CCM: Chuo cha Dodoma kiitwe JK University

Si waanze na hii SHULE hapa waipe jina la Mtu yeyote wa CCM wanayemtaka. Kwa mfano MWIGULU NCHEMBA Primary School, Makamba PS, Pinda PS, JAh-Kaya Primary School, Salma Shule ya Msingi, Shule ya vidudu Abbas Kimbisa, etc.


Mbona nyingi tu shule za hadhi ya jina lake, nashangaa wanarukia mapendeezo ya CHADEMA kuibadili CHUO CHA MADINI CHA DODOMA kuwa .........
 

Attachments

  • elimu bora 6.JPG
    50.8 KB · Views: 48
Akisha kufa sawa kiitwe hivyo!
Hata sokoine kiliitwa baada ya kufa, nyerere intanational, chuo cha mwalimu nyerere, huo ni uchwara hilo jina ni baya halipendezi.
 

basi maadam umetaja ya chadema...tupendekeze kiitwe slaa !!
Nadhani utaridhika...kwani dar es saaalm inter. Arport si cha public? Kwa nini uliitwa nyerere ? Si heshima kwa baba wa taifa?
Utakataa kama una ubinafsi tu...lakini ana stahili....
Na hilo ni ombi la ccm mkoa dodoma...kama serikali watakubali ama laa ni jambo la kusubiri....
Si unasema katiba ni la chadema? Mbona kalikubali? Wala sio shinikizo....ni ukomavu wa kisiasa wa jk...tukubali ....ana makosa na mapungufu yake lakini jjk..ni mwanasiasa imara na aliekomaa...
 
Jamani msishangae sana.Katika CCM hakuna vichwa vinavyofikiria sawasawa kazi yao kila kukicha ni kujipendekeza tu kwa wakubwa wao ili wapewe fadhila.Wananchi wa Dodoma na watanzania kwa ujumla tukatae kubadilishwa jina la chuo hicho.
 

Sidhani kama lilikuwa pendekezo la CCM uwanja wa ndege uitwe Mwalimu Nyerere International Airport na sidhani kama aliomba. Iconic leader hupewa heshima hizo tena na watu wengine tu na si familia yake.

Mimi sikusema kiitwe Slaa, suala la CDM limekuja baada ya wewe kusema hilo ni wazo la JK kuanzisha kile chuo. CCM ilikopi na kupaste wazo la CDM. Jomo Kenyata, Nelson Mandela na yeye akaona ajichomeke, loh, hebu niambie wanafanana hao?

Huo ukomavu wake nadhani unao wewe moyoni mwake, mara nyingi mimi humsikia tu akisema 'anashangaa' kwenye mambo ambayo alitakiwa achukue hatua, labda huo ndio ukomavu unaouzungumzia.
 
Kuna ubaya gani Au lipi la ajabu, Kwani haijatokea hapa duniani. SOKOINE N.K.

Hakuna kitu kibaya kama kuweka siasa kwenye elimu (na mambo ya utaalam). Tusisahau tuna mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo mtu hawezi kuamua jambo la umma kwa kushauriana na wanachama wenzake tu. Mi nisingekuwa na shida kama pendekezo hili lingeanzia bungeni-mahala ambapo angalau kuna neutrality ya kiasi fulani. Hali hii ya kuifungamanisha UDOM na CCM badala ya kuifungamanisha na watanzania inakipa chuo taswira mbaya na kufunika jitihada kubwa iliyofanywa kujenga chuo.

Hiv shahada ya heshima ya uzamivu aliyopewa na UDOM haitoshi kuonyesha mchango wake? Mnara wa CCM ulio ktk "lango" la kuingilia UDOM hautoshi? Ni muhim sana eneo la taaluma liwe huru ili fikra huru ziweze kuchipua. Na hapa ndipo UDSM inapoonyesha njia-UHURU NI HEKIMA.
 


nilidhani ni julius kambarage..!
Kumbe ni jakaya??
Ok.kwaheri..
 
nilidhani ni julius kambarage..!
Kumbe ni jakaya??
Ok.kwaheri..

