Tetesi: CCM asili inamuandaa mgombea wake 2020

Ndugu wana jamvi, kuna taarifa nilizozipata ambazo ni mkakati wa muda miaka mitano hadi kufikia Septemba, 2020 CCM asili itakuwa tayari ina mgombea wake katika uchaguzi wa uraisi. Mkakati huu unaratibiwa na viongozi wakongwe ndani ya CCM wakishirikiana na vijana wa CCM wapambanaji waliotelekezwa katika awamu hii ya uongozi.

Kama mnavyofahamu katika awamu hii kuna viongozi wengi wa CCM ambayo ni majeruhi kutokana na kutumia fedha na nguvu zao nyingi kukisaidia chama kishinde katika uchaguzi wa mwaka 2015 lakini wametupwa kama vile hawana chochote walichokifanya ndani ya chama.

Hali iliyopo kwa sasa inasemekana kuna makundi makubwa mawili ndani ya chama ambayo Rais ameyatengeneza kwa makusudi ili kuwakomoa baadhi ya wananchama waliokuwa wanajiona kama wao ndio wanaccm kweli kweli. Makundi yaliyopo kwa sasa ni;

1. CCM ASILI (CCM A) = Hili ni kundi lililojaa wanachama wengi wakongwe na wenye mbinu nyingi katika chaguzi mbali mbali, ikiwa ni pamoja na majeruhi wengi katika awamu hii ya uongozi.

2. CCM MWENDOKASI (CCM B) = Hili ni kundi lililojaa wanachama wengi wenye kunufaika na utawala huu na ambao wengi wao si wazoefu sana na mambo ya kisiasa ila imetokea tu wamebahatika kupewa vyeo katika Serikali hii na kujiona wao ndio wenye chama kwa sasa.

Katika makundi haya japo hayajitangazi moja kwa moja lakini yapo na yanaendelea kufanya mikakati kivyake. Kundi la pili (CCM MWENDOKASI), hili kundi liko mtaani na linajinadi kila uchwao na linajaribu kutafuta watu wao ili ifikapo mwaka 2017 waweze kuwapenyeza kwenye uongozi na kushika madaraka.

Kundi la kwanza (CCM ASILI) hawa wako kimya na wanafanya mikakati yao kimya kimya, hutawasikia mitaani au kwenye mashina ya chama wakifanya makeke yoyote ila mipango yao ni mikubwa. Kundi hili lina ushawishi mkubwa sana ndani ya CCM na inasemekana hali itakuwa sio ya kawaida kwenye uchaguzi wa chama mwaka 2017.

Inasemekana mwaka 2020 CCM haitabaki kama ilivyo, hali itakuwa tofauti sana na inawezekana hakutakuwa na kitu kinachojulikana kama utamaduni wa kuachiana.

Taarifa hizi nimezipata kutoka kwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisia ndani ya chama cha Mapinduzi na ambaye yeye amejitabulisha kuwa kwa sasa yuko kundi Mwendokasi kwa sababu anafaidika na utawala huu lakini mapenzi yake yanaegemea kundi la Asili kwasababu wana hoja za msingi kwamba chama kimeporwa na watu wasiojua misingi ya Chama Cha Mapinduzi.

Nawatakieni kila la kheri!!!!!!!
CCM A + CCM B= 2CCM +

CCM A + CCM B=2CCM +A+B!!!!!!!!!!!!
 
Chama kikishakuwa kubwa mara zote watu wanatofautiana ila inategemeana wenye kutumia nguvu na wenye kutumia akili,hayo hayaepukiki kwenye chama cha siasa
 
Porojo hizo wewe peleka huko ufipa mnakoandaana, CCM maji marefu!!
 
Bora tungemuacha yule aliyeshinda kwenye kura za chama .. Ila jinsia eti ndo ikawa shida sasa sijui mnaona majanga haya... Bora angekaa Dr pamoja na kua jinsia yake inachangamoto
 
kama CCM hakikusambaratika 2015 hakiwezi kusambaratika in next 20 yrs
 
Kuumia kwa ccm ndio kupona kwa watanzania.............

Kama tu uchaguzi uliopita hakuna mtu Mwenye uhakika kama alishinda ije iwe 2020?

Ni kweli huyu mgombea inabidi abadiliswhe 2020 lasivyo atashindwa vibaya na atakatalia ikulu.........

Hapo ndipo nchi itakapoingia matatani.....

Mwaka mmoja tu mmeshaanza kunena kwa lugha! maisha ya ujanja ujanja yana tabu zake.
 
Hakuna mwanadamu yeyote anaependa kuvuruzwa. Hii inapelekea kuwa na strggle ktk kila nyanja ya maisha.

Struggle zipo kuanzia ndani ya familia, shuleni, ofisini, ktk taasisi za dini mpaka mamlaka za juu.

Mwaweza ona mpo pamoja ila kumbe ni tofauti.

Sishangai kwa hili.
 
misingi ya chama imeainishwa katika Katiba ya Chama na kanuni zake....Kanuni na Katiba viko wazi kila mtu anajua. Sidhani kama kuna kiongozi wa chama ambaye hajapitia Katiba na kanuni/miongozo ya chama.

Kusema hawajui misingi ya chama, kauli hii inatia mashaka. Vinginevyo waseme wanayo misingi mingine ambayo imefichwa kwenye Katiba ya kificho (kama kweli ipo) ya chama.
 
Back
Top Bottom