Nimeona Leo mgombea ubunge jimbo la Kaliua ndugu Aloice Kwezi gari la matangazo wanasema na wasanii watakuwepo FM. Akademia tena huku ni vijijini ambako mmekuwa mkijinasibu ndio kura zenu zipo wasanii wa nini sasa.
Kiukweli kabisa wananchi wanawapuuza sana CCM mmekosa sana mvuto. Hivi babu anakuunga mkono kweli maana alivyo yule mzee Kapuya alishinda kwenye kura za maoni halafu akakatwa una wakati mgumu sana ndugu yangu.
Sakaya nae alibebwa na upepo wa ukawa mwaka huu halo ni tete sana. CHADEMA nao mgombea wao hata hajulikani kabisa kampeni hapigi sa sijui wanawaza nini.