CCM ichague moja: Kuendelea na kesi ya Lissu au kuingia kwenye maridhiano

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Wasira.png
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira, hivi karibuni amesikika akisema kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ndiye anayechangia kucheleweshwa kwa kesi yake ya uhaini kwa kuwasilisha mapingamizi mara kwa mara.

Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV Julai 20, 2026, Wasira pia alizungumzia suala la maridhiano. Alisema kuwa iwapo CHADEMA itaweka masharti magumu, CCM itayapima ili kuona kama yana mantiki; yasipokuwa na msingi, haitayakubali. Aidha, alipinga pendekezo la kuhusisha msuluhishi kutoka nje ya nchi, akidai hatua hiyo haitaleta suluhisho linalotarajiwa.

Katika mahojiano yake na DW Kiswahili, Wasira alipinga pia wito wa kuachiliwa kwa Lissu. Alisisitiza kuwa Tanzania ina mihimili mitatu ya dola—Mahakama, Bunge na Serikali—na kwamba kwa kuwa kesi ya Lissu iko mahakamani, hakuna mamlaka inayopaswa kuingilia mchakato wa kimahakama.

Hata hivyo, ukifuatilia kauli hizi kwa karibu, zinazua maswali kuhusu msimamo wa CCM. Kwa upande mmoja, chama kinasema hakiwezi kuingilia Mahakama, lakini kwa upande mwingine, Serikali ndiyo iliyoanzisha mashtaka dhidi ya Lissu. Chini ya sheria za Tanzania, Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali (DPP), kwa mamlaka yanayotolewa na Rais, anaweza kuondoa mashitaka kupitia utaratibu wa nolle prosequi.

Hili si jambo jipya. Mfano wa karibu ni kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ambayo ilifutwa kabla ya kufikia hukumu. Ikiwa hilo liliwezekana kwa Mbowe, kwa nini hoja hiyo ionekane haiwezekani katika kesi ya Lissu? Kauli kwamba "Mahakama haiingiliwi" inahitaji kutazamwa katika muktadha mpana wa mamlaka ya Serikali katika kuanzisha au kuondoa mashitaka ya jinai.

Pia ni muhimu kutambua kwamba wanaotoa wito wa kuachiliwa kwa Lissu hawafanyi hivyo kwa misingi ya huruma pekee. Wengi wanaona suala hilo kama sehemu ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa uliojitokeza baada ya matukio ya uchaguzi wa mwaka 2025. Ni vigumu kuzungumzia maridhiano ya kweli wakati kiongozi wa chama kikuu cha upinzani bado yuko mahabusu akikabiliwa na kesi ya uhaini.

Kuhusu madai kwamba Lissu ndiye anayochelewesha kesi yake, rekodi ya mwenendo wa kesi inaibua taswira tofauti. Kumekuwa na madai kutoka kwa upande wa utetezi kwamba Lissu alishawishiwa kukubali makosa ambayo amekuwa akiyakana ili aweze kuachiliwa, madai ambayo yeye mwenyewe ameyakana hadharani.

1784709848417.png

Aidha, hadi Oktoba 2025, upande wa Jamhuri ulikumbana na changamoto ya kuingiza baadhi ya ushahidi wake mahakamani baada ya ushahidi muhimu kukataliwa. Kesi ikaahirishwa hadi Novemba 13, 2025, na baadaye Februari 2026, huku upande wa mashtaka ukiendelea kujaribu kuingiza shahidi mwingine bila mafanikio.

Hatimaye, Jamhuri ndiyo iliyokwenda Mahakama ya Rufani kuomba mapitio ya maamuzi hayo. Rufaa hiyo ilichukua takribani miezi minne kabla ya kusikilizwa Julai 3, 2026, na hadi sasa bado haijulikani uamuzi wake utatolewa lini.

