Tetesi: CCM asili inamuandaa mgombea wake 2020

Tetesi: CCM asili inamuandaa mgombea wake 2020

Hao ccmA au asili ni waulize wana mbinu na ukomavu kimikakati kama Kingunge, EL, Sumai na wapambe wao?

Na washawasha!
 
JUMA PONDA MALI(JPM) uchaguzi ujao utakuwa Mgumu sana Kwake lazima atumie Ukurunzinza kubaki otherwise lazima wamkate kibaku.
 
hamna tatizo ..tutamuomba magufuli agombee binafsi ....afu tumpe nchi awanyooshe vizuri akiwa hana chama
 
Ndugu wana jamvi, kuna taarifa nilizozipata ambazo ni mkakati wa muda miaka mitano hadi kufikia Septemba, 2020 CCM asili itakuwa tayari ina mgombea wake katika uchaguzi wa uraisi. Mkakati huu unaratibiwa na viongozi wakongwe ndani ya CCM wakishirikiana na vijana wa CCM wapambanaji waliotelekezwa katika awamu hii ya uongozi.

Kama mnavyofahamu katika awamu hii kuna viongozi wengi wa CCM ambayo ni majeruhi kutokana na kutumia fedha na nguvu zao nyingi kukisaidia chama kishinde katika uchaguzi wa mwaka 2015 lakini wametupwa kama vile hawana chochote walichokifanya ndani ya chama.

Hali iliyopo kwa sasa inasemekana kuna makundi makubwa mawili ndani ya chama ambayo Rais ameyatengeneza kwa makusudi ili kuwakomoa baadhi ya wananchama waliokuwa wanajiona kama wao ndio wanaccm kweli kweli. Makundi yaliyopo kwa sasa ni;

1. CCM ASILI (CCM A) = Hili ni kundi lililojaa wanachama wengi wakongwe na wenye mbinu nyingi katika chaguzi mbali mbali, ikiwa ni pamoja na majeruhi wengi katika awamu hii ya uongozi.

2. CCM MWENDOKASI (CCM B) = Hili ni kundi lililojaa wanachama wengi wenye kunufaika na utawala huu na ambao wengi wao si wazoefu sana na mambo ya kisiasa ila imetokea tu wamebahatika kupewa vyeo katika Serikali hii na kujiona wao ndio wenye chama kwa sasa.

Katika makundi haya japo hayajitangazi moja kwa moja lakini yapo na yanaendelea kufanya mikakati kivyake. Kundi la pili (CCM MWENDOKASI), hili kundi liko mtaani na linajinadi kila uchwao na linajaribu kutafuta watu wao ili ifikapo mwaka 2017 waweze kuwapenyeza kwenye uongozi na kushika madaraka.

Kundi la kwanza (CCM ASILI) hawa wako kimya na wanafanya mikakati yao kimya kimya, hutawasikia mitaani au kwenye mashina ya chama wakifanya makeke yoyote ila mipango yao ni mikubwa. Kundi hili lina ushawishi mkubwa sana ndani ya CCM na inasemekana hali itakuwa sio ya kawaida kwenye uchaguzi wa chama mwaka 2017.

Inasemekana mwaka 2020 CCM haitabaki kama ilivyo, hali itakuwa tofauti sana na inawezekana hakutakuwa na kitu kinachojulikana kama utamaduni wa kuachiana.

Taarifa hizi nimezipata kutoka kwa kiongozi wa ngazi ya juu kabisia ndani ya chama cha Mapinduzi na ambaye yeye amejitabulisha kuwa kwa sasa yuko kundi Mwendokasi kwa sababu anafaidika na utawala huu lakini mapenzi yake yanaegemea kundi la Asili kwasababu wana hoja za msingi kwamba chama kimeporwa na watu wasiojua misingi ya Chama Cha Mapinduzi.


Nawatakieni kila la kheri!!!!!!!
Peleka umbea chadema.
 
Bavicha wanajitahidi kutpa vibomu uchwara,hakuna kipindi ambapo ccm ipo imara na moja kama sasa,kazi ni kutimua mabaki ya mafisadi na wasaliti,mambo ya asili na mwendokasi yapo kwenu chadema,kuna watu wa slaa na lowassa na ushahidi upo kukaa kimya kwa kina mnyika na genge lake
 
Uchumi umeangukia mikononi mwa wahindi, vijana wa kitanzania wanachoweza ni KUPIKA UWONGO, MAJUNGU NA PROPAGANDA ZA WANASIASA - WAKIBADILI KAZI NI KWENDA kubet kwenye kampuni ya MHINDI.HASARA SANA
 
Upinzani Kuongoza nchi kwa kutegemea CCM isambaratike yenyewe ni dalili ya Upinzani ulio dolola, Kwa hali ya sasa ktk hatma ya siasa za kitanzania, kila kiongozi wa upinzani anasema"Kwa mwenendo huu hakuna chama cha Upinzani kitakachobaki salama, ni muda mwafaka wa kuunganisha nguvu kupinga udikiteta nchini mwetu na kupigania demokrasia ya kweli" Kinachoshangaza ni kwamba Tangu vyama vya upinzani vianze kuimba huu wimbo, bado hawajawa na mikakati ya pamoja baina ya chama kimoja na kingine juu ya hili, Kwenye operation ambayo CHADEMA waliibatiza OP UKUTA hata vyama wenza wa UKAWA havikushiriki.Naenda mbali zaidi ,Prof Mkumbo nae kwa upande mwingine ACT, amekua mtu wa kulalamika tu, kwamba upinzani unapaswa kuwa na mbinu mpya bila kuzitaja mbinu hizo.Upinzani kama hawajawa na ajenda ya pamoja juu ya usiginaji wa demokrasia unaofanywa na CCM kama wao wanavyodai,wasitegemee CCM kuondoka madarakani kwa kufanya press conferences na makongamano ya ndani bila Umoja,CCM itaendelea kupeta bila kizuizi.........
 
Ccm mwendokasi ndio hii ya Gari bovu? Basi ndio maana hao Asili wako kimya maana Gari bovu ndani ya mwendokasi unategemea nini kama sio kupinduka na kuwa mwisho wa safari?
Chakaza una miaka 9 mingine ya kuisoma namba hadi mnyooke, Hapa Kazi Tu
 
swala sio ccm swala ni nani mrithi wa ccm??chadema,cuf hawa kila siku wanalumbana wenyewe kwa wenyewe??hawa wasio na msimamo na matamko yao??wote tunajua mapungufu ya ccm lakini ni bora hayo kuliko kutoa nchi kwa chama kisichojielewa kinasimamia mlengo gani kwa wakati gani.
 
Chakaza una miaka 9 mingine ya kuisoma namba hadi mnyooke, Hapa Kazi Tu

Aa wapi acer, ngoma hii ni 2020 lazima ipasuke. Na hapo ni kama bwana mkubwa hajaamua mwenyewe kuachia ngazi maana muziki unaonekana kumuwia mgumu mapema sana.
 
CCM asili miaka yote walikiwa wapi wakati nchi inatafunwa, msifanye watanzania wajinga.
CCM ni CCM tu, hata mbadilishe majina ni ilele.
Na kwa taarifa yenu na hili manalijua watanzania wahaitaji CCM wanataka maendeleo.
 
JPM haendi kokote, maneno ya wakosaji. Walioshindwa kutawala na kuleta maendeleo kwa walipa kodi wakae kimya. 2020 itakuwa judged by performance sio majungu.
 
Back
Top Bottom