CCM Iliyo Hitimu - Pictorial Paspektiv

CCM Iliyo Hitimu - Pictorial Paspektiv

Steve Dii

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2007
Posts
6,402
Reaction score
1,273
There goes my thousand words......

steved-albums-mh_pinda-picture170-ccmmbeya-jkziara-michuziblog.jpg

"JK akisalimiana na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali muda mfupi kabla ya kufungua jengo jipya la halmashauri hiyo jana. Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu" (18-10-2008)

Picha na maelezo kwa hisani ya: issamichuzi.blogspot.com

There goes my thousand words......

steved-albums-mh_pinda-picture170-ccmmbeya-jkziara-michuziblog.jpg

"JK akisalimiana na baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbarali muda mfupi kabla ya kufungua jengo jipya la halmashauri hiyo jana. Picha zote na mdau Freddy Maro wa Ikulu" (18-10-2008)​

Picha na maelezo kwa hisani ya: issamichuzi.blogspot.com​

teh teh teh, hayo majoho yasikutishe, pengine wamehitimu nursery school, shule ya msingi au hata ya shule ya upili tu.
 
teh teh teh, hayo majoho yasikutishe, pengine wamehitimu nursery school, shule ya msingi au hata ya shule ya upili tu.

.... he he, mimi nilifikiri ulimbukeni upo kwenye mchepuko wa 'international school academies' za dar tu, kumbe ume transpire jamii nzima na rika zote !! lol
 
.... he he, mimi nilifikiri ulimbukeni upo kwenye mchepuko wa 'international school academies' za dar tu, kumbe ume transpire jamii nzima na rika zote !! lol

Hao kama sikosei ni madiwani, watu bwana kwa kupenda misifa.... hivi hawa jamaa kwani ni lazima waende kumpokea rais; majukumu yao wanamwachia nani? je isingetosha rais akawafuata huko kwenye chumba cha mkutano?
 
Hivi ni kwa nini wanavaa hayo majoho? yana maana gani?
 
Lakini ukiangalia hizi picha yani una cheka mwenyewe tu.
 
Lakini ukiangalia hizi picha yani una cheka mwenyewe tu.

Labda ni sikukuu ya mavazi. FairPlayer au Ladslaus Modest watakuwa na explanation nzuri tu zaidi... 🙂
 
Labda ni sikukuu ya mavazi. FairPlayer au Ladslaus Modest watakuwa na explanation nzuri tu zaidi... 🙂

Huwa naelewa wanafunzi wa sekondari wanapofanya hivyo LAKINI kwa hizi yani taswira inayokuja haraka haraka ni kuwa bado tuna safari ndefu.
 
Hivi ni kwa nini wanavaa hayo majoho? yana maana gani?

Nasikia walikuwa wanamwambia JK usione kuwa sisi ni madiwani tumepiga shule wewe...... ni kiwango gani wamefika mimi sijui

Si unaona hata huyo jamaa wa kwanza alivyotoa tumbo kumwonyesha JK.. Lol

Bado sijajua akienda BK nao watavaa majoho ya majaji .... lol
 
Na nyinyi bwana, sasa bila hayo magwanda mngejuaje kuwa ni ni madiwani? Hata mfalme huwezi kumjua bila taji.
 
OK, hayo majoho yanaweza kuwa sehemu ya sare za madiwani, sasa watuambie hizo mortarboards vichani ni za nini? Hebu angalia definition halisi ya mortarboard.

mor·tar·board [ˈmɔrtərˌbɔrd, -ˌboʊrd] : Also called cap, a cap with a close-fitting crown surmounted by a stiff, flat, square piece from which a tassel hangs, worn as part of academic costume.
 
Tanzania ya sasa kila kukicha watu wanabuni njia za kutumia wenyewe wanavyoita, kuvuta. Ukiambiwa kiasi alichovuta mkandarasi aliyeshona hayo majoho machozi yanaweza kukutoka. Rais alitakiwa kuwakemea pale pale alipokuwa akisalimiana nao.
 
Halmashauri zetu nyingi ni MASKINI sana kugharamia anasa kama hizi huku shule hazina madarasa, madawati, nyumba za Walimu; Zahanati ziko hoi; mahakama za mwanzo hazina kiti hata cha Hakimu; barabara mbovu kabisa....
 
Back
Top Bottom