Kwa msingi huo, si sahihi kueleza kwamba Lissu ndiye amekuwa akikata rufaa mara kwa mara. Kwa mujibu wa mwenendo wa kesi ulioonekana hadharani, ni upande wa Jamhuri uliowasilisha rufaa kuhusu maamuzi ya mahakama. Hali hii pia imeibua mjadala kuhusu kasi ya utoaji wa haki katika kesi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa inamhusu mshtakiwa mmoja.

Wasira pia amesema CCM haitafuti maridhiano na CHADEMA pekee, bali na Watanzania wote. Kauli hiyo ina mantiki. Hata hivyo, swali linalobaki ni kwa nini mchakato huo unasuasua ikiwa ni CCM yenyewe iliyouahidi umma.

Kwa muda mrefu kumekuwa na ahadi za kuunda tume, kufanya mashauriano na kuanzisha michakato mbalimbali ya maridhiano, lakini hatua za utekelezaji zimekuwa zikionekana kwenda taratibu. Hali hiyo imewafanya baadhi ya wadau kuhoji kama kweli kuna dhamira ya kisiasa ya kufikia maridhiano ya maana.

Ndiyo maana CCM inapaswa kufanya uamuzi wa wazi kuhusu mwelekeo wake.

Iwapo inalenga maridhiano ya kisiasa, italazimika kukubali kwamba maridhiano yanahitaji kila upande kufanya maamuzi magumu. Hilo linaweza kujumuisha kutafuta suluhu ya kesi ya Lissu na kushughulikia kwa uwazi masuala ya uwajibikaji kuhusu matukio yaliyoambatana na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.

Lakini kama CCM haiwezi kukubaliana na masharti yanayotolewa na CHADEMA, basi inaweza kuendelea na mazungumzo na wadau wengine wa kisiasa au kuamua kuachana kabisa na ajenda ya maridhiano.

Haiwezekani kuendelea kutuma ujumbe unaoonekana kuvutana pande mbili kwa wakati mmoja. Taifa linahitaji msimamo ulio wazi.

Kwa hiyo, CCM inapaswa kuchagua njia moja kati ya mbili: ama iendelee na mchakato wa maridhiano kwa kuchukua hatua zinazoweza kujenga imani kwa pande zote, au iamue kuendelea na kesi ya Lissu hadi mwisho wake kwa kuiacha Mahakama iamue.

Kujaribu kufanya yote mawili kwa wakati mmoja kunaendelea kuacha maswali mengi kuliko majibu kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa nchi.
 
​
CCM has nothing to do with kesi ya Lissu ni serikali.
Tusiichanganye CCM na serikali
Mchanganyiko huu unakuja kwasababu Mwenyekiti wa CCM ndie mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu
P​
 
We..mse@z&..fuc^ ... haaaa sorry 😞nilitaka nikutukane sikujua kuwa tayari una BLUE TIKI...Ninge kutusi bure...nawapongeza JF kwa kutoa hizi BLUE TIKI vinginevyo tungekuwa tunatusi watu tukizani ni wazima vichwani ....😁😁😁
 
Hii inaonyesha viongozi wengi hasa WA chichiemu hawako Kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi Bali maslahi Yao.

Kuhusu Kesi ya Lissu na sasa ya Muhadhiri wa UDOM, ni wazi hizi Kesi sio za uhaini kama zinavyotaka kuwekwa, Bali za kisiasa, na Nia ya kulazimisha upande wenye Haki kumpigia magoti upande usio na Haki.
 
4. MASHARTI NA MUDA MAALUMU KUTOKA COMMONWEALTH CMG(The Ultimatum)

Kutokana na mapendekezo ya Mjumbe Maalum, CMAG imetoa maelekezo yenye ukomo wa muda (Time-bound actions) kwa Tanzania:

Ndani ya Siku 30: Kutatua suala la kushikiliwa kwa Tundu Lissu kupitia njia za kisiasa au kisheria, na kuwaachia wengine wote wanaoshikiliwa kwa kutumia haki zao kwa amani.

Ndani ya Siku 60: Kurejesha upatikanaji kamili wa mitandao ya kijamii na kuacha vitisho dhidi ya vyombo vya habari na watetezi wa uhuru wa kujieleza.

