CCM can reclaim her legitimacy, by going back to the roots, SI POROJO ZA MEDIA!

Bongolander

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2007
Posts
5,067
Reaction score
2,210
Wakuu inaonekana sasa kuwa CCM kama chama, kimeanzisha na kuimarisha propaganda [kudanganya au ku-mislead watu], kutumia mamluki na baadhi ya waliohongwa na kupenyezwa kwenye vyombo vya habari, kuvitumia vyombo vilivyonunuliwa na waliokiteka chama, kufanya mabadiliko katika safu yake. Hapa JF ndio ajabu wamekuja watu hata ambao wanasahau post walizopost mwezi mmoja au miezi mwili iliyopita, lakini sasa wamenza kutangaza kile ambacho katika baadhi ya duru za kisiasa huwa zinasema ni "kumpaka lipstick Nguruwe", au "kuweka mvinyo wa zamani kwenye chupa mpya".

Tulio wengi katika jukwaa hili inawezekana ni wazalendo, wenye uchungu na tunaoipenda Tanzania, na tunajua ni CCM ipi ilivyokuwa Chama cha wakulima na wafanyakazi, ni CCM ipi ilivyokuwa inafanya kazi kwa maslahi ya Tanzania. Na tunajua kabisa kuwa CCM ile haipo tena, kuna vijana wengi kama Nape Nnauye wanaomba Mungu na wengine wanajitahidi sana kujaribu kukirudisha chama kwenye njia yake, kazi ambayo kimsingi ni "daunting task". Ni ngumu kwa kuwa mafisadi wanajua (kwa sasa) wana karata zote.

Sijui kama kuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayeamini kuwa Mzee Mangula na Mzee Kinana wanaweza kuwashinda mafisadi, na kuifanya CCM kiwe chama cha Mapinduzi, chama cha wakulima na wafanyakazi, chama cha kutetea haki na kinachoweza kuleta Maendeleo ya nchi. As of now I remain extremely pessimistic, because most of what they are currently doing is merely cosmetic. It does not show any sign that there are significant steps and deliberate efforts in rooting out the system that supports corruption and favoritism and personalization of the party and her offices.

Lakini tatizo kubwa linalokiathiri chama toka JK ashike hatamu ni "internal skirmishes" ambazo kufikia 2014 zitakuwa mapambano wazi, kwa kuwa mafisadi wameapa kuwa chama hakirudi kwa CCM asili, kwa kuwa kikirudi huko hawatakuwa salama. Na CCM asili ambao wameaza kuonekana in the form of upinzani, wameanza kuonesha haja ya kurudi kwenye malengo ya kuanzisha Chama. Yaani CCM iwe chama cha kuendeleza nchi, sio kuifilisi nchi kama sasa, iwe chama cha kutoa leadership na sio kuficha fighting for survival.

Mpaka sasa ukiangalia Tanzania inayoongozwa na CCM, utaona kuwa hakuna malengo halisi ya kuifanya Tanzania ipige hatua, ni tofauti sana na CCM 20 years ago wakati viongozi walikuwa wanatamba kuwa we have managed to have a country with lowest illiteracy rates, lowest crime rates, lowest rates of malnutrition, fairly good hospitals etc etc…sasa hivi kila kitu kiko chini, kilicho juu ni ripoti ya World Bank inayosema Tanzania ina miasha bora sana.

Kenya ukiangalia maendeleo waliyopiga katika miaka mitano huwezi kuamini kama ni jirani zetu, licha ya ukabila na vurugu za mapigano yao. Sawa na Rwanda. Mwezi uliopita nilitamani kulia nilipokuwa napita Nairobi na kunaglia barabara ya Thika. Nikajiuliza why not Tanzania which is relatively peaceful, secure and stable. Kenya na Rwanda si Ulaya, If the can do it why not us????

Nigependa tujadili kama kwenye strategy wanayotumia CCM kwa sasa ni healthy, kama kweli itasaidia kutuondolea matatizo ya sasa.

Kama kweli CCM ambayo inataka kuendelea kutawala, ni lazima irudi kwenye msingi wa kuanzishwa kwake. Ni lazima kisiwe chama cha kuwahurumia mafisadi, chama cha kulinda wezi wa mali za taifa, kiwe chama cha wakulima na wafanyakazi, chama cha kuendelea nchi na kulinda utu na heshi ya mtanzania, na zaidi ya yote kuifanya Tanzania ambayo tumepewa na mungu, kuwa juu ya yote ya vyama na ubinafsi wa watu. By doing so CCM ita regain real legitimacy, the one it had wakati wa Abeid Karume, Julius Nyerere, Rashid Kawawa, Edward Sokoine etc etc…hizi blah blah za kwenye media haziwezi kuturudishia CCM inayotakiwa.
 
Bongolander,

Kwanza nikiri hii ni moja ya article nzuri sana na ya kistaarabu sana nimewahi kuisoma JF kwa muda mrefu sasa.

