Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Chama Cha mapinduzi kilipasuka miakaa tisa iliyopita; ufisadi, undugu na umimi ndio uliopelekea kikose dira kwenye jamii. Leo kinachofanyika siyo kukijenga chama wala kuijenga Nchi bali chama kimejikita kujitoa magamba Kisha yanaota mapya.
Leo mataifa mengi yanapambana kusimamia uchumi lakini Tanzania tunasimamia Kwa namna yoyote Ile kujenga chama aidha Kwa kuumiza Watu au kutumia Dola kutokukosoa mawazo ya Mwenyekiti.
Mwenyekiti aliyepita aliamua anachotaka bila wanachama kusema chochote; Kila alichowaza mwenyekiti ndicho kilionekana ni SAHIHI na watu wote wakalazimishwa kuzunguka kuzitangaza fikra za mwenyekiti bila kujali yupo sajhihi au hayupo SAHIHI.
Leo mwenyekiti kaondoka kaja mwenyekiti Mpya, amekuja na agenda zake zinazokinzana 100% na mtangulizi wake lakini watu walewale waliomsifia mwenyekiti aliyepita ndio haohao wanaomsifia mwenyekiti aliyepo. Hivyo Kwa tafsiri nyepesi chama hakina haja na wanachama Bali kinamsikiliza mwenyekiti.
Unajiuliza Leo Kinana na Membe wanatija Gani Kwa uchumi wetu? Makundi Yao yana tija Gani Kwa Taifa? Watoto wa Marais na vigogo wa CCM wanaiwazia vyema Tanzania au wanawaza namna ya kuziimarisha familia zao? For years now tumepita kwenye maumivu makubwa Hawa wote hakuna aliyesimama akasema lolote. Wao wamepita magumu yaliyokinyume na haki, hakuna aliyeweza hata kujitetea badala yake pamoja na ukongwe wao walikwenda kumpigia magoti mwenyekiti. Kama walishindwa kusimama na kujitetea wanaweza kusimama kulitetea Taifa?
Sifa kuu ya kiongoz wa watu nikujisimamia Mwenyewe, uwezi kushindwa kujisimamia ukaweza kuwasimamia wengine. Kama umeshindwa kusema hapana Kwa udhalilishaji juu Yako ni vigumu kuwasemea wengine, na hapo ndipo utakapobaini kilichofanywa na chama Cha mapinduzi nikuwaleta walioshindwa kujisimamia wakatusimamie. Impossible.
Endapo Leo hii dola itajitenga na CCM na kuacha uwanja huru wa siasa CCM inaondoka; ipo Wazi kwamba CCM badal ya kufanya siasa wanaangaika na nafsi na Mali za wapinzani wao. Siasa za hoja zimekwama Kwa sababu hakuna sera inayoeleweka: sera ya CCM ni Mawazo ya Mwenyekiti Jambo ambalo siyo SAHIHI Kwa Nchi.
Tunahitaji kutoka kwenye ujima wa kumwita Membe Kachero mbobezi hata pale tunapoona Wazi kwamba mbinu za ukachero haziwezi kumsaidia yeye Mwenyewe, hazimsaidii kuona Mbele Wala hazimsaidii hata kujilinda.
Tunahitaji kuachana na fikra za akina Kinana ambao hata uwezo wakudhibiti mawasiliano yao wenyewe awana na pale wanapobaini wanaingiliwa Awana Cha kufanya. Tuachane na watu ambao wao uchungu nikuumizwa Kwa familia zao na Mali zao na siyo wananchi.
Kiongozi anayeshindwa kukemea maovu dhidi yake awezi kuongoza watu; kama ameshindwa kujihudumia na kujisimamia ni vigumu kusimamia wengine.
Tukubali CCM imebaki Mali ya KUNDI la watu flani Kwa maslahi Yao binafsi na siyo chama kilichojengwa Kwa maslahi ya wananchi.