CCM ijiandae kisaikolojia, mwaka huu lolote linaweza kutokea

CCM ijiandae kisaikolojia, mwaka huu lolote linaweza kutokea

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Najua CCM imejiandaa kushinda kwa mbinu yeyote ile, Jecha style, NEC style, wizi n.k. ila wajue Wapinzani wao nao wamejiandaa kutoshindwa kirahisi kwa mbinu zozote zile, iwe hacking, kuingia barabarani, kuwatumia mabeberu n.k.

Kitu cha msingi CCM wajue kuwa wapiga kura ni binadamu siyo madaraja wala roboti kuwa utaziwekea program zikuchague, unaweza kuwaona wako upande wako kimwili kumbe kiroho hawako nawe. Mfano wa karibu ni wajumbe wa CCM wakati wa kura za maoni, kabla ya kura kila mjumbe alikuwa akisema 'TUKO PAMOJA MHESHIMIWA'.👍 na dole gumba juu, lakini waliwashangaza wengi.

So CCM wajiandae kwa yote kushinda na kushindwa, hawatakuwa wa kwanza kwa chama kilichopigania Uhuru kuwa chama cha upinzani, wajifunze yaliyotokea kwa KANU, ZANU-PF n.k. wataishi kwa amani vinginevyo kuna wengi watakufa kwa presha itakapofika Novemba mwaka huu.
 
Kwa kweli hii nchi ni yetu sote, wasitupangie na kutufokea.
 
Back
Top Bottom