Nikiri pia kuwa CCM kama chama kina matatizo mengi sana leo pengine kuliko jana, lakini pia ni vizuri kuelewa kuwa kwa changamoto za leo za jamii yetu na mazingira ya leo, pamoja na matatizo ya CCM leo kama taasisi ni imara kiasi cha kustahimili mikikimikiki ya siasa za leo! Lakini pia ni ukweli usiofichika kuwa kwasasa Tanzania hakijapatikana Chama mbadala wa CCM, natambua huu ni UKWELI ambao unauma si kwa wapenda upinzani bali hata kwetu CCM hili la kutokuwa na chama mbadala mpaka leo kwa miaka 20 ya vyama vingi nchini si jambo zuri kwa demokrasia yetu na hata kwa afya ya CCM yenyewe!

Juu ya media, ni kweli tumebadili namna tunavyo shghulika na media and am very happy kwamba mabadiliko yetu yamekuwa na impact ndo maana watu wana feel na kuuliza kinachoendelea, so weather ni mkakati mzuri au mbaya kwa afya ya demokrasia,la kwanza kubwa ni kuwa ni mkakati ambao umekuwa na matunda. Kwanini mkakati huu uliwekwa, sababu zingine siwezi kuzisema lakini moja kubwa ni kuwa kwa kipindi sasa palikuwa na juhudi kubwa AMBAZO PIA BADO ZINAENDELEA za kuichafua sura ya CCM mbele ya umma kwa makusudi na wakati mwingine kwa kutokujua. CCM ikabebeshwa dhambi nyingi hata isizozistahili na waliotumika kufanya kazi hiyo kwa sehemu kubwa ni sehemu ya media, SIO WOTE ni kundi dogo lakini ambalo lilikuwa linajua linachofanya.

Nitoe mfano mdogo sana ambao atakayetaka kuniamini aniamini, asiyetaka ruksa kutoniamini( nasisitiza sitoi mfano huu kuisafisha CCM kwenye hili ila najaribu kuonyesha dhambi tunazobebeshwa ambazo si zetu).. INAAMINIKA CCM ILITUMIA PESA ZA EPA ZILIZOCHUKULIWA NA KAGODA KWENYE UCHAGUZI WA 2005, WAKATI IKIAMINIKA HIVYO, PESA YA KWANZA YA KAGODA IMETOKA JANUARY 2006 WAKATI UCHAGUZI ULISHAFANYIKA MWAKA 2005. Lakini leo utamwambia nani kuwa CCM haikutumia pesa ya Kagoda AKAKUAMINI??! Huu ni mfano tu, lakini yapo mengine mengi!!

Nakubaliana na wewe kuwa msingi mkuu hapa wa CCM kukubalika na kurudi kwenye msingi wake wa awali. Lakini pia kuhakikisha serikali zake zinafanya kazi ya kuhudumia watu tena wanyonge ili kubadili maisha yao kutoka ya chini kuwa bora zaidi.. Ndio msingi wa kuitwa Chama Cha Mapinduzi, chama kinachopindua maisha ya watu kutoka ya hali duni kuwa ya hali nzuri kuliko jana na kesho kuliko leo..

BUT AGAIN NAKUSHUKURU KWA ARTICLE YAKO!
 
Last edited by a moderator:
Bongolander,

Well, Ukweli ni kwamba Chama cha mapinduzi si chama cha mapinduzi tena. Nyerere alijaribu kufanya mapinduzi kufanya nchi hii ijitegemee na siasa yake ya ujamaa na kujitegemea hata hivyo Alishindwa. Wengi wa waliopo ndani ya CCM hawajui hata Mapinduzi maana yake ni nini.

Tuliona wakati wa Nyerere kulikuwa na itikadi hiyo ambayo malengo yake ilikuwa kubadili fikra za watu kuhusu Taifa lao alifanikiwa sana kujenga uzalendo kwa watu na lengo lake ilikuwa kufanya Taifa hili lijitegemee wiimbo ambao CCM hawawezi kuuimba kwa sasa. Hawawezi kujjita kwamba wao ni chama cha mapinduzi wakati nchi yetu mpaka leo kwa asilimia karibu hamsini inategemea wahisani. Ni mapinduzi gani walioishafanya mpaka sasa tukajisifu, je ni ya kilimo? Viwanda? Au siasa yetu ambayo imelegalega? Je ni ELIMU? Ambayo mpaka leo haijamfanya kijana wa Taifa hili kujitegemea kwa mawazo kwa kugundua kitu chochote au kuanzisha kitu chochote kikubwa ambacho kitaleta tija kwa Taifa. Elimu ambayo haimjengi mwanafunzi katika utaifa na uzalendo, Elimu yetu haijatengenezwa kulisaidia Taifa hili bali matumbo binafsi ya watu. Ni lazima tutambue hili Taifa tutalijenga pamoja kwa busara na maarifa.

Nchi yetu imekosa dira sababu ya viongozi wabovu wa wasio na maono. Nasema tena hatutaweza kupiga hatua kama Taifa kama watu wetu wasipojitambua wao ni kina nani na wana malengo gani na nafasi yao ni ipi katika dunia.

Vyombo vya Habari vina nafasi kubwa sana katika ujenzi wa Taifa imara kama watu wake watawajibika kuwalisha walisha wananchi mambo ambayo yatajenga msingi wa Taifa hili na ku shape akili za watu wetu. Mtazamo wa watu wetu katika kujenga Taifa imara ni muhimu sana. Tuna Taifa lenye mgawanyiko sasa hivi kwasababu ya vyombo hivi kutumiwa na watu kwa malengo binafsi.

