CCM - Hebu jaribuni kuwa reasonable

jebibay

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2012
Posts
1,431
Reaction score
640
Wakuu,

Fact moja katika bunge hili la katiba ni kwamba CCM wana uwakilishi mkubwa kupita makundi yote ukiyaweka kwa pamoja !. Kutokana na huu ukweli, ni wazi kwamba CCM watakuwa wengi katika kila kamati itakayoundwa na inawezekana kabisa wenyeviti wengi wa kamati (kama sio wote) wakatoka CCM !

Kwa kuzingatia ukweli huu, wajumbe wa Bunge la katiba ambao ni wana CCM wanapoongelea kundi la walio wachache wanajua kabisa katika kamati zote wao hawatakuwa katika hili group la wachache...na kwa sababu wako wengi wanaweza wakapitisha hoja zao kwa urahisi tu, ambazo watazitetea wenyewe kwa sababu wenyeviti watakaoziwakilisha mostly nao watakuwa wana CCM...Kwa hiyo CCM mkitaka mnaweza kutengeneza katiba yenu halafu mkaiita ya waTz. Baadhi yetu tunaamini mtafanya hivyo, na tumeshaandaa kura zetu za HAPANA tayari tayari, kwa sababu hatutakubali katiba mpya feki ! Heri tujue hatuna katiba ili tuendelee kuidai kuliko kuwa na katiba feki....

Tukiacha hilo la katiba mtakayoitoa kama itazingatia maoni ya wananchi au la, ninachotaka kuzungumzia hapa ni hii issue ambayo na nyie CCM mmekuwa mnaizungumzia mara kwa mara...issue ya amani, maridhiano, kuheshimiana na blah blah nyingine zinazofanana na hizo. Wakati mwenyekiti wenu wa Taifa, analiongelea hili, wengi tulimchukulia serious ingawa wengi wetu hatumwamini (ingawa ni Rais wetu) kwa sababu yeye kama mlivyo wana CCM wengi ni watu wa maneno tu na unafiki kwa kiwango kikubwa.

Na kuthibitisha wasiwasi wetu kwake ni pale matendo mlioanza kuyafanya CCM (under his watch) baada ya hiyo kauli yake. Matendo yenu yamekuwa completely contrary na lugha ya maridhiano, kutunza amani, kusikiliza wachache etc....Pinda naye jana bungeni, kama kawaida yake aliongea kidizaini hizo hizo, lakini kilichofuata Bungeni baada ya yeye kuongea ni kwa vijana wake kwenda kinyume kabisa na hiyo spirit ya wengi wape, wachache wasikilize.......

Ninachotaka kuwaambia CCM ni kwamba kila mtu ana redline yake...na ukivuka hiyo whether unataka au hutaki utatafuta kutokuelewana/shari, hata kama wewe ndio mwenye serikali....Just imagine, nyie mko wengi, mnaamua mnachotaka, mnapata nafasi kupitia wenyeviti wenu kutetea hizo hoja zenu.....halafu eti mnataka kulazimisha nyie HAO HAO ndio muwe midomo ya wale wachache ! Are you really serious !? Hivi mnafikiri nani atalikubali hilo ? Yaani wewe hukubaliani na mimi, halafu unalazimisha utetee hoja yangu! Tena kwa kunilazimisha ! Ndio maana Bungeni jana Lissu aling'aka na kusema hilo haliwekani....

Nyerere alisema kwamba....mtu mzima akikwambia jambo la kipumbavu ambalo anajua ni la kipumbavu na anajua wewe unajua ni la kipumbavu halafu ukalikubali anakudharau !. Sasa nyie mnafikiri nani atakubali jambo hili la kipumbavu ambalo mnataka kulilazimisha !

In summary ninawaomba muwe reosanable. Kuna vitu vingi mnaweza kufanya kwa wingi wenu...ingawa tutavipinga...bado mnaweza kuvipitisha, ila mnapofikia hatua ya kulazimisha NYIE HAO HAO muwe sauti yetu wakati wa-kuwapinga nyie, hapo mnavuka mipaka (redline) na kwa VYOVYOTE vile, hakuwezi kuwa na maelewano.....

Please, be reasonable !

UPDATE :
Ninashukuru busara zimetumika na muafaka umepatikana katika hili. Muafaka ni kwamba Mwenyekiti atapresent hoja zote (za wengi na wachache) halafu wale wachache watamchagua mmoja wao na yeye atafafanua hoja zao kwa muda wa nusu saa. Huku ndio kuwa reasonable na ninampongeza sana Mheshimiwa Kificho kwani najua ana mchango mkubwa katika busara hili....