Ndani ya Siku 90: Kuitisha jukwaa shirikishi na la kuaminika la vyama vya siasa (likiongozwa na mwezeshaji huru) kujadili mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, ushindani wa kisiasa, wafungwa, na uwajibikaji.

Bila Kuchelewa: Kuanza uchunguzi huru wa makosa ya jinai uliopendekezwa na Tume ya Uchunguzi, pamoja na fidia kwa wahanga.

MWISHO WA UBAYA NI AIBU.h
 
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Stephen Wasira, hivi karibuni amesikika akisema kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ndiye anayechangia kucheleweshwa kwa kesi yake ya uhaini kwa kuwasilisha mapingamizi mara kwa mara.

Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV Julai 20, 2026, Wasira pia alizungumzia suala la maridhiano. Alisema kuwa iwapo CHADEMA itaweka masharti magumu, CCM itayapima ili kuona kama yana mantiki; yasipokuwa na msingi, haitayakubali. Aidha, alipinga pendekezo la kuhusisha msuluhishi kutoka nje ya nchi, akidai hatua hiyo haitaleta suluhisho linalotarajiwa.

Katika mahojiano yake na DW Kiswahili, Wasira alipinga pia wito wa kuachiliwa kwa Lissu. Alisisitiza kuwa Tanzania ina mihimili mitatu ya dola—Mahakama, Bunge na Serikali—na kwamba kwa kuwa kesi ya Lissu iko mahakamani, hakuna mamlaka inayopaswa kuingilia mchakato wa kimahakama.

Hata hivyo, ukifuatilia kauli hizi kwa karibu, zinazua maswali kuhusu msimamo wa CCM. Kwa upande mmoja, chama kinasema hakiwezi kuingilia Mahakama, lakini kwa upande mwingine, Serikali ndiyo iliyoanzisha mashtaka dhidi ya Lissu. Chini ya sheria za Tanzania, Mkurugenzi wa Mashitaka wa Serikali (DPP), kwa mamlaka yanayotolewa na Rais, anaweza kuondoa mashitaka kupitia utaratibu wa nolle prosequi.

Hili si jambo jipya. Mfano wa karibu ni kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ambayo ilifutwa kabla ya kufikia hukumu. Ikiwa hilo liliwezekana kwa Mbowe, kwa nini hoja hiyo ionekane haiwezekani katika kesi ya Lissu? Kauli kwamba "Mahakama haiingiliwi" inahitaji kutazamwa katika muktadha mpana wa mamlaka ya Serikali katika kuanzisha au kuondoa mashitaka ya jinai.

Pia ni muhimu kutambua kwamba wanaotoa wito wa kuachiliwa kwa Lissu hawafanyi hivyo kwa misingi ya huruma pekee. Wengi wanaona suala hilo kama sehemu ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa uliojitokeza baada ya matukio ya uchaguzi wa mwaka 2025. Ni vigumu kuzungumzia maridhiano ya kweli wakati kiongozi wa chama kikuu cha upinzani bado yuko mahabusu akikabiliwa na kesi ya uhaini.

Kuhusu madai kwamba Lissu ndiye anayochelewesha kesi yake, rekodi ya mwenendo wa kesi inaibua taswira tofauti. Kumekuwa na madai kutoka kwa upande wa utetezi kwamba Lissu alishawishiwa kukubali makosa ambayo amekuwa akiyakana ili aweze kuachiliwa, madai ambayo yeye mwenyewe ameyakana hadharani.

Aidha, hadi Oktoba 2025, upande wa Jamhuri ulikumbana na changamoto ya kuingiza baadhi ya ushahidi wake mahakamani baada ya ushahidi muhimu kukataliwa. Kesi ikaahirishwa hadi Novemba 13, 2025, na baadaye Februari 2026, huku upande wa mashtaka ukiendelea kujaribu kuingiza shahidi mwingine bila mafanikio.

