CCM ni baba wa vyama vyote vya siasa Tanzania. Vyama vyote vinaitazama CCM kama kioo chao. Iwe kwenye jema au baya. Mara nyingi huko CHADEMA kukitokea mambo ya kipuuzi hukimbilia kujitetea kuwa CCM wanafanya mabaya zaidi. Kwa mfano ukiuliza kuhusu michango na ruzuku utajibiwa kwa kuambiwa kaulize CCM kuhusu ufisadi.
Kwa sasa ndani ya CHADEMA kuna sakata la rushwa kwenye chaguzi zao ila makada waandamizi wamekimbilia kuitaja CCM inahusika.
Ninakisihi Chama Cha Mapinduzi kusimamia vizuri ilani yake na kuwachukulia hatua makada wake wanaofanya mambo ya hovyo. Hii itasaidia vyama vidogo kama CHADEMA kuiga mema badala ya mabaya.