hp4510
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 7,235
- 7,392
Kwa miaka 5 mfululizo CCM imefanya mambo mengi ambayo yangetosha kuwa mabango yao ya kampeni kwenye uchaguzi wa 2020. Kazi zilizofanyika awamu ya tano pia zilijumuishwa kwenye wimbo wa Harmonize unaoelezea mafanikio ya awamu ya tano, na wimbo huu ulitoka mapema sana na kuchezwa kwenye media zote nchini hata kabla tarehe ya uchaguzi haijatangazwa.
Mafanikio ya awamu ya tano yanaonekana kwa macho ya nyama kwa kila mwenye macho, lakini pia yamehubiriwa sana katika kipindi chote cha miaka 5 katika kila mkutano na kila mwenye masikio amesikia. Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwi sikia. Kusema ukweli sikutegemea kuona mabango mengi tena ya kampeni ili hela za mabango zielekezwe kwenye kitu kingine japo hata kwa kuweka nyasi bandia kwenye viwanja vya CCM ili soka lichezwe kwa ufasaha kwenye viwanja vyote.
Hizi gharama za mabango tena sijui ni nani alizipendekeza, kwangu mimi naona mabango hayakuwa na sababu na hayana mchango kwa kampeni za CCM hasa za Urais, maana mafanikio ya CCM na serikali ya awamu ya tano yalishasemwa sana na viongozi wote wa chama na serikali, hata wanapopiga kampeni wanayarudia tena yale yale ya ndege, reli, bwawa, rushwa, umeme na hospitali.
Au wenzangu JF mnaonaje? Gharama hizi za kutengeneza mabango ulikuwa ni ushauri kutoka kwa nani kwa malengo gani? TAKUKURU hebu pitenipiteni huko pia.
Kunywa soda kwa bili yangu