Hatimaye, Jamhuri ndiyo iliyokwenda Mahakama ya Rufani kuomba mapitio ya maamuzi hayo. Rufaa hiyo ilichukua takribani miezi minne kabla ya kusikilizwa Julai 3, 2026, na hadi sasa bado haijulikani uamuzi wake utatolewa lini.

Kwa msingi huo, si sahihi kueleza kwamba Lissu ndiye amekuwa akikata rufaa mara kwa mara. Kwa mujibu wa mwenendo wa kesi ulioonekana hadharani, ni upande wa Jamhuri uliowasilisha rufaa kuhusu maamuzi ya mahakama. Hali hii pia imeibua mjadala kuhusu kasi ya utoaji wa haki katika kesi hiyo, hasa ikizingatiwa kuwa inamhusu mshtakiwa mmoja.

Wasira pia amesema CCM haitafuti maridhiano na CHADEMA pekee, bali na Watanzania wote. Kauli hiyo ina mantiki. Hata hivyo, swali linalobaki ni kwa nini mchakato huo unasuasua ikiwa ni CCM yenyewe iliyouahidi umma.

Kwa muda mrefu kumekuwa na ahadi za kuunda tume, kufanya mashauriano na kuanzisha michakato mbalimbali ya maridhiano, lakini hatua za utekelezaji zimekuwa zikionekana kwenda taratibu. Hali hiyo imewafanya baadhi ya wadau kuhoji kama kweli kuna dhamira ya kisiasa ya kufikia maridhiano ya maana.

Ndiyo maana CCM inapaswa kufanya uamuzi wa wazi kuhusu mwelekeo wake.

Iwapo inalenga maridhiano ya kisiasa, italazimika kukubali kwamba maridhiano yanahitaji kila upande kufanya maamuzi magumu. Hilo linaweza kujumuisha kutafuta suluhu ya kesi ya Lissu na kushughulikia kwa uwazi masuala ya uwajibikaji kuhusu matukio yaliyoambatana na uchaguzi wa Oktoba 29, 2025.

Lakini kama CCM haiwezi kukubaliana na masharti yanayotolewa na CHADEMA, basi inaweza kuendelea na mazungumzo na wadau wengine wa kisiasa au kuamua kuachana kabisa na ajenda ya maridhiano.

Haiwezekani kuendelea kutuma ujumbe unaoonekana kuvutana pande mbili kwa wakati mmoja. Taifa linahitaji msimamo ulio wazi.

Kwa hiyo, CCM inapaswa kuchagua njia moja kati ya mbili: ama iendelee na mchakato wa maridhiano kwa kuchukua hatua zinazoweza kujenga imani kwa pande zote, au iamue kuendelea na kesi ya Lissu hadi mwisho wake kwa kuiacha Mahakama iamue.

Kujaribu kufanya yote mawili kwa wakati mmoja kunaendelea kuacha maswali mengi kuliko majibu kuhusu mwelekeo wa kisiasa wa nchi.
Umeongea vizuri mkuu,hii inafikilisha, Naona Kama serikali na chama tawala Hawana Nia ya dhati ya Maridhiano, Mfano mzuri ni makaburu wa afrika ya kusini, Mandela akiwa kifungoni , alitolewa kwanza, Maridhiano yakafanyika,waliokufa wanatakiwa kuwajibishwa,waliwajibishwa akiwemo mkuu wa kutesa Eugene kock!Na uchaguzi ukafanyika,Nchi imesonga Hadi Sasa!Tukiamua,Tunaweza.
 
CCM has nothing to do with kesi ya Lissu ni serikali.
Tusiichanganye CCM na serikali
Mchanganyiko huu unakuja kwasababu Mwenyekiti wa CCM ndie mkuu wa nchi, mkuu wa serikali na amiri jeshi mkuu
P​
Hebu fafanua,Mbowe alishtakiwa Kwa kosa hilihili, CCM ikiwa madarakani!Ni Vipi tofauti hapo Kwa TAL?
 
Back
Top Bottom