Wolle Melkas Fernando
JF-Expert Member
- May 4, 2016
- 284
- 396
CCM inapaswa kuacha kutafuta visingizio kuhusu kuporomoka kwa mvuto wake kisiasa. Tatizo kubwa haliko kwa wapinzani, bali kwenye maamuzi ambayo chama chenyewe kimekuwa kikiyafanya.
Baada ya kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kulikuwa na kundi kubwa la wanachama na wafuasi waliotaka kuona umoja ukirejeshwa. Humphrey Polepole alikuwa miongoni mwa watu ambao wangeweza kuwa daraja la kuunganisha makundi tofauti ndani ya CCM na hata kupunguza msuguano wa kisasa nje ya CCM.
Badala yake, mazingira yaliyohusu kupotea kwake yalizua maswali mengi ambayo, kwa maoni ya wengi, hayajajibiwa kwa kiwango cha kuridhisha si kwa upande wa CCM hata serikali. Na CCM ilishindwa hata kulaani tu kutoweshwa kikatili kwa Polepole.
Wafuasi wa Magufuli walikuwa wanamwona Polepole kama faraja Yao, baada ya kutoweshwa kwake, wengi wameichukia CCM. Kuliko njia iliyotumika kumnyamazisha, ni bora ingetumika njia yenye faida kwa Chama.
Kisha yakafuata matukio ya Oktoba 29, 2025 na kauli mbalimbali zilizoongeza hasira na kupunguza imani ya wananchi. Hayo yote yameendelea kuathiri taswira ya CCM mbele ya umma.
Siasa si urithi wa kudumu. Unajua iko hivi Wananchi ndio huamua nani awaongoze kwa kuzingatia matendo, uwajibikaji na mikakati na si historian inayoamua Nani aongoze.
Ndiyo maana CCM inapaswa kufanya tathmini ya kina, kujisahihisha na kurejesha imani ya wananchi badala ya kutafuta mchawi wa changamoto zake.
Na Kwa mtazamo wangu, CCM imechelewa kujirekebisha. Isipokuwa kutokee mabadiliko makubwa ya kiuongozi, kimkakati na katika namna inavyowasiliana na wananchi na binafsi huenda isiwe rahisi CCM kurejea kwenye kiwango cha mvuto na ushawishi wa kisiasa kilichowahikuwa NAO miaka ya huko nyuma.