Mtu66
Senior Member
- Jun 26, 2007
- 165
- 3
CCM, CHADEMA wakatana mapanga
Mmoja anyofolewa sikio, ashonwa nyuzi nane
na Mwandishi wetu
KAMPENI za uchaguzi mkuu wa urais, ubunge na udiwani, zimeanza kuingia dosari baada ya vijana wanaosadikiwa kuwa kikosi cha Green Guard wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kutembeza kipigo kwa kuwakatakata mapanga zaidi ya vijana wanne wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika jimbo Busanda mkoani Mwanza. Habari zilizopatikana jana kutoka Busanda zinasema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 9, wakati mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Lolensia Bukwimba, alipokuwa akirudi kwenye mikutano yake ya kampeni.
Akizungumza na Tanzania kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Busanda Mazemle Joel alisema tukio hilo ni moja ya matukio mabaya kutokea tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu Agosti 21, mwaka huu.
Huwezi amini kwamba hivi sasa kuna vijana wangu wanne hali zao ni mbaya, wamekatwa na mapanga na vijana ambao walikuwa wakimlinda mgombea wa CCM; walishuka kwenye gari lake na kuanza kutembeleza kipigo, alisema Joel.
Alisema Green Guard, wakiwa kwenye gari la mgombea walikuwa wakionyesha alama ya kidole gumba ambayo hutumiwa kama salamu ya wana CCM, lakini walijibiwa kwa kuonyeshwa alama ya vidole viwili ambayo hutumiwa na CHADEMA kama alama ya salamu ya chama.
Aliwataja vijana waliokatwa kuwa ni Isaka Samweli (25) ambaye amekatwa vibaya kichwani na kushonwa nyuzi zaidi ya 10, Salum Mohamed (amechanwachanwa sehemu mbalimbali za mwili), Minani Atanas (amekatwa sikio lote la upande wa kulia) na Emannuel Lameck.
Mmoja wa majeruhi hao, Mohamed, alisema, Nilikuwa nauza miwa yangu, hawa jamaa wakapita mbele yetu wakituonyesha alama ya dole gumba na mimi nikawajibu kwa alama ya vidole viwili; eti hilo ni kosa ndiyo wakashuka kwenye gari na kuja kunipiga.
Alisema tukio hilo lilitokea mbele ya Bukwimba na mgombea udiwani wa CCM maarufu kwa jina mama Mingisa ambao kwa pamoja hawakuchukua hatua zozote.
Alisema moja ya tatizo kubwa lililoko Busanda ni vijana hao wa CCM, kila wanapofanya unyama huo wakipelekwa polisi hawachukuliwi hatua zozote, jambo ambalo wamedai si haki.
Tumekosa majibu hawa jamani kila tukiwapeleka polisi wanaachiwa baada ya muda mfupi, hatujui wana uhusiano gani na polisi, tunataka wachukuliwe hatua zinazostahili.
tunawaelewa vizuri; yupo mtu anaitwa Mwanza Mwanza huyu alikuwa na kufuli la baiskeli na nondo akaanza kunipiga hovyo hovyo bila kosa lolote, nimeumia vibaya sana mgongoni.
Naye mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, Finias Magesa, alisema hali ilipofikia sasa inatisha na kuvitaka vyombo vya dola kutenda haki dhidi ya wahusika.
Sasa ni wazi kwamba amani iko hatarini kutoweka, tunaliomba jeshi la polisi kutenda haki, vitendo hivi havikubaliki hata kidogo jamani haki itendeke hali ni mbaya kule Rwamgasa, Kaduda na Nyamigota, alisema Magesa.
Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Nonocius Komba, alipoulizwa alisema mpaka jana alikuwa hajapata taarifa za tukio hilo na kuahidi kulifuatilia kisha kulitolea taarifa leo.
Kwa upande wake, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Rajab Kundya, alipotafutwa na gazeti ili kuelezea tukio hilo, alisema jana kutwa nzima alikuwa kwenye msafara wa mgombea urais wa chama hicho, Jakaya Kikwete, hivyo kuahidi kutoa ufafanuzi zaidi leo.
....Vyombo vya DOLA acheni ushabiki..Keshokuwa mtanawa DAMU ya wake au wajomba zenu..