Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Kelele za Oktoba, 2025 zimerudi tena za kuhubiri amani amani! Acha inyeshe tena tuone panapovuja
========
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita kimewataka Watanzania kutoshiriki maandamano yanayodaiwa kufanyika Julai 7, kikisema hatua hiyo inaweza kuhatarisha amani na utulivu wa nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Wilayani Geita, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Wilaya ya Geita, Gabriel Masunga Nyasilu, amesema kuwa maandamano hayo si sehemu ya utamaduni wa Watanzania katika kuwasilisha maoni, malalamiko au madai yao kwa Serikali.
Soma Pia: Waziri Mkuu tumekuelewa, tutailinda amani ya nchi zaidi ya nyeti zetu
Nyasilu amesema CCM inaamini kuwa Tanzania ina mifumo na njia halali zinazowezesha wananchi kufikisha hoja zao kwa mamlaka husika kwa njia ya amani na mazungumzo, badala ya kushiriki vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa nchi.