Tetesi: CCM asili inamuandaa mgombea wake 2020

I cannot see kundi ambalo linaweza kumzuia Magufuli asirudi for the second term. Believe me no one has that courage inside ccm.
 
Hembu wasituchoshe wamwache baba wa watu atumikie vipindi viwili kama ni kweli nina imani hawatafanikiwa na watakuwa ni uchu wa madaraka tu si vinginevyo washindwe na walegee
 
Ila wewe jamaa una muda wa kutosha kukesha na kushinda JF na kuchangia kila mada kila muda. Halafu hapo hapo unadai hakuna hela mtaani...
 
Hizi ni ndoto za mchana.,kama JPM kawadhibiti upinzani na Muungano wenu wa UKAWA,unadhani kuna anayemuweza kwenye chama chake?,.Swali jingine la kujiuliza,unadhani mpaka wewe unaleta hizi story hapa JF hakuna mtu aliyeshafikisha Hii info kwa mwenyekiti wa chama?.,kuna jamaa kaongea kitu humu,mpaka 2020 kuna watu humu watakuwa wanaandika kichina humu kwa wanavyobanwa na JPM.Jifunzeni kufanya kazi halali,mambo yamebadilika sana.
 

japo mimi sina chama chochote ila nionavyo dr pondamali lazima amalize za mkwezi kwanza ndo wengine wachukue.. kama wakiweza kusimamisha mgombea tofauti basi itakuwa mageuzi ya kihistoria ndani na nje ya chama kileee
 
Ila wewe jamaa una muda wa kutosha kukesha na kushinda JF na kuchangia kila mada kila muda. Halafu hapo hapo unadai hakuna hela mtaani...
Ni pm Uje nikuajiri kuna kazi kwenye office yangu .....

Mi sio kama serikali yako ambavyo haiwezi kutoa Ajira wakati watu wanalipa kodi
 
Kama ni kweli basi itakuwa ni zamu yao kukabana wenyewe kwa wenyewe,ila hili la mwendokasi linaweza kuwa kweli,kuna watu wengi sana hawasikiki na wameamua kukaa kimya tu,na kimya kikuu kina mshindo,tusubiri tuone,Ehh mwenyezi Mungu tupe uzima waja wako tuyashuhudie matendo makuu.
 
Ni pm Uje nikuajiri kuna kazi kwenye office yangu .....

Mi sio kama serikali yako ambavyo haiwezi kutoa Ajira wakati watu wanalipa kodi

Ajira yako ni pale Ufipa. Mmepewa kompyuta na vifurushi vya bure basi mambo burudani. Mnajimwaga tu vijana wa Aikael
 
Ajira yako ni pale Ufipa. Mmepewa kompyuta na vifurushi vya bure basi mambo burudani. Mnajimwaga tu vijana wa Aikael
Mawazo yako madogo eti kila anayemkosoa mkulu ni wa ufipa wakati wakosoaji wake wengi wamejaa serikalini!!!

Ni upuuzi kutolijua hilo......
 
wao wana mapepo sisi tuna Mungu alie hai Magufuli mbele kwa mbele......
 
 
CCM sio saccos huyo mwenye hilo kundi lako unalosema mwambie hata asijifiche ajitokeze hadharani lakini atachapwa tu akisimama na JPM. Huyu hana mpinzani na hatakuwa nae ever.
 
Magufuli 2015-2025
 
Wazee wa "kuna taarifa"," nimepata tetesi" ,"kuna mkakati"..."A na B"

Ila kuna hii John Mnyika Katibu chadema bara hamkubali Lowassa kwa ajili hiyo kapunguziwa kazi zake zinaingiliwa na Katibu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalimu ambaye huko Zanzibar hajulikani ,hii nayo ni mpasuko wa Chadema Asili (Mnyika na Mbowe) na Chadema Mkurupuko(Lowassa na Mwalimu).

Pia Chadema wanamhofia Lipumba kuongoza vizuri uenyekiti wake maridhawa kwa kuwa ataufafanua huo umoja wa kitapeli "ukawa" kwamba Chadema waliugeuza maana kwa kujinufaisha kupata kura nyingi za urais na hatimaye ruzuku ya kura za raid zimeenda kwao na CUF hawafaidiki.
Na ule mchezo walioufanya Chadema kuweka wagombea wa ubunge na udiwani sehemu walizotakiwa wasimamishe wagombea CUF ,NLD &NCCR..

Kwamba Mbowe aliagiza 1st October kufanya ukuta ya pili matokeo yake kaishia Uwanja wa Taifa bega kwa bega na "Mzee wa Kibiriti cha gesi"

Nyie wana kuna tetesi nyingi sana hamzijui tu,alijisemea Juma Duni Haji "pale Chadema kila mmoja kambale"
 
Wahanga ni wengi sana hakuna mwen hamu na Juma Ponda Mali.....nadhani hata wale wanaomzuguka basi tu!
 
Si rahisi kihivi sababu mwenye kisu ndiye mlaji.Kisu anacho JPM
Umenikumbusha msemo wa president Kenyatta aliposema, "kumeza mate sio kukula nyama, sisi tunakula nyama wacha wao waendelee kumeza mate"!!
 
Hakuna cha asili wala cha nini. Haya maandalizi ya namna hii yanahitaji pesa nyingi sana kuzidi zile za kugawa makanisani na miskitini. JPM amefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwa kubana upatikanani wa hela chafu ambazo niseme ndo zingewezesha hiyo unayoita asili. Kwa hali Iilivyo sasa mifukuni kwa hao asili wako ni tete sembuse uwasubirishe tena mpaka 2020......sipati picha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…