CCM - Chama kinachotoa uwanja sawa kwa kila anayetaka kuwania nafasi za kuwakilisha wananchi

CCM - Chama kinachotoa uwanja sawa kwa kila anayetaka kuwania nafasi za kuwakilisha wananchi

Environmental Security

Senior Member
Joined
May 21, 2020
Posts
181
Reaction score
262
Chama Cha Mapinduzi, ndicho chama ambacho kinatenda kwa usawa kabisa bila kubagua katika kuruhusu wanachama wake kuwania nafasi mbalimbali za kuwawakilisha wananchi katika vyombo mbalimbali vya maamuzi, hilo unaweza kuthibitisha hata kwa kupitia kwa Rais wetu mpendwa JPM ambaye aliingia katika kuwania urais bila kuwa na kambi wala kubebwa na mtu ndani ya chama, na pia mchakato mzima ulithibitisha kuwa hata wewe maadam unatimiza vigezo vya kikatiba, waweza kuomba nafasi ya kuwawakilisha wananchi kwa ngazi yoyote ile ukifuata katiba na miongozo ya chama, sio kama baadhi ya vyama ambavyo wapo wenye chama na hao wanaweza kuamua chochote watakavyo na wanajiita ni wanademokrasia.

Nyakati za uchaguzi, ndani ya CCM kila jimbo haijalishi ni la nani awe spika, waziri au yeyote, lazima utaona kuna watu wamejitokeza kuchuana naye ili kupata nafasi ya kuwakilisha wananchi, lakini kwa wenzetu kuna watu wao ni wao na kila wakati wa uchaguzi wao ndio wagombea na akijitokeza mtu kuchuana naye basi atapewa majina yao flan flan hasa la usaliti.

Kwa utaratibu uliotangazwa wa kuwachuja wagombea wa ubunge kupitia mkutano mkuu wa jimbo, CCM kwa mara nyingine imedhihirisha uimara wake na utayari wa kuruhusu watu waamue juu ya nani wanayemtaka awawakilishe, sio kupangiwa na viongozi wachache (Big up sana CCM).

Na mimi napenda kuchukua fursa hii kukaribisha vijana wote wazalendo wanaolipenda taifa lao, pamoja na waTanzania wenzangu wengine wote ambao wanakidhi vigezo vya kukatiba kuweza kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi, wajiunge na CCM (kama bado hujajiunga) na zaidi wajitokeze kuomba nafasi za kuwawakilisha wananchi, Chama kimeweka ulingo sa
wa, karibuni sana kwa ujasiri, kwa uzalendo Tujenge taifa letu kupitia chama chetu waTanzania.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
 
Ngoja tuone Magufuli akiondoka madarakani 2025 kama mtaendelea na haya maisha yenu ya kinafiki.
 
Polepole kawapiga marufuku wanaccm kuchukua fomu ya kugombea urais Wa muungano.Anasema mgombea tayari chama kinaye, wanaccm wanauliza kwa vikao vipi?
 
Back
Top Bottom