CCM imefungamanishwa na DOLA ndio sababu haikusajiliwa 1992, Waziri aliyesema haiwezekani kuitoa CCM madarakani yuko sahihi!

Kwa vile CCM wamefunga milango ya kuweza kuwa na uchaguzi huru na haki ni mapinduzi ya kijeshi pekee au machafuko yataiondoa madarakani.
 
Dkt Bashiru alishasema itakua ni ujinga kuwa na dola na kushindwa kuitumia iyo dola kubaki madarakan πŸ˜€
 

..Nchi ingekuwa chini ya serikali ya mpito ambayo ingeratibu usajili wa vyama vipya vya siasa, na kuandaa uchaguzi mkuu.
 
Sasa Kwa miaka yote kiliyokaa kwenye utawala ulitegemea kingekua tofauti na haya mawazo yako mkuu? Ingekua ni ajabu sana.
 
Ufafanuzi mzuri
 
Hata KANU walikuwa hivyo. Walioko huko ulikotaja nao hawaitaki ccm
 
Shukran Yohanambatizaji. Hatimaye UMESEMA!

Huu ndio ukweli ambao Watanzania wote wanatakiwa kuujua: CCM=SERIKALI AKA DOLA; CCM=STATE PARTY (CHAMA DOLA). Unaitoaje madarakani dola yenye vifaru, mizinga na vikorombwezo vyote? Kwa vikaratasi? Kwa kelele majukwaani na mitandaoni?

Kifupi, dhana ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa (multiparty democracy) HAIPO. Kilichopo ni ulaghai.

Yaani CHADEMA na vyama vingine vya upinzani vinashindana na DOLA kwenye majukwaa ya siasa! Huo ni ubatili: FALLACY. Ndio maana kila siku wanaitwa WASALITI aka vibaraka wa mabeberu.

Vyombo vya dola (incl. polisi) haviwezi kumuelewa mtu anayempinga au kumkosoa amiri jeshi mkuu hadharani kwa kisingizio cha kufanya siasa! Wanaona ni uhaini na utovu wa nidhamu usiovumilika!

Usipokubaliana na ukweli huu wameshatoa ushauri: Hamia Burundi au ingia mwenyewe porini tukutane huko! 😳
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…