 
Kweli CCM janga...hawana utu.
Wamekaa kimaslahi tu.
Siku wakifa watachomwa moto mkali sana kwa dhuluma wanazotufanyia wanatanzania.
 
Wadau, naona kuna upotoshwaji mkubwa unajengwa katika suala hili. Kabla sijaeleza suala hilo, naomba niwakumbushe kilichotokea jana kwenye ukumbi wa Bunge.

Ni kwamba, wakati wa session ya asubuhi, kikao hakikufanyika baada ya wajumbe kutofautiana jinsi ya kujadili au kuwasilisha Rasimu ya Pili ya Kanuni za Bunge Maalum. Kama mnakumbuka vizuri, siku ya Ijumaa iliamuliwa kuwa Kamati Maalum iliyoundwa kushughulikia Kanuni iliambiwa iandae Rasimu ya Pili ya Kanuni za Bunge Maalum na iliagizwa kuwa wajumbe wapate Rasimu hiyo ya Pili siku ya Jumamosi. Hata hivyo, hadi jana jumatatu, wajumbe walilalamika kuwa wengi walipata nakala hizo siku ya Jumapili na wengine mpaka jana walikuwa hawajapata. Kutokana na hali hiyo ndipo wakaomba wapewe nakala siku hiyo, wazipitie, wafanye marekebisho na hatimaye wayawasilishe.

Sasa katika hilo la wajumbe kuwasilisha marekebisho yao, ndipo mjadala ulipoibuka wa namna ya kuwasilisha. wapo wabunge waliotaka marekebisho yao wayawasilishe moja kwa moja bungeni huku wengine wakitaka wawasilishe kwanza kwenye kamati, kamati iyachambue na kuyaingiza kwenye Rasimu ya Pili ya Kanuni. Hata hivyo, hoja hiyo ya pili iliungwa mkono na wabunge wengi na ndipo ilipoamuliwa kuwa wabunge wenye marekebisho, wayawasilishe kwenye Kamati Teule hadi saa saba na saa 11 Bunge lirejee.

Bunge liliporejea jioni, Mwenyekiti MZEE KIFICHO alimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati MAHALU asome Rasimu ya Pili ya Kanuni. MAHALU alipitia ukrasa kwa ukrasa na kifungu kwa kifungu kusoma tu marekebisho yaliyofanywa. Baada ya zoezi hilo, ndipo Mwenyekiti Kificho alipotumia busara zake kuwaalika viongozi muhimu waliopo Bungeni kuzungumza na wajumbe hasa ikizingatiwa kuwa zoezi lililokuwa linafuata ni kupitisha kanuni hizo kifungu kwa kifungu. Wa kwanza kuzungumza alikuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye aliwaomba na kuwasihi wajumbe kuacha lugha za kejeli, kujali maslahi ya taifa mbele na kushikamana kutekeleza jukumu lililo mbele yao. Aidha, alitoa rai kwa Mwenyekiti kuwa vile vifungu ambavyo vitaonekana kuwa na ugumu katika kuvipitisha, watu wanaoheshimika na wenye weledi kwenye jambo hilo wateuliwe ili kupata muuafaka wa pamoja. Hoja hiyo iliungwa mkono na watu wengine waliopewa nafasi ya kuzungumza akiwemo Freeman Mbowe, Vuai Ali Vuai na Ibrahimu Lipumba.

Baada ya watu hao kuzungumza, ndipo zoezi la kupitisha kanuni lilipoanza kwa kupitia kifungu kwa kifungu na wale wabunge wenye marekebisho ambao majina yao yaliwasilishwa kwenye kamati walipewa nafasi ya kuwasilisha marekebisho yao.

