Hivi wewe,huko kwenu hamna utaratibu wa kumpomgeza/kumsifia mtu mara anapofanya jambo lolote zuri????,wenzio wengi humu wanaipongeza CCM kwa hatua hii ambayo inalenga kurudisha demokrasa ndani ya Chama lakini wewe kama kawaida yako ni lawama tuuuuu..aaaaaarghhh,unaboa sasa.Halafu hivi kwa akili yako unategemea CCM itaanguka katika uchaguzi wa mwakani???,lol(hizo ni ndoto za mchana kweupeeee),katika hali ya kawaida hauwezi kumfananisha/kumpambanisha JK na Lipumba wewe,CCM haijaanguka na itachukua muda kuanguka(kwa upinzani dhaifu uliopo Tanzania,maana ndani ya upinzani tayari kuna upinzani),sanasana CUF ndo inaelekea kufa(kifo chake kitakuwa baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwakani),CUF hamna sera zaidi ya vurugu na lawama/visingizio kibaoooo.Halafu unasema CUF ina mbinu za kimataifa(mataifa gani hayo ndugu,ya Amerika,Ulaya ama Arabuni??)!!!!Lol,what is mbinu za kimataifa wewe Sultani MWIBA??,Hizo si ndo zimewafanya mgaragazwe na CCM katika chaguzi zote zilizopita???,ama unazungumzia mbinu za ushindi wa Pembaa,lol....Kalagabaho
Kumpongeza Sultani CCM ni mwiko kwa Mtanzania mwenye uchungu na Taifa hili ,unapongeza ,hivi ni kitu gani cha kupongezwa ambacho kitamnufaisha mwananchi wa kawaida ,kama utaratibu mbona sio mpya ,ni vyama vingi tu vyenye kujali maslahi ya mwananchi ndio viinatumia sera hiyo.
Hawa majambazi walikuwa wameshikilia hatamu ya kila kitu ,hata mtu achaguliwae na wananchi kutoka huko vijijini ,wao walikuwa wanapinga na kulitupilia mbali wakitoa sababu hizi na zile ,eti kupongeza baada ya miaka 50 ya utawala ndio unafahamu kama ilikuwa wakitenda zambi ,hivi watu hawakulalamika katika miaka hiyo ? Unataka kuniambia kuwa Demokrasia ndio imemfikia Sultani CCM ?
Hawa ni wa kulaaniwa si wakupongezwa ,hivi huku ndio kujisafisha na mizambi iliyowatapakaa mwili mzima ? Nakushangaa sana unaposema watu wote hapa JF wanapongeza ,hakuna anepongeza ila aliekuwamo humo kwenye ufuasi wa Sultani CCM ,mnapongezana wenyewe kwa wenyewe kama mlivyozoea.
Mwenye akili inayoyatazama mambo yanayotokea Tanzania hawezi kupongeza hatua hiyo ,kwani ni hatua nyingine ya kutaka kufanya aina nyengine ya ufisadi.
Utawala wa Sultani CCM umepotea kabisa katika giza la dhulma ni vigumu kujiweka sawa ,na kuweza kuiongoza nchi hii katika misingi ya sheria inayoheshimu haki za wengine ,ni kuwafanya watu punguani kama hao wanaosema kuwa hatua iliyofikiwa ni muhimu ,muhimu kwa nani ? Lazima ujiulize ? Hakuna Mtanzania yeyote ambae ataichagua CCM na kufaidika na mfumo huo uliokuwa mpya kwao ni kuwalaghai watu tu na kutaka kujionyesha kuwa wanajali maslahi ya wengine ,uwongo mkubwa kuliko yote.
Mwananchi aliefungua na kufunguka akili hawezi kuhadaiwa na janja hii ,njia nyingine ya kuwachota watu akili zao ,huku ni kutaka kuwadanganya watu.
Vinara wa Sultani CCM wanajua wazi kuwa ikiwa system ambayo kwao wao ni mpya itatumika basi ni hatari kuliko mwanzo ,hivyo mbinu na mizengewe itafanywa huko huko kwenye mizizi hukohuko vijijini watawafuata na kufanya ya kufanya ,kijana kaa macho naona wewe si mwenyeji wa siasa za Sultani CCM.
Sultani CCM hatakubali kufanyiwa ujinga wa mnayoyatamani ,hakubali hata siku moja atawaingilia huko huko matawini na kuwachafua ili kuhakikisha wateja wake wanapata ajira ,we unasema tu eti tunapongeza ,ndio maana yake unapongeza kwa habari za juu ,ingia deep uwone siasa ,usifikiri siasa ni kukaa na kuandika ili uonekane na wewe unafurahia demokrasia ya Sultani CCM ,wewe unafurahia wenzako wana hesabu zingine kabisa ,ndio hivyo kama ulivyomsikia Kilango ameona mbali sana kuwa sasa mambo ni hatari ,Sultani CCM anataka kuibuka na wateja tokea chini jambo ambalo litawawacho mbali wananchi kulalamikia ionekane kuwa ni chaguo lao au sivyo ?
Mbinu hizi ni vizuri kuzijua na mapema hivyo lakufanywa ni kwa wananchi kumkwepa Sultani CCM kwa njia zote anazo kuja nazo.
Hiki Chama kimeshakufa hakuna ambae ana kifurahikia hata mmoja isipokuwa wache ambao hupatiwa ajira za kufagia kwenye maofisi ya serikali na ya Chama chao ,Mwananchi ambae hana hisa katika Chama hiki basi ujue hana imani nacho maana ni Chama kinacho jali maslahi binafsi.