Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,210
- Thread starter
- #21
CCM inawezekana kurudi katika misngi yake ya awli, ila inakibidi chama kichukue maamuzi magumu katika kufanikisha hilo jambo, tofauti na hapo tusubiri ndani ya CCM kunatokea chama kingine ambacho kitafuata misingi iliyo wekwa na CCM ya wafanyakazi, wakulima na yenye kujali maslai ya taifa na wananchi wake kwa ujumla.
Mheshimiwa Juma, suala la maamuzi magumu hilo haliwezekani kabisa, limesemwa sana lakini kila kikao cha juu cha chama kikikutana unachosikia baada ya mkutano ni kauli tu. Hakuna uamuzi mgumu wowote uliochukuliwa na kutekelezwa.
Labda tufafanue kidogo tunaposema chama kifanya maamuzi magumu. Maana yake ni kuwa miiko ya uongozi na maadili kwa viongozi wa chama vitekelezwe na kusimamiwa ipasavyo. Hilo likifanyika matatizo mengi yanaweza kupungua, lakini ukiangalia kwa undani, kufuata miiko ya uongozi na maadili yake, nia sawa na kuwaambia mafisadi waache matendo mabaya wanayofanya, na wachukuliwe hatua kutokana na makosa yao. The thing is, who has that courage?
Kuna waheshimiwa ambao hata ndani ya chama wanasifika kwa uchafu lakini hakuna aliyethubutu kuwaondoa, tena hata wanatoa vitisho kuwa mkitufukuza mtakiona. Sana sana kilichotokea ni kusema wajivue gamba, toka hilo limesemwa hadi sasa, ni Rostam peke yake amejiweka pembeni kidogo, amechukua remote control. Wachafu na machafu mengi yanaendelea kuwepo na hakuna cha maana kinachofanyika. Kimsingi mafisadi ndio wana fina say ya mambo ya chama, na kurudi kwenye maadili na miiko kunakwenda kinyume na maslahi yao binafsi.
Kumeguka kwa CCM, kama kukitokea itakuwa ni rehema kutoka kwa Mungu, kuna uwezekano ikatokea CCM ile ambayo tulikuwa nayo miaka 20 iliyopita. CCM ambayo mwenzetu Nape Nnauye anaipigania.