Nimekuwa nikiamini kila wakati tunaweza kuendesha siasa zetu vizuri katika misingi yenye nidhamu kama tutakuwa wazalendo. Kama vyama vyote vitaongozwa na utaifa na sio uchu wa kuingia madarakani au kubakia madarakani. Siasa za kistaraabu zinawezekana kabisa ikiwa tutashindanisha mawazo na wananchi kuamua kwa kupitia njia za kidemocrasia.

Tunaweza kujenga siasa kwenye misingi ya democrasia na haki. Lakini hili kwa Afrika limekuwa Tatizo kubwa watu kufanya siasa za kistaarabu imekuwa tatizo na watu kuachia madaraka wanaposhindwa uchaguzi imekuwa tatizo pia.
 
Last edited by a moderator:
Bongolander,

CCM kurudia misingi yake haina maana kwamba ni lazima kirudi kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi kama awali; Kinachohitajika ni kwa CCM kuwa karibu na wananchi wa aina zote; Kwa mfano, mahitaji ya wakulima na wafanyakazi yanaweza kutengenezewa mazingira mazuri sana kwa serikali ya CCM kuviwezesha vyama vya wafanyakazi, vyama vya ushirika, vyama vya wakulima, vyama vya wafugaji, na pia CCM kuja na ubunifu juu ya jinsi gani vyama hivi vinaweza kushirikiana kwa ukaribu na serikali ya CCM; Vinginevyo CCM kujinadi tena e.g. - kama chama cha wafanyakazi huku serikali yake ikiendelea kuwa na mahusiano mabovu na wafanyakazi - madaktari, walimu n.k, itakuwa ni siasa za kupoteza tu muda; Muhimu ni kwa CCM au chama kingine chochote kitachoingia madarakani kuwa na mahusiano ya karibu na wakulima na wafanyakazi, hata kama chama hicho kitaingia ikulu kama chama cha Wachimba Madini au Chama Cha Wavuvi;

Now about change - hakuna jamii duniani iliyopiga hatua kimaendeleo kwa njia ya kulinda peace, order and stability; Haya mambo matatu might be a pre-requisite ya Maendeleo kwa nchi lakini only if nchi husika imefikia a certain threshold, kitu ambacho Tanzania bado hatuna; Hata Mwalimu Nyerere alipata tamka miaka ya tisini kwamba "Watanzania Wanataka Mabadiliko, Wasipoyapata Kupitia CCM, watayatafuta kupitia Chama Kingine." Na wakati huo Chadema haikuwa na nguvu kama ya leo, which means kwamba hata ingekuwa sio Chadema, wananchi wangetafuta mabadiliko kupitia aidha CCM iliyozaliwa upya au Vyama vingine vya upinzani; Lakini kwa kiasi kikubwa, viongozi wengi wa CCM treat hali tete ya kisiasa nchini kama vile ni zao la Chadema wakati ukweli ni kwamba hili ni zao la umma; Chadema wametokea tu kuwa beneficiaries katika muda muafaka;

Tatizo ni kwamba wananchi wanataka progress, huku CCM aidha ikihimiza umuhimu wa jamii to conserve kilichozolekea, viongozi kutoa matamko yanayoashiria kwamba ni wajibu wa wananchi kuridhika/kuwa na shukrani na mafanikio yaliyopatikana chini ya CCM huku wakihimiza wapuuze siasa za chadema, au ikijaribu to dictate the pace of change katika livelihoods za wananchi, on its own terms; Wanacho hitaji watanzania ni progress, and progressivism is an ideology in itself, and it goes hand in hand with the disturbance of peace, order and stability; CCM inazidi kupoteza muda kushindana with the wind of change; Busara kwa CCM ni kupokea mtazamo mpya wa umma, huku ikifanya jitihada kubwa Chama kiwe on the driver's seat to manage this wind of change to its own advantage; Vinginevyo you may succeed to convince or force Tanzanians to conserve (hence conservatism) on the cultural/social front kwa kuhimiza umuhimu to conserve peace, order, stability for their own good, but on the economic front, social conservatism will not work; Majority are for progressivism (kiuchumi), tena progress on their own terms based on what they see around them – rasilimali zikinufaisha wachache n.k, not progress on terms za watawala; CCM has to understand kwamba Peace, Order and Stability vinaweza kuwa assets muhimu katika mchakato wa kutafutia wananchi maendeleo, but only to an extent kwani on the economic front, too much of peace, stability and order can become 'a liability' to the majority;

As a society, we are very fragile and vulnerable kuendelea kuimba nyimbo za amani na utulivu wakati all correlates za state instability kwa mujibu wa nadharia juu ya machafuko ya nchi, do not favour our country; Such correlates za conflicts and instability among countries ni pamoja na large youth population (aidha underemployed or unemployed); highly heterogeneous ethnic and religious groups (we have so many ethnic groups and the nation is almost equally divided between Muslims and Christians); Chronic Foreign Aid Dependence which leads to fiscal bad habits (mfano EPA); income poverty miongoni mwa wengi, n.k; Yote haya ni yanahusishwa na machafuko ndani ya mataifa mbalimbali, and all these are indicators blinking in Tanzania kwa muda mrefu, ni suala tu la lini bomu litalipuka;

To sum it up, again, amani na utulivu haviwezi kwenda hand in hand with demand for change miongoni mwa umma katika jamii changa kiuchumi kama Tanzania, hasa iwapo mabadiliko husika yanatishia kutikisa mfumo na muundo uliozoeleka na unaoshikiliwa na ‘wenyewe'; historia kidunia haituelezi otherwise; Demand for change ya status quo, goes hand in hand with msukosuko wa order, peace and stability; Kilicho muhimu kwa CCM ni kujiuliza, je chama kipo tayari to change with the society OR it wants the society to leave it behind?

