Pre GE2025 CCM hii imeenda, message sent

Pre GE2025 CCM hii imeenda, message sent

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nape akiwa Waziri na akiwa amevaa kichwani kofia ya CCM amesema anataka kumfundisha Byabatto namna ya kushinda uchaguzi hatakama hapendi na wananchi wake. Amezitaja mbinu anazozifahamu na kuzitumia kupata ushindi wakati wa uchaguzi. Mbinu hizi amezitumia kwake jimbo la Mtama akaona zinafanyakazi kwa 100% kutoa matokeo chanya. Sasa hatujui kama mbinu hizi ni zake tu au ni za chama chake.

Nape alisema kitu anachokijua kinavyofanyika na anachofanyafanya yeye mwenyewe na amekuwa akikisema mara kwa mara hata huko nyuma wakati aliposema ushindi wa bao la mkono. NI mtu ambae ameshika nafasi ya mwenezi wa CCM taifa ni mtu anayefahamu habari za ndaaaani kabisa ndani ya CCM.

Hakusema utani hata kidogo bali alisema kilichopo, hivyo hakuna namna yoyote ya kuweza kurudisha mdomoni kile alichokisema hata kama atatumbuliwa ama kukanushwa na CCM. Ametuhakikishia kile wapinzani walichokuwa na wasiwasi nacho kwa miaka mingi kuhusu uchaguzi. Dunia imeelewa na kupata za ndaaaaani kabisa kupitia mtu wa ndaaaaani kabisa wa CCM na serikali kuwa uchaguzi unaibwa, no doubt about it any more.

Kwa mtaji huu, nami naunga mkono hoja ya Tume huru kabisa ya Uchaguzi na matokeo kuhojiwa mahakamani.

Pia soma
- Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza, ili mradi ukimaliza unasema Mungu nisamehe!

Kauli ya Chama ~ CCM yakataa maneno aliyosema Nape kuhusu ushindi wa kura unategemea na anayehesabu kura

Pia, utetezi wake: Kuelekea 2025 - Nape Nnauye: Kauli ya "Matokeo ya kura inategemea nani anahesabu na nani anatangaza" ilikuwa ni ya utani
 
Back
Top Bottom