HOJA YA WENGI NA WACHACHE
Kwenye Rasimu ya Pili ya Kanuni, imeelezwa kuwa kutakuwa na kamati 12 ambazo zitapewa vifungu vya kujadili Rasimu ya Pili ya Katiba. kwamba kila kamati itajadili na kuandaa taarifa yake. Baada ya zoezi hilo, kamati tatu (kama sijakosea) zitakutana kwa muda wa siku mbili kukusanya mawazo ya kamati hizo na kuandaa taarifa moja. Taarifa hiyo itaeleza msimamo wa walio wengi na walio wachache na kuyawasilisha mbele ya Bunge Maalum. Katika hili ndipo hoja ilipoibuka. Beatrice SHELUKINDO ambaye alionekana kuungwa mkono na wabune wengi bila ya kujali makundi yao alisema kuwa utaratibu huo urekebishe. Badala ya kamati tatu kukutana, kila kamati iwasilishe taarifa yake bungeni kwa saa moja ikiwa na maoni au msimamo wa wachache na walio wengi. Pia wale wachache wapewe nafasi ya kutoa maoni juu ya hoja za ndani ya Bunge. Hoja yake kwa kweli iliungwa mkono na wabunge wengi na wala haikuonekana kama ingekuwa na utata. Utata ulikuja baada ya Tundu Lisu ambaye pia ni miongoni mwa wanaounda kamati hiyo kusema kuwa haiwezekani na hatakuwa tayari kuona walio wachache wanasemewa na walio wengi. Yeye alitaka kuwa kuwe na taarifa mbili, Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ambayo itaeleza maoni ya walio wengi na Taarifa ya walio wachache. Hata hivyo katika majadiliano, ikaonekana kuwa hoja ya Lisu haikuwa na msingi. Kwamba, kwa kuwa Mwenyekiti wa Kila kamati atawakilisha makundi yote yaani ya walio wengi na wachache, hakuna mantiki ya kuandaa tena taarifa ya wachache. Badala yake, wale wachache watapewa nafasi kwenye Bunge kufafanua hoja zao. Hata hivyo kutokana na ufinyu wa muda, hoja hiyo ilikuwa haijapatiwa ufumbuzi na kikao cha leo ambacho kitaanza saa NNE ASUBUHI kitalipatia ufumbuzi.

Wana JF, kuna watu wana mitambo ya kupika uongo na wametumia vizuri fursa ya kukosekana kwa JF kwa siku mbili kuiga mambo yanayofanyika kule kwingine. nawasihi sana kuwa watulivu na kushirikisha akili zetu vizuri.

Nawasilisha.
 
Mkuu, lazima uwachukie CCM kutokana na chama chenu CHADEMA kuendelea kusambaratika. soon utahamia ACT

hujitambui wewe,hivi chama kinasambaratishwa kwa uharo wenu mitandaoni!!!
njoo field uuone moto wa cdm!!!
Hakunaga kama cdm tz! tunakiunga mkono na pamoja tutashinda hila za magamba na vibaraka vyao!!!
 
Katika swala hili, ni issue moja tu tuna problem nayo...MOJA tu !. Nayo ni kwamba hatukubali kabisa, wale walio wengi ambao hawajakubaliana na mawazo ya walio wachache, hao hao ndio wawe wasemaji wa walio wachache !.

Mbona ni hoja nyepesi na rahisi tu kueleweka ? Hivi wewe utakubali yule asiyekubaliana na wewe ndio awe msemaji wa kutetea kitu kile kile asichokikubali !? Kama wewe unalikubali hilo sisi hatulikubali !. Kama Tundu Lissu alivyosema, haiwezekani na mimi nakubaliana naye, HAIWEZEKANI KABISA !

Narudia tena, yote mnaweza kufanya kwa sababu mpo wengi na kwenye kura mtashinda....Lakini pale mnapotaka nyie hao hao ndio muwe midomo yetu wakati wa kuwapinga na kupunguza uwezo wetu wa kutetea hoja zetu, hilo hatutakubali kwa namna yeyote ile !

Besides, wakati Tundu Lissu anasema haiwezekani, hakuna msemaji yeyote aliyesema chochote isipokuwa mwanasheria wa Zanzibar ambaye pia naye ni mwanakamati na yeye ofcourse alisema maamuzi ya kamati, ambayo ni kwamba walio wachache watajisemea wenyewe ingawa maoni yao yatajumuishwa kwenye taarifa kuu. Kwa hiyo unaposema baada ya Lissu kusema hivyo alionekana hana hoja kwenye mjadala unakuwa hausemi kweli kwa sababu HAKUKUWA na mjadala wowote baada ya Lissu kusema hayo maneno !

 
umesema kweli kabisa wazee wa ''chopa 3 kata 3''!

hujitambui wewe,hivi chama kinasambaratishwa kwa uharo wenu mitandaoni!!!
njoo field uuone moto wa cdm!!!
Hakunaga kama cdm tz! tunakiunga mkono na pamoja tutashinda hila za magamba na vibaraka vyao!!!
 
Hahahahaa chama mie ya babu simo...hasira zangu ziko kwa hawa wasio na aibu

Usikatae ukweli babu ndiye mliyemkabidhi panga la ukombozi kumbe kaliweka rehani kwa tamaa zake; basi ungekuwa na hasira na babu maana hana aibu wala soni hana!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…