Unlike before, CCM haina tena uhalali to dictate the pace of change in the society, badala yake imebakia na options mbili – aidha kubadilika according to demands za umma, OR kukubali chama kimeguke, upande mmoja ukifuata dhana ya progressivism kwa integrity/moral soundness ya hali ya juu, huku ikiachia upande uliobakia uendelee na madudu wanayo yaamini ikiwa ni pamoja na nguvu za dola, vyombo vya habari na fedha; Nje ya hapo, CCM haina hati miliki na taifa letu, ivipishe vyama vingine kwa mujibu wa matakwa ya wananchi, vinginevyo kukataa mabadiliko kutaipa CCM ushindi wa muda tu, kwani hatimaye nchi itaingia katika machafuko, na wahalifu watakuwa ni wale waliokuwa wanapinga mabadiliko, haitakuwa wale wanaoshinikiza mabadiliko, hata kama pande zote zitahusika katika umwagaji damu wa raia wasio na hatia;
 
Which roots? The oxymoronic "Ujamaa na Kujitegemea" ?

Mkuu by going back to the roots i mean CCM should be the party of those she leads, not the party of those who is in power, as it is now. Mchambuzi has made a very good point, that is it should cater for the interest of the masses (jamii ya watanzania ina wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wavuvi, wachimba madini etc etc etc), that is where roots of CCM are.

There is no doubt that if you talk about the policy of Ujamaa and self reliance now, as it was practiced few years after independence and during the reign of Mwalimu, you will be completely out of touch with the current national and international realities.

Kwa sasa CCM ni chama cha walio madarakani, kinafanya kazi ya kuhakikisha walio madarakani wananeemeka na waendelea kuneemeka, ni chama cha wenye nguvu si cha wanyonge, in short it has been hijacked by mafisadi and it is serving their ineterests. Ndio maana wajumbe wengi hapa JF wanasema CCM ya 2012 ni chama tofauti kabisa na CCM pre Zanzibar declaration, may be CHADEMA 2012 is a bit close to CCM pre Zanzibar declaration.

Media campaign ya kutangaza kuwa CCM sasa ni nzuri sana na kufanya sura yake iwe nzuri kwenye vyombo vya habari, haina maana kuwa CCM all of a sudden imeanza ku-serve interests za nchi na wale inaowatawala. Until that is seen, bado CCM kimo mikononi mwa mafisadi.
 

CCM has been a party of abracadabra from the get go, hence the contradictory "Ujamaa na Kujitegemea".
 

Bongolander ccm lazima ishindwe uchaguzi na ndipo kukirabati yawezekana. Maana mafisadi wote watahamia vyama vingine kuutafuta mkate........na asali
 
Last edited by a moderator:
Bongolander;

If one reads your post causally, he/she might agree with you that in order to retain their position, CCM need to rediscover their roots. The roots that drastically improved the illiteracy rate to more that 90%, that built one dispensary in every ten villages, and many more. However, the truth of the matter is if CCM had been excellent 20 years ago, the country wouldn't have been in this shape. We are in this shape because the party didn't have a plan. And, whenever they had one, it was poorly planned and funded by unsustainable foreign resources.

Think about this. The country has enjoyed peace for the past 50 years, and if there was any good development plan 30 or 20 years ago, by now we would have picked it and we wouldn't accept any sorts of mediocrities we experience today. For example, any Tanzanian who attended a decent school 20 or 30 years ago, we wouldn't accept his child to attend government primary and secondary schools.

And let me tell you this. If CHADEMA had been an opposition party in late 70s and 80s, it would have garnered the same popularity and CCM would have used the same propaganda and tactics. So whatever you see here now or in other media isn't new. CCM is deeply rooted in propaganda and back in the days, they used to have a special secretariat within the party dealing with propaganda.

Furthermore, we need to get rid with this Wakulima and Wafanyakazi nonsense. Tanzania wasn't a class society and we didn't need a political party to specifically address the concerns of peasants and workers which didn't exist. If you take time to read the original doctrine of CCM, you will discover that the party was trying resolve imaginary issues. So there's no reasons to ask them to retain the roots because they didn't have any.

So rather than asking CCM to look into the past, CCM members need to face the truth. First, they need to comprehend that losing elections isn't a bad thing at all. For, it gives the party the opportunity to re-evaluate its policies and get rid of bad apples. For example, CCM will not get rid of Lowassa or Sitta if they continue to win. CCM will not learn from their past mistakes if they continue to win.

