ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Kwa maoni yangu moja ya mbinu ambazo CCM imezitumia kwa ustadi mkubwa ni kumuingiza MwanaFA serikalini. Sizungumzii uwezo wake binafsi au kama anafaa kuwa waziri au hafai, bali athari za kisiasa ambazo hatua hiyo imezalisha ndani ya tasnia ya muziki.
MwanaFA ni mmoja wa wasanii wenye ushawishi mkubwa katika muziki wa Hip Hop Tanzania. Ana heshima kubwa kutoka kwa mashabiki na wasanii wenzake. Matokeo yake ni kwamba wasanii wengi wanaonekana kuwa waangalifu sana wanapoulizwa maswali yanayohusu siasa au utendaji wa serikali.
Leo ukitazama interviews za wasanii wa Hip Hop kama Nikki Mbishi, P The MC na wengine wengi utakuta wakiepuka kujieleza wazi kuhusu misimamo yao ya kisiasa. Utasikia kauli kama "mimi si mfuasi wa chama chochote" au "sipendi kuzungumzia siasa". lakini miaka iliyopita ambapo wasanii walikuwa wakitoa maoni yao kwa uwazi zaidi kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa.
MwanaFA ndani ya serikali ameongeza ugumu wa wasanii kuikosoa serikali kwa nguvu kama zamani wanahofia kuonekana wanamshambulia mmoja wa watu wao wenyewe ni kama wanamuonea aibu..wanaujua ukweli ila wanaishia kuiponda serikali kimya kimya kwa chini chini wakati wao ndo walikuwa wanapaswa wawe kioo cha jamii waelezee hisia za watu nazungumzia hasa wasanii wa hiphop.
Pia tunaona baadhi ya wasanii waliokuwa wakionekana wakali katika ukosoaji zamani, leo hii wamekuwa watetezi au wasifiaji wa serikali. wote wasanii wakina dudubaya wametepetwa kila wakipost sasa hivi lazima amtag Rais mama samia ..labda aliyebaki kwenye harakati ni sugu peke yake..nitajie msanii gani mwingine anakosoa serikali inapokosea kwa sasa.
Ikumbukwe kuwa wasanii wana ushawishi mkubwa sana kwa vijana. Watu wengi hufuatilia page zao kila siku kuliko hata kufuatilia wanasiasa. Mitazamo yao inaweza kuathiri namna mashabiki wanavyoiona serikali, upinzani au masuala ya kijamii.Kwa hali hio kweli upinzani tutaboa mbele ya ccm?