CCM ikitawala miaka 100 bado hatutopata Katiba mpya kwakuwa kila Rais anaamua atakavyo?

Ccm hawawezi kufanya kitu kinachopelekea hatima yao. ccm ni binadamu kama binadamu wengine ambao pia wanatamani waendelee kula mema ya nchi.
Ukiwashangaa ccm kutopenda katiba mpya mimi nakushangaa wewe.
 
Tunahitaji kiongozi mwenye maono, anae waza zaidi nje ya box
Naunga mkono, kiongozi huyu sasa ni Samia. Suala la Katiba lilikuwepo kwenye ilani ya CCM iliyopita, kwa vile lilikuwepo na JPM akasema sio kipaumbele chake na hatukumshinikiza, na kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya sasa halipo, then tusimshinikize Samia, ni rais mwenye maono, msikivu, ana jicho japo linaonekana limeregea, lakini linaona sana!.
Angalia sifa nyingine za samia
P
 
Ma-Askofu wakianza kudai katiba mpya sasahivi inapatikana
 
Da! umepiga nyundo sn mkuu
 
Ccm hawawezi kufanya kitu kinachopelekea hatima yao. ccm ni binadamu kama binadamu wengine ambao pia wanatamani waendelee kula mema ya nchi.
Ukiwashangaa ccm kutopenda katiba mpya mimi nakushangaa wewe.
Vyeo vya kupendeleana vitaisha na CCM itakufa mazima, tuidai katiba mpya kwa nguvu zetu zote na isiwe hisani ya Rais
 
Paschal vyeo vya uteuzi naona kama vimeisha mkuu, naomba urudi kwenye uandishi wako wa 2016 utusaidie kusukuma hili jambo najua unaushawishi mkubwa sn mkuu, ipende nchi kuliko maslahi yako binafsi na MUNGU atakubariki sn mkuu. Tushirikine na NGO's, CDM, watumishi wa MUNGU n.k wengine wapenda nchi kama mimi.
 
Yoyote atakae ingia pale iwe ccm ,chadema,nccr,tlp hakuna atakae badilisha katiba ilivyo nona vile kwa kunufaisha sehemu flani tu
 
Vyeo vya kupendeleana vitaisha na CCM itakufa mazima, tuidai katiba mpya kwa nguvu zetu zote na isiwe hisani ya Rais
Tunaidai vipi? Kwa kupost humu jf nadhani haitoshi hata kidogo. Tujikite kwenye uelimishaji mitaani, makazini, mashambani na mitandao kama youtube ,fb na instagram.
Humu jf nadhani ni kila mtu ameshachagua upende wake.
 
Hata hapa wanapita wengi sn, pia ulichosema ni sahihi tuelimishe jamii ijue umuhimu wa katiba mpya
 
IliTanzania itoke kweye hili tatizo la maendeleo endelevu ni lazima tubadili Katiba kwanza. Nchi ijengwe na wananchi wenyewe na sii serikali. Too musch power to President ni tatizo pia, hawezi kuwajibika kwa waliomchagua ila kwa chama kilichomweka madarakani. Na ili chama kibakie madarakani lazima wapinge mabadiliko ya katiba kwa nguvu zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…