Second, CCM need to know that their party is fighting with other political parties to address the issues of the same constituency. When it comes to economic and social issues the country doesn't have a political divide. CCM, Chadema, CUF, and TLP share the same issues.

So instead of reverting to ideological orientation of the past in which the top brass of CCM decided what the country should follow, now CCM need to listen people's concerns and solve them accordingly. If they can't, people have other choices.
 
Bongolander article yako nimeipenda sana na kwa kiwango kikubwa imebeba idea ambazo CCM imezipoteza kwa miongo kadhaa sasa na kwa kweli zidhani kwa hali ilivyo sasa kama kuna uwezekano wa kurudi kwenye roots zake kama unavyotamani iwe.

Kwa sasa chama hiki idadi kubwa ya top leaders na hapa unaweza kuzungumzia familia na hata uzao wao umejikita katika kitu kimoja tu; UVUNAJI MALI NA UFISADI. Idadi ya wanaojikita katika uharamia huo ni kubwa sana na mtandao wake umeenea hadi ngazi za chini kabisa.No wonder ndani ya CCM ukakumbana na madiwani au viongozi wenye record chafu za ujambazi, ufisadi wa waziwazi na matukio mengine ya kimafia.

Unapokuwa na idadi kubwa ya viongozi wanaobeba mtandao mpana wa wachuma fedha na ufisadi usitegemee miujiza ya CCM kurudi kwenye asili yake ya kuwa chama cha watetezi wa wakulima na wafanyakazi.Hizi ni ndoto za mchana.Ukitaka kujua ugumu wa kutimia kwa ndoto hii ni kuasisiwa kwa dhana ya kujivua gamba na jinsi ilivyo pepesuka na hatimaye kufa kibudu huku akina Nape Nnauye na mwenzake John Chiligati wakiishia kuchoreshwa na Mwenyekiti wao wa chama.

Ni wazi kuwepo kwa idadi kubwa ya wapiga dili, wachuma mali na mafisadi ndani ya chama usitegemee wakubali mkate wao upotee kirahisi. Hii ikiunganishwa na Ufisadi wa kitaasisi unaotamalaki sasa nchini ndiyo kwanza unafifisha matumaini yote ya kurudi kwa CCM asilia.

Hivi tulishawahi kujiuliza sababu ya CCM kulipiga teke Azimio la Arusha badala ya kuendelea kulifanyia maboresho ili liendane na nyakati? Tumejiuliza ni kwa nini CCM walikuja na azimio la kuzika Maadili ya Uongozi? Umeshawahi kujiuliza kwa nini Wafuasi wengi wa CCM wamekaa 'kidili dili' na 'kimagumashi' huku wakitegema ulinzi wa viongozi wa juu wa chama? Umeshawahi kuumiza kichwa na kuhoji sababu za rasilimali zetu kubakwa kirahisi pasipo kuwa na kauli nzito kutoka kwa uongozi wa CCM na viongozi wake?

Jibu ni rahisi sana. Chama kimepoteza taste ya kwa waasisi wake ambao ni wakulima na wafanyakazi. Na hakuna ubishi, chuki waliyonayo wananchi dhidi ya chama hiki ni kwa sababu ya madudu hayo niliyoyataja japo kwa uchache. CCM inaweza kutumia dola, propaganda na kila aina ya vitimbi katika kuendesha siasa zake lakini kama haitakaa chini na kuchora mistali vizuri japo kwa kugusa hayo masuala hapo juu hakika ni ndoto kutegemea mapya kutoka kwao.

Kubadilisha sekretarieti hakuwezi kusaidia kitu, kuvunja baraza la mawaziri ndiyo kabisa hakuwezi kuleta jipya lolote. Kuna watu wanawaona akina Mwakyembe na Magufuli kama wapigaji kazi kwelikweli lakini katika uhalisia ni wasaka sifa tu wasio na dira katika utendaji wao. Jiulize tu, nini dira na mipango ya Dkt. Mwakyembe katika uimarishaji wa Reli, Usafiri wa anga na majini na zaidi ufufuaji wa bandari zetu? Why anakuja na touches za kusaka sifa badala ya massive plans zinazolenga kufufua kisawasawa sekta ya usafirishaji na uchukuzi? Jibu ni rahisi tu, anafanya kile kitakachompa umaarufu wa haraka na rahisi.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Nape ukweli unabaki pale pale. I really appreciate juhudi zako binafsi na zile za wengine wachahce ndani ya CCM kujaribu kuifanya iwe ya wanachi na si ya mafisadi. Lakini naamini kuwa tunakosea kuwabeza wapinzani. Hapa ndio tunakosema, kama kweli tungekuwa na nia thabiti ya kutaka upinzani wa kweli hapa Tanzania tungekuwa nao. Kama kweli tungekuwa na nia ya kuendeleza nchi yetu na watu wetu tungekuwa mbali kuliko tulipo sasa.

I do reject the notion that Tanzania is lacking alternative party to govern the country, and use it as justification to let CCM keep on governing. Kwa hatua iliyofikia sasa Tanzania tunaweza kwenda vizuri hata bila chama, kama akitokea mtu mwenye nia akiwa madarakani kuna thousands of Tanzanians wanaoweza kuwa mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya nk nk nk. Tena hata wazuri kuliko wanasiasa. Kuna watanzania wengi sana nje ya siasa who are more capable, honest and visionary than those in offices now.

viongozi wa siasa si wengi kiasi kwamba tukasema CUF au CDM hawana watu wa kuongoza nchi.