Jamani Mnyonge mnyopngeni lakini haki yake mpeni, Jamaa anastahili kwani amewekeza sana ktk elimu. Shule za Kata pamoja na changamoto zake nyingi lakini angalu elimu ya sekondari siyo anasa kama zamani
 
jamani mnyonge mnyopngeni lakini haki yake mpeni, jamaa anastahili kwani amewekeza sana ktk elimu. Shule za kata pamoja na changamoto zake nyingi lakini angalu elimu ya sekondari siyo anasa kama zamani



ni kweli siyo anasa kama zamani
je uko radhi kumwacha mwanao anapata elimu ile kama kweli unaufaham umuhimu wa msingi imara wa elimu??
Tuwe wakweli katika hilo
 

Mi sioni tatizo kabisa hata wangekiita Mama Salma Kikwete University! Yawezekana Kimbisa anatambua undaifu wa hicho Chuo, hivyo hata akikipa jina lolote lile kama KIMBISA UNiversity haoni tatizo. Sisi tunatambuka kwamba Chuo Kikuu Cha Dodoma ni Chuo muhimu sana kwa Taifa letu na si vizuri misingi mizuri ikaanza kubomolewa kwa kupachika majina ya wakubwa. Afadhali wangekiita Mkapa University!
 

Mi sioni tatizo kabisa hata wangekiita Mama Salma Kikwete University! Yawezekana Kimbisa anatambua undaifu wa hicho Chuo, hivyo hata akikipa jina lolote lile kama KIMBISA UNiversity haoni tatizo. Sisi tunatambuka kwamba Chuo Kikuu Cha Dodoma ni Chuo muhimu sana kwa Taifa letu na si vizuri misingi mizuri ikaanza kubomolewa kwa kupachika majina ya wakubwa.
 
Huo ndio ukengeufu mkubwa... ni sawa na kuwatukana watanzania kwa kumpa heshima hiyo kikwete...
 
Kwani heshima mpaka kile chuo kiitwe jina lake mbona wapo walipa kodi kibao laikini hawpewi chochote tuache umwinyi bwana kiache kiitwe UDOM.Heshima atapata mbinguni duniani hakuna heshima.
 
Nimesikiliza Channel Ten eti CCM wanapendekeza UDOM iitwe Kikwete University. Hii si ni dharau kwa Tasinia ya Elimu nchini? Sasa nimeamini maneno ya Karume kuwa ndani ya vikao vyao kuna watu wana akili za samaki.
mbona mimi sikumsikia aisee, inawezekana akawa miongoni mwa watu waliosema 'ukweli 10 bora' katika karne iliyoisha na hii!
 
Jamani Mnyonge mnyopngeni lakini haki yake mpeni, Jamaa anastahili kwani amewekeza sana ktk elimu. Shule za Kata pamoja na changamoto zake nyingi lakini angalu elimu ya sekondari siyo anasa kama zamani

kama vipi tafuta shule ya kata moja ndo ipe jina lake hasa ile ambayo inajikongoja bcoz nayo yeye kahamasisha
 
Huo ndio ukengeufu mkubwa... ni sawa na kuwatukana watanzania kwa kumpa heshima hiyo kikwete...
nasikia hata hilo daraja la maragarasi Waha wanataka walibadilishe jina baada ya kugundua kuwa pesa zinazolijenga ni za msaada wenye interest kubwa na 10% kibao
 
Sasa hivi utasikia na lile daraja linalojengwa kwa fedha zetu za NSSF linapewa jina la mtu kama lilivyopewa lile la RUFIJI. Majina yenu jamani yaandikeni mioyoni mwetu kwa uadilifu na utumishi wema na sio kwenye mabango, mnaitia laana nchi.

Basi Gereza la Segerea liitwe jina la Babu Seya kwa kuwa yeye na ukoo wake watakaa huko mpaka watakavyokufa
 
hakuna ubaya.....anastahili heshima hio
kwa lipi alilolifanya mkuu??? udom imetengenezwa kwa fedha ya ccm au wananchi na wadau mbali mbali??? au ndo umetumwa?? tumia kichwa kufiria na sio mak*****o!!!
 
Jamani Mnyonge mnyopngeni lakini haki yake mpeni, Jamaa anastahili kwani amewekeza sana ktk elimu. Shule za Kata pamoja na changamoto zake nyingi lakini angalu elimu ya sekondari siyo anasa kama zamani
sasa kuna maana gani mtoto anamaliza miaka mnne shule ya kata(nieleweke sio ya walioukata ni ya kata) alafu anapiga div zero!!! si bora angekaa nyumbani afanye biashara kuliko kupoteza 4years!!!! shule walimu hamna,vitabu hakuna, alafu mwisho wa siku wanapiga zero na div four wote.,....ina make sense kweli??? kweli watu wadhaifu watampenda dhaifu!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…