa kweli ni ajabu kabisa, pamoja na CCM na mtukufu Rais kujinasibisha kuwa wapo kwenye vita kali ya kupambana na Rushwa, Ufisadi, nk lakini kisiasa yupo chini sana sana

3: CCM imechokwa kila kona, kinachotumika sasa ni Ni nguvu ya vyombo vya usalama pamoja na watendaji wa Kiserikali (Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Tume ya Uchaguzi nk) kuwaweka CCM Madarakani.

Lakini CCM na vyombo vyake wakae wakijua hili wanalolifanya lina mwisho, na mwisho unaweza kuwa mzuri ndicho tunachokiomba, lakini pia mwisho unaweza kuwa mmbaya na wenye maafa makubwa sana,
Hao wanaoumizwa sio kama hawana ndugu zao wanajeshi, Polisi, nk itafika siku watu wanaotumainiwa na CCM kama ngai yao watagoma kwenda kuwapiga na kuwaumiza baba zao, mama zao, kaka zao, jirani zao nk.

Kwenye jeshi la Polisi ni unit ndogo sana inayopaswa kuwa na Silaha, sehemu kubwa ya jeshi ni TII SHERIA BILA SHULUTI, lakini kwa sasa jeshi lote la Polisi limekuwa sio tena jeshi la Kiraia bali ni kama special unit ya JWTZ

siyo kizazi hiki,.....kwa sasa itabidi muendelee kunung'unika na kulalamika kama kawaida...wanajua waswahili waoga sana kuingia barabarani..ni watu wa kulalamika tu...ndiyo maana wanafanya vyovyote ili washinde....labda mpaka kizazi cha tano
 
Tunawashukuru kwa kweli mmetuonyesha dancing style ya kufua mtu. Tunaifanyia mazoezi na tutakutana tena ulingoni 2020.
Wewe unaharibu chit-chat kwa kuleta siasa huku. Ulianza na thread ya kununua makada wa chama sijui sasa hivi unatuletea habari za dance ya ccm, kwanini usianzishe mada hizi jukwaa la siasa?
 
Eti mtamwaga damu ....hivi mnadhani ni rahisi eeeh kwenda kupigwa risasi huku unajiona kisa matumbo ya wengine .......endeleeni kuziendekeza siasa hizo mnaacha zitawafanya kua wehu
 
siyo kizazi hiki,.....kwa sasa itabidi muendelee kunung'unika na kulalamika kama kawaida...wanajua waswahili waoga sana kuingia barabarani..ni watu wa kulalamika tu...ndiyo maana wanafanya vyovyote ili washinde....labda mpaka kizazi cha tano

Wala haitaanzia kwenye Upinzani, itaanzia ndani ya CCM yenyewe na hawatakuwa na pakushika
 
Back
Top Bottom