Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naunga mkono, kiongozi huyu sasa ni Samia. Suala la Katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM iliyopita, kwa vile lilikuwepo na JPM akasema sio kipaumbele chake na hatukumshinikiza, na kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya sasa halipo, then tusimshinikize Samia, ni rais mwenye maono, msikivu, ana jicho japo linaonekana limeregea, lakini linaona sana!.Tunahitaji kiongozi mwenye maono, anae waza zaidi nje ya box
Well saidWala siyo muungano ndugu. Sababu ni kwamba katiba mpya inapunguza sana mamlaka ya rais. Lkn pia inaiweka CCM ishindwe namna ya kutumia vyombo vya dola kubakia madarakani.
Ma-Askofu wakianza kudai katiba mpya sasahivi inapatikanaNaunga mkono, kiongozi huyu sasa ni Samia. Suala la Katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM iliyopita, kwa vile lilikuwepo na JPM akasema sio kipaumbele chake na hatukumshinikiza, na kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya sasa halipo, then tusimshinikize Samia, ni rais mwenye maono, msikivu, ana jicho japo linaonekana limeregea, lakini linaona sana!.
Angalia sifa nyingine za samia
PSiku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
Wanabodi, Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha mahojiano ya Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzia Siku ya Wanawake Duniani kwenye TBC akihojiwa na Shabani Kissu. Kwa Waliosikiliza kipindi hiki, kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya...www.jamiiforums.com
Da! umepiga nyundo sn mkuuRais anaongoza kweli kwa Katiba, sheria, taratibu na kanuni mbalimbali ambazo zipo kwa manufaa ya nchi. Japo pia anatekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama chake.
Ukitegemea tu Civics ni ngumu kuelewa mfumo mzima wa utendaji wa kazi za Rais. Kikubwa ni kujiongeza na kujua mbali na yote, nchi uhitaji visionary leader. Rais alie na maono. Anae weza kufikiria nje ya Box na si akili kuishia tu kwenye kile alichopangiwa kufanya. Ukiwa na Rais wa namna hiyo ambae anaangalia tu Ilani, bila kutazama nyakati na mabadiliko ya kimfumo na kidunia basi huyo Rais si mbunifu.
Tunahitaji Rais ambae anaangalia Ilani yake ya Uchaguzi lakini pia anaangalia mahitaji ya kitaifa na kujenga Taifa lisilo na mawaa.
Ndo maana kuna mihimili mingine ambayo ipo kukidhi haja ya kujenga Taifa moja.
Na hii mihimili mingine haina Ilani bali inatekeleza majukumu kwa kuzingatia sheria na taratibu mbalimbali.
Mfano, Ilani ya CCM haijawai kukubali mgombea binafsi katika uchaguzi wa Tanzania. Lakini katika miaka ya nyuma elfu mbili na kitu, Mahakam Kuu ilitoa maamuzi ya kuwepo mgombea binafsi au wagombea binafsi katika chaguzi. Japo mahakama ya Rufaa ilibatirisha maamuzi hayo kimizengwe.
Hivyo Mahakama, Bunge zinauwezo wa kuelekeza au kutoa maamuzi ya kufanyika kwa jambo japo hilo jambo haliko katika Ilani ya uchaguzi wa CCM. Ndo maana nikasema kwa kutumia hii mifumo tunaweza kupata katiba mpya kwani Rais hatohitaji kukwepa.
Kikwete alivyoanzisha mchakato wa katiba mpya, haikuwa katika Ilani ya uchaguzi. Ila ni kiongozi alie angalia nje ya Box na kuona kuna hitaji hilo kwa wakati huo.
Ni mangapi marais wanafanya na hayako katika Ilani ya uchaguzi? Tusitafute visingizio visio na mantiki. Mabadiliko ya Haki za binadamu yalianza kuwekwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1984, na baadae iliendelea . haya mabadiliko ya kwanza wakati yanafanyika, hayakuwa kwenye Ilani. Ila kutokana na muda na mahitaji katika jamii ilifanyika. Utakumbuka Rais alikuwa na mamlaka ya kumuweka mtu kuzuizini. CCM hawakupenda lakini ilibidi watii.
Mfumo wa Vyama vingi haukuwa katika Ilani, na CCM wengi waliukataa. Lakini kwa busara za Nyerere kwa kuwaza nje ya Box alisema hata wachache wasikilizwe! Akungoja vurugu zitokee, ndo aruhusu vyama vingi. Hakusema hilo alikuwepo katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 1990. Si kila kitu ni Ilani ya Uchaguzi.
Tunahitaji kiongozi mwenye maono, anae waza zaidi nje ya box si kufungwa na visingizio vya Ilani ya CCM. Na hii inadhihirisha udharimu wa CCM kwa wananchi. Wanakwepa kuweka mabadiliko ya Katiba katika Ilani yao kwakua, hawajali kabisa wananchi. Wapo kwa maslahi yao binafsi. Ilani lazima itazame nini pia wananchi wanataka, si kulaghai laghai. Ifike mwisho sasa. TUMECHOKA!
Vyeo vya kupendeleana vitaisha na CCM itakufa mazima, tuidai katiba mpya kwa nguvu zetu zote na isiwe hisani ya RaisCcm hawawezi kufanya kitu kinachopelekea hatima yao. ccm ni binadamu kama binadamu wengine ambao pia wanatamani waendelee kula mema ya nchi.
Ukiwashangaa ccm kutopenda katiba mpya mimi nakushangaa wewe.
Paschal vyeo vya uteuzi naona kama vimeisha mkuu, naomba urudi kwenye uandishi wako wa 2016 utusaidie kusukuma hili jambo najua unaushawishi mkubwa sn mkuu, ipende nchi kuliko maslahi yako binafsi na MUNGU atakubariki sn mkuu. Tushirikine na NGO's, CDM, watumishi wa MUNGU n.k wengine wapenda nchi kama mimi.Naunga mkono, kiongozi huyu sasa ni Samia. Suala la Katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM iliyopita, kwa vile lilikuwepo na JPM akasema sio kipaumbele chake na hatukumshinikiza, na kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya sasa halipo, then tusimshinikize Samia, ni rais mwenye maono, msikivu, ana jicho japo linaonekana limeregea, lakini linaona sana!.
Angalia sifa nyingine za samia
PSiku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
Wanabodi, Leo asubuhi nimeangalia kipindi cha mahojiano ya Makamo wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumzia Siku ya Wanawake Duniani kwenye TBC akihojiwa na Shabani Kissu. Kwa Waliosikiliza kipindi hiki, kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya...www.jamiiforums.com
Nakubaliana na wewe mkuuKatiba mpya itapatikana iwapo kizazi hiki cha kinafiki kitaondoka chote
Ni dharau sababu wanajua dola ipo upande waoTatizo kubwa la ccm Ni kutosoma mahitaji ya umma kwa wakatii
Tunaidai vipi? Kwa kupost humu jf nadhani haitoshi hata kidogo. Tujikite kwenye uelimishaji mitaani, makazini, mashambani na mitandao kama youtube ,fb na instagram.Vyeo vya kupendeleana vitaisha na CCM itakufa mazima, tuidai katiba mpya kwa nguvu zetu zote na isiwe hisani ya Rais
Hata hapa wanapita wengi sn, pia ulichosema ni sahihi tuelimishe jamii ijue umuhimu wa katiba mpyaTunaidai vipi? Kwa kupost humu jf nadhani haitoshi hata kidogo. Tujikite kwenye uelimishaji mitaani, makazini, mashambani na mitandao kama youtube ,fb na instagram.
Humu jf nadhani ni kila mtu ameshachagua upende wake.