Wakuu,
Fact moja katika bunge hili la katiba ni kwamba CCM wana uwakilishi mkubwa kupita makundi yote ukiyaweka kwa pamoja !. Kutokana na huu ukweli, ni wazi kwamba CCM watakuwa wengi katika kila kamati itakayoundwa na inawezekana kabisa wenyeviti wengi wa kamati (kama sio wote) wakatoka CCM !
Kwa kuzingatia ukweli huu, wajumbe wa Bunge la katiba ambao ni wana CCM wanapoongelea kundi la walio wachache wanajua kabisa katika kamati zote wao hawatakuwa katika hili group la wachache...na kwa sababu wako wengi wanaweza wakapitisha hoja zao kwa urahisi tu, ambazo watazitetea wenyewe kwa sababu wenyeviti watakaoziwakilisha mostly nao watakuwa wana CCM...Kwa hiyo CCM mkitaka mnaweza kutengeneza katiba yenu halafu mkaiita ya waTz. Baadhi yetu tunaamini mtafanya hivyo, na tumeshaandaa kura zetu za HAPANA tayari tayari, kwa sababu hatutakubali katiba mpya feki ! Heri tujue hatuna katiba ili tuendelee kuidai kuliko kuwa na katiba feki....
Tukiacha hilo la katiba mtakayoitoa kama itazingatia maoni ya wananchi au la, ninachotaka kuzungumzia hapa ni hii issue ambayo na nyie CCM mmekuwa mnaizungumzia mara kwa mara...issue ya amani, maridhiano, kuheshimiana na blah blah nyingine zinazofanana na hizo. Wakati mwenyekiti wenu wa Taifa, analiongelea hili, wengi tulimchukulia serious ingawa wengi wetu hatumwamini (ingawa ni Rais wetu) kwa sababu yeye kama mlivyo wana CCM wengi ni watu wa maneno tu na unafiki kwa kiwango kikubwa.
Na kuthibitisha wasiwasi wetu kwake ni pale matendo mlioanza kuyafanya CCM (under his watch) baada ya hiyo kauli yake. Matendo yenu yamekuwa completely contrary na lugha ya maridhiano, kutunza amani, kusikiliza wachache etc....Pinda naye jana bungeni, kama kawaida yake aliongea kidizaini hizo hizo, lakini kilichofuata Bungeni baada ya yeye kuongea ni kwa vijana wake kwenda kinyume kabisa na hiyo spirit ya wengi wape, wachache wasikilize.......
Ninachotaka kuwaambia CCM ni kwamba kila mtu ana redline yake...na ukivuka hiyo whether unataka au hutaki utatafuta kutokuelewana/shari, hata kama wewe ndio mwenye serikali....Just imagine, nyie mko wengi, mnaamua mnachotaka, mnapata nafasi kupitia wenyeviti wenu kutetea hizo hoja zenu.....halafu eti mnataka kulazimisha nyie HAO HAO ndio muwe midomo ya wale wachache ! Are you really serious !? Hivi mnafikiri nani atalikubali hilo ? Yaani wewe hukubaliani na mimi, halafu unalazimisha utetee hoja yangu! Tena kwa kunilazimisha ! Ndio maana Bungeni jana Lissu aling'aka na kusema hilo haliwekani....
Nyerere alisema kwamba....mtu mzima akikwambia jambo la kipumbavu ambalo anajua ni la kipumbavu na anajua wewe unajua ni la kipumbavu halafu ukalikubali anakudharau !. Sasa nyie mnafikiri nani atakubali jambo hili la kipumbavu ambalo mnataka kulilazimisha !
In summary ninawaomba muwe reosanable. Kuna vitu vingi mnaweza kufanya kwa wingi wenu...ingawa tutavipinga...bado mnaweza kuvipitisha, ila mnapofikia hatua ya kulazimisha NYIE HAO HAO muwe sauti yetu wakati wa-kuwapinga nyie, hapo mnavuka mipaka (redline) na kwa VYOVYOTE vile, hakuwezi kuwa na maelewano.....
Please, be reasonable !
UPDATE :
Ninashukuru busara zimetumika na muafaka umepatikana katika hili. Muafaka ni kwamba Mwenyekiti atapresent hoja zote (za wengi na wachache) halafu wale wachache watamchagua mmoja wao na yeye atafafanua hoja zao kwa muda wa nusu saa. Huku ndio kuwa reasonable na ninampongeza sana Mheshimiwa Kificho kwani najua ana mchango mkubwa katika busara hili....