Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
CCM imekuwa ikipoteza uungwaji mkono katika maeneo mbalimbali ya nchi kwa muda sasa na chaguzi zimekuwa zikithibitisha ukweli huu.
CCM ilianza kufutika taratibu katika mikoa ya Kigoma,mikoa ya kanda ya kaskazini, ikaja Dar-es-Salaam, kisha Mbeya, maeneo ya mijini na kwenye majiji nchi nzima hasa mwaka 2015, na hii 2020 inapoteza kanda karibu zote ambazo zilikuwa ngome yake mfano ni kanda ya kati na kanda ya kusini bila kusahau kanda ya ziwa ambako inafutika kwa kasi zaidi mwaka huu.
Kwa kanda ya kati, mkoa wa Dodoma pekee ndio unaoweza kuibeba CCM na wagombea wake kwa mwaka huu huku ikikabiliwa na hatari ya kukataliwa katika maeneo mengi ya mkoa wa Singida.
Katika mikoa iliyoko katika Kanda ya Nyanda za Juu kusini, CCM ndio kabisa inatokomea na huku kote CHADEMA ndio inatawala na ACT ikiwa na nafasi ya kutawala maeneo mengi ya mkoa wa Kigoma kwa upande wa kanda ya Magharibi.
Kanda ya kusini (mikoa ya Lindi na Mtwara) nako mambo yanaendelea kuharibika na hii ilianza mwaka 2015 kutokana na issue ya gesi, na sasa issue ya korosho imekuja kuharibu zaidi na kuweka CCM pabaya zaidi.
Ukiacha Dodoma, CCM imebaki na mikoa kama Rukwa, Tabora,Tanga, Pwani na mingineyo michache tena ikiwa na nguvu zaidi vijijini kuliko mijini katika mikoa hii.
Kwa upande wa Zanzibar, huko ndio kabisa wana hali mbaya kuanzia Pemba na sasa hata Unguja.
Kwa kifupi, CCM inaendelea kupoteza ngome zake zote na sasa inaanza kukataliwa hata katika maeneo mengi ya vijijini mfano mzuri ni huko Tarime katika mkoa wa Mara.
Habari ndio hio!