Wilderness Voice
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 921
- 1,649
Nasikitika sana, na ninakishangaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kujiona kuwa kina hati miliki ya nchi na wananchi. Eti CCM kinasema hakina mpango na Katiba mpya. Ambayo hata walio asisi hii nchi, akiwepo Mwalimu Nyerere alikiri kuwa hii Katiba siyo nzuri kwani inampa Rais Madaraka makubwa kiasi kwamba Rais anaweza tumia huo mwanya kufanya atakacho.
Nimshukuru Rais mstaafu Kikwete, kuanzisha mchakato na baadae akauuwa yeye mwenyewe, kwa kuiponda tume na maazimio yaliyofikiwa na hivyo kutupilia mbali mchakato huo wa katiba, lakini alithubutu.
Najua kilichofanya asitishe mchakato huo wa Katiba ni maswala yaliyojitokeza ya Muungano na hasa Serikali tatu. Kwani Rais anaapa kuulinda Muungano wa Tanzania. Hivyo angeruhusu hilo jambo kutokea, ilikuwa ajiuzuru na hivyo kuruhusu serikali ya mpito kuchukua nafasi, kitu ambacho nadhani kingeenda KINYUME na miiko ya CCM. Tunakumbuka yalomfika Abdul Jumbe Mwinyi. Hata hivyo nampa kongole Mhe. J. Kikwete kwa uthubutu huo.
Serikali inayojiita awamu ya sita, japo si awamu ya sita kulingana na katiba tuliyonayo. Hakuna uchaguzi uliyoitishwa, bali Rais aliyopo anaendeleza awamu ya tano mpaka itapofikia ukingoni mwaka 2025. Rais ni wa Sita awamu ya tano. Hivyo tusilazimishwe. Lakini Watanzania uamlishwa kama kuku, ingia ndani tunaingia. Tumejaa ushabiki na undumila kuwili. Mtu akipinga asubiri matusi na kejeri ili tu kumvunja moyo. oK, Tuache hayo!
Tayari Rais wetu Mama Samia, kupitia Katibu mwenezi wa CCM, alieleza serikali ya CCM haina mpango kuruhusu mchakato wa Katiba Mpya. Nacho jiuliza, hivi CCM wana mamlaka gani kikatiba, kukataa kusiwepo mabadiliko ya Katiba? Je, ni kwakua Rais ni wa CCM?
Je kwa style hii ya CCM hata ikitawala miaka 100 ijayo hatutapata katiba mpya kisa CCM na Rais ndo waamuzi? Tena CCM inaongea kwa kujisikia na kutamba kwamba hakuna Katiba mpya! Ni nani kaiweka CCM madarakani? Si wananchi? Ni kwanini leo hawa CCM wanawadharau wananchi kwa kusema hakuna katiba Mpya!
Watanzania, tufikie sehemu, tuihadhibu CCM, si kujipendekeza! Ili kuleta mabadiliko sahihi na kuondokana na mazoea! Hii katiba iliyopo itatuchelewesha kupata maendeleo. Kuna mifumo mingi ambayo inahitajika kufanyiwa marekebisho, ili kuifanya Tanzania ibadilike na iendelee. Nchi nyingi duniani ufanya mabadiliko ya kimfumo ambayo uwa katika katiba kwa maslahi mapana ya nchi. Kwanini CCM ijione ndiyo yenye dhamana katika hili?
Hata Rais Kikwete hakuwa na mamlaka ya kusitisha mambo ambayo tayari yalikuwa yamepitishwa na Bunge la Katiba. Rais kwa utashi wake akagoma na kutoa vijembe kwenye Tume kuwa mara katiba ni jitabu kubwa utadhani desa la physics. Ni kweli katiba haikuhitaji kuwa kubwa kama kitabu cha hadithi za Alf lela Ulela! Lakini tulichokihitaji ni mfumo mpya wa katiba. Angewapa muda kufanya usahihi na kisha kwendelea na mchakato kuliko kusitisha kila kitu.
Imefikia wakati sasa, uchaguzi wa 2025 usifanyike kama hatuna katiba mpya. Mikakati ifuatayo ifanyike:
Safari hii kieleweke. CCM si Mungu wa kutuamlia tutakacho. Shida tumekuwa na wanasiasa wanafiki, ambao hawana uzalendo wao uangalia matumbo yao na familia zao. Ebu tubadilike na tuchukue hatua sasa.
Nimemkumbuka Mch. Mtikila! Kheri yake aliweza kubadili mambo kwa kuishitaki serikali mahakamani, na hata kuhamasisha wananchi. Hata Mstaafu Rais Mwinyi hawezi msahau huyu!
SHIME WATANZANIA TUDAI KATIBA MPYA. WAKATI NI SASA! TUSIPO DAI TUSAHAU!

- Kwenda mahakamani kudai mwendelezo na mchakato wa katiba Mpya wendelee, kwani Rais aliuzuia kimakosa.
- Viongozi wote wa vyama vya siasa, vyama vya wafanyakazi, NGOs, Asasi mbalimbali za haki za binadamu, Viongozi wa dini lugha iwe moja Katiba Mpya.
- Maandamano ni haki na msingi wa kudai utendaji haki. Kila mwezi kuwe na siku moja ya maandamano ya amani nchi nzima kudai katiba mpya.
- Kuwepo kampeni ya kuwasusia viongozi wa Serikali katika mikutano yao, kwani ni wao ndo hawataki uwepo wa katiba mpya. Hata Rais hasusiwe.
- Tuwatake wabunge wetu wahoji kuhusu katiba mpya Bungeni, kama hawataki, nao tusiwatambue!