By the way who has been torpedoing the opposition? Who has weaken them? kuna mzee mmoja alisema CCM ilikuwa inafanya hivyo. lisingekuwa jambo baya kama CCM ingekuwa ina deliver the goods.
 
Bongolander, kabla sijachangia mada yako napenda nichangie machache aliyosema Nape Nnauye hapo juu.
Kwanza, Nape yupo katika state of denial kuwa CCM ina matatizo. Anasema kuna jitihada za makusudi za vyombo vya habari kuchafua taswira ya CCM,anataka kutumianisha kuwa habari zote zinazohusu CCM na Serikali yake ni uzushi tu

Nape anapaswa kuelewa kuwa vyombo vya habari vimetoa mchango mkubwa sana katika kulisadia taifa kujua nini kinaendelea behind the curtain. Je, si kweli kuwa kuna wizi, ufisadi na ubadhirifu unaofanywa na CCM dhidi ya taifa?
Mfano, Nape anasema issue kama ya Kagoda haihusiani na CCM, well, je ni kwanini CCM imekuwa ikificha sana ukweli wa issue hiyo na nyingine kama kweli haihusiki.

Kuhusu mada ya Bongolander, niseme, kama alivyo Nape katika state of denial ndivyo walivyo viongozi wengi.
CCM imepoteza ile thamani yake ya kuwa chama cha umma na kwamba kila mtu ana nafasi ya kuchangia, kuongoza na kuelekeza. Kilichobaki sasa hivi ni CCM yenye kundi linaloongoza na wengine wamebaki kuburuzwa.

State of denial ni kuamini kuwa Katibu mkuu au makamu mwenyekiti au mwenyekiti ndio tatizo ndani ya chama bila kujua kuwa chama kimetekwa nyara. Ni kwa mtazamo huo, hata mabadiliko tunayoyaona ya uongozi kila uchao ni katika hali ya kutapa tapa na kukwepa ukweli. CCM haiwezi kurudi katika msimamo wake wa zamani kwasababu nguvu ya chama sasa ipo mikononi mwa watu wachache na si chama.

Chama tawala hakiwezi kuongoza tena kwa kufikiria namna ya kupanga safu za uongozi, kununua viongozi na hata kurithisha uongozi kutoka kizazi hadi kingine. Waziri mkuu mstaafu amesema kuhusu kukithiri kwa rushwa, Mangula alisema hayo na mwenyekiti naye alisema. Hii maana yake nini? Jibu ni kuwa chama sasa si sera na vision au mission isipokuwa sehemu ya ajira na dili za watu binafasi.

Kwa mtazamo huo tusitegemee kuwa ndani ya CCM kuna mtu mwenye fikra za kuiendeleza hii nchi kwa namna yoyote ile kwavile fikra zilizopo si za uongozi bali njia ya neema. Na wale wemye mapenzi mema na CCM na nchi hii hawapewi nafasi za kushiriki kwasababu nafasi za ushiriki ndani ya chama zinahodhiwa na kundi mahsusi lenye agenda zake na si za CCM

CCM hakihitaji kuwa chama cha wafanyakazi na wakulima, kinatakiwa kikubaliane na mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni kwasababu huko ndiko dunia ilipo sasa hivi.
Hilo litawezekana endapo CCM itakubali na kuamua kwa dhati kukabiliana na kundi linalowashikilia mateka.

Hakuna jitihada zingine zozote ziwe za vyombo vya habari, mikutano au iwavyo ambapo wananchi wataielewa CCM kama si kupambana kwa dhati ili kujiondoa katika umetaka ''hostage' unaofanywa na watu wachache wanaokihodhi sasa hivi.

Watekaji nyara ndani ya CCM wamefikia mahali pa kukifanya kionekane kama chama cha juzi. Katika ukongwe wa miaka 50 hakuna aliyetarajia CCM itaweza kukaa Dodoma kwa wiki nzima ikijadili makundi na kukimbizana na wala rushwa badala ya kuonyesha dira na uongozi wa taifa.

Wananchi wa kawaida wanaodhaniwa hawajui wameyaona ya Dodoma na kujiuliza kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na chama kinachokuwa kwa umri na kuvia kifikra, mkakati na mipango ya taifa hili?

Wanajiuliza ukongwe wa miaka 50 unatofauti gani na chama kilichoanzishwa juzi na je si wakati wa kubadili mwelekeo?
Hapo ndipo tunaona kuyumba kwake.

Nihitimishe kwa kusema, CCM haihitaji kutafuta mchawi iwe vyombo vya habari au upinzani.
Wachawi wa CCM wamo ndani na kwa bahati mbaya wanaogopwa na kila mtu.

Bila kukabiliana na wachawi hao hata kama kuna sera au viongozi wazuri kupindukia, bado hali ya CCM itakuwa mbaya chini ya umetaka.Kwani CCM ina upungufu wa sera au wasimamizi wa sera?

Hivyo ni lazima kwanza viongozi wa CCM wakiri uwepo wa tatizo kubwa sana, wawe na political will ya kukabiliana na tatizo, wajitahmini wapi walijikwaa na wapi wanapaswa kuelekea kufuatana na mazingira ya dunia ya sasa.

Kubaki na hadithi za kuorodhesha bara bara za lami huku watu wakizidi kuzama katika lindi la umasikini bila matumaini kunapelekea wananchi kukata tamaa na hapo ipo siku watasema ngoja tujaribu kwingine na ndio utakuwa mwisho wa CCM
 

Nnauye;

Concerning your explanation about EPA, you are doing yourself disservice. For, it seems to me that you don't understand how the procurement of services in government and organizations works. If you do, probably you are just here to try to deceive the public.

In financing and accounting, it takes months or even years from the time the service is rendered or goods are supplied to the time the money is paid to servicer or vendors. So the timing you explain above makes sense to me and it doesn't exonerate CCM. Rather, it reinforces the idea that CCM actually committed the crime, and there was an intent to cover up.

If the election was held at the end of 2005 and if KAGODA played its part to help CCM win the election, when do you expect CCM to repay the money back? 2004, 2005, 2006? In 2004 the service wasn't rendered yet. In 2005, it was the time the service was rendered. In 2006, the service was already consumed and it was time remit the payments.
 
Hii notion ya Chama cha wakulima na wafanyakazi ndiyo inanipa wasiwasi, hata kipindi kile hii notion inaletwa, Tanzania haikuwa nchi ya wakulima na wafanyakazi tu. Mchango uliotolewa na unaendelea kutolewa na sekta ya wafanyabiashara hauwezi kuwekwa kapuni au chini ya meza ili kuhararisha maandiko ndani ya katiba yanayosema nchi niya Ujamaa na kujitegemea. Kwa kufanya hivyo inakuwa ni catalyst for failure

CCM haiwezi kurudia 'misingi yake' ambao practically ilikuwa imposed by force katika jamii.

CCM kwa sasa inaachwa nyuma na jamii kila kukicha kwa sababu mpaka sasa haijui inasimamia nini na falsafa yake ni ipi?.

Kama kweli CCM ilikuwa inasimamia misingi ambayo ni endelevu, kwa miaka zaidi ya 45 toka Azimio la Arusha lilipoanziswa, maendeleo katika nchi yenye stability, peace and order hayaendani na hali halisi ya mazingira na natural resources zilizokuwapo na ambazo zipo kwa sasa.

Mpaka hapo CCM itakapo ondokana na hiki kivuli cha falsafa ambayo ndiyo kikwazo katika maendeleo ya jamii ya sasa, itaendelea kubaki nyuma na jamii itachagua chama kingine kinachoendana na kasi ya mabadiliko yao katika siasa, uchumi na kijamii.

Inasikitisha unapokuwa na viongozi ndani ya CCM wanaosema CCM bado haina mpinzani wa kweli. Kwa kiongozi makini anayejua historia ya Tanzania angejua kuwa mpinzani wa CCM siyo vyama vya upinzani bali ni wananchi wenyewe. Vyama vya siasa ni gari tu ambalo wananchi wanadandia kuwafikisha kule wanakotarajia kufika. Ilianzia kwa NCCR-Mageuzi na sasa ni CHADEMA.

Kama CCM itaendelea kushindwa kwenda na wakati na matumaini ya wananchi, wananchi watatafuta njia nyingine yeyoye ile ili kukidhi haja ya matarajio yao na mabadiliko katika jamii.
 

Mchambuzi you have made a very candid assesment of the current situation. Unajua kuna jambo ambalo watanzania bado tunakuwa wazito kuelewa, hasa ndani ya CCM kwenyewe. Viongozi wanatamba kuwa CCM imelinda order and stability, as if order and stability is the end and not the means to prosperity. In fact wanasahu kuwa wanajidhalilisha na kujionesha kuwa ni wajinga, kwa kusema tumekuwa na amani kwa miaka 50 lakini kimaendeleo tuko nyuma kuliko nchi nyingi ambazo zimekuwa kwenye vurugu na vurumai tangu uhuru. This is what makes me sick.

In fact kuna capital kubwa sana Tanzania ambayo nchi nyingine haina, lakini capital hiyo inachezewa sana na CCM mpya(CCM ya mafisadi). Kwa sasa tumeweka mbolea ya kutokea vurugu kubwa ambazo itakuwa vigumu sana kuzi-contain. Si siri sasa hivi vitendo vya kuuana, kuchochea udini, kulinda wezi na kuadhibu na kuuwa walinga wezi ndio zinaendelea sasa. Kwa sasa hali si mbaya lakini wananchi wakijua undani wake tunaweza kuwa pabaya sana. CCM inajipa credit ya amani na utulivu bila kujua kuwa ni watanzania wote wanaotakiwa kupewa credit hiyo.

CCM kama chama haitaki kukubali ukweli kuwa imetu-fail watanzania, inaamini kuwa ina haki miliki ya kutawala Tanzania na inatakiwa kulinda hakimiliki hiyo, hata iwe kwa gharama ya kuwagawa watanzania na kuwaibia.
 
Bongolander,

Sidhani kama ni sahihi kuchukulia yanayofanywa na CCM kama ni strategy as long as wananchokifanya sio kitu kitakachotuletea au kutuelekeza wananchi kwenye ubora wa kitu chochote kile katika maisha yetu; huu ni uhuni tu!
 
Last edited by a moderator:

Nape unataka kutuaminisha kwamba CCM haikutumia fedha za EPA kwenye uchaguzi kwa sababu gawiwo la kwanza kagoda ililipata 2006. Njia nzuri zaidi ya kukisafisha chama chako na hili ni kutueleza CCM ilipata wapi pesa za kufanya kampeni za kufuru namna ile.
 
CCM kama chama haitaki kukubali ukweli kuwa imetu-fail watanzania, inaamini kuwa ina haki miliki ya kutawala Tanzania na inatakiwa kulinda hakimiliki hiyo, hata iwe kwa gharama ya kuwagawa watanzania na kuwaibia.

I second you on this, vinginevyo how can we face the future chini ya CCM if Viongozi wake cant face the Facts?
 

Kuna tatizo lipo miongoni mwa wanasiasa wetu kuhubiri kisicho halisi na kuuficha uhalisia. Tusipo fika mahali tukajenga siasa za Black and White tutaendelea kupiga mark time.

Ukijaribu kuyaangalia maelezo ya Nape Nnauye ni wazi ni yaleyale ya kukwepa uhalisia wa mambo na kujenga siasa zetu na hata mambo yetu mengi ya msingi kwenye mazingira ya upotofu na ugizagiza. Hili lazima tuli address na liweze kutoweka. Lazima kama taifa tuwe wa kuuface ukweli no matter unauma kiasi gani.

Kusema hakuna mbadala wa CCM kwa sasa ni kudanganya watu. Maana CCM kama chama pamoja na structure yake ambayo imedumu kwa muda mrefu inatumia watanzania kama nguvu kazi katika kutekeleza mikakati, sera na mipango mbalimbali ya kitaifa. Watu hawa kwa maana ya watendaji hawamilikiwi na CCM pekee, chama chochote kinaweza kuwatumia.

Na tatizo tulilonalo si kukosa chama mbadala,lahasha! Tatizo tulilo nalo ni namna ya kupanga mipango, ilani na mikakati yetu. Aidha, tatizo lingine ni matumizi yasiyo sahihi na ya hovyo ya rasilimali watu na rasilimali asili tulizo nazo. Hapa ndipo tulikokwama. Mipango iliyokuwepo huko nyuma kama nilivyoitaja kwenye mchango wako hapo juu imetelekezwa. Kuanzia Azimio la Arusha, Vyama vya Ushirika, Ujenzi wa viwanda, Mapinduzi ya Kilimo nk.nk. vyote vime paralyse. Kwa sasa hakuna tunaloshika. Strategically hatujielewi. Hata Nape akiulizwa sasa hivi baada ya miaka 20 tutakuwa wapi hana jibu. Hata viongozi wetu wa juu hawawezi kujibu hili.

Tunaposema mbadala ni fikra mpya katika kupanga, kuja na sera, ilani na mipango ya kumgusa na kumkomboa mtanzania wa kawaida. Kuwa na watendaji visionary ambao watagawa rasilimali watu na asili accordingly na hivyo kuleta maisha bora kwa watanzania. Hili halipo kwa sasa, na limekosekana ndani ya CCM hivyo lazima watu wenyewe watalitafuta nje ya chama hiki. Kusema kwamba hakuna chama mbadala inaweza kwa neno tamu kwa mtu mmoja mmoja lakini wenye kujua umbadala wa chama ni wenye kuweka viongozi madarakani ambao ni wananchi kwa ujumla wao.Na wakati ukifika wala hawaulizi, wanafanya mabadiliko tu.

Hapo juu unasema media ndizo zimekuwa zikikichafua CCM na kwamba ndiyo sababu ya hali kuwa ilivyo sasa. Nadhani unajaribu kuukwepa ukweli kwamba uwepo wa upinzani unaoungwa mkono na wananchi wengi kumekuwa ni mkuki kwa CCM. Hata mpepesuko uliokikuta chama hiki kiasi cha kuvunja baraza la mawaziri mara kadhaa na hata kubadilishwa kama nguo kwa sekretarieti ni ili kujaribu kwenda na kasi ya upinzani uliopo sasa.

Hili halihitaji elimu kubwa sana kuling'amua.Katika vikao vingi vya CCM makabrasha yamekuwa yakionesha hofu ya upinzani kutamalaki. Hata uchaguzi uliopita wa CCM agenda ya upinzani kutishia uhai wa CCM ndiyo imekuwa kete ya kuwapa watu uongozi. Kusema kwamba upinzani imara haupo ni kukwepa kivuri tu lakini ukweli unafahamika. Na ni bora ukaishi kwa kuukubali ukweli ili uweze kupona na kujikosoa kuliko kuupuuza.
 
Last edited by a moderator:
CCM inawezekana kurudi katika misngi yake ya awli, ila inakibidi chama kichukue maamuzi magumu katika kufanikisha hilo jambo, tofauti na hapo tusubiri ndani ya CCM kunatokea chama kingine ambacho kitafuata misingi iliyo wekwa na CCM ya wafanyakazi, wakulima na yenye kujali maslai ya taifa na wananchi wake kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…