CCM imeharibu Elimu yetu. Utumiaje kiingereza miaka 10 kujifunzia halafu usijue kiingereza?

Zamani zipi hizo? Hao wa zamani si ndiyo hawa akina Jenista Mhagama, ndungulile na Ndalichako? Mbona wanaongea broken?

Wale wanasheria waliokuwa wanaitetea serikali kule nje kwenye zile kesi za uvunjwaji holela wa mikataba, si wazamani wale?

Mfano prof. Mduma na prof. Osolo, si wa zamani wale? Mbona wanaongea kwa shida sana??

Hiyo zamani mlikuwa mnasifiana ujinga tu.
Hakuna unachoelewa.

Tumesoma hapa hapa. Shule za serikali. Tumefanya kazi kwenye serikali za nje na mashirika ya kimataifa miaka mingi kwa elimu hii hii ya shule za serikali za Tanzania. Na tumeheshimika sana.

Wewe unazungumzia wateule wa CCM kwa kigezo cha uchawa. Tanzania ina wasomi wa kweli wengi ndani na nje ya nchi. Nyinyi kwenye circles zenu za CCM mnazunguka na majina hayo hayo ya machawa mkifikiri ndio wasomi pekee walioko nchini.
 
umetumia utafiti au kipimo kipi kwamba wasomi wetu hawajui english?
 
Hakuna unachoelewa.

Tumesoma hapa hapa. Shule za serikali. Tumefanya kazi kwenye serikali za nje na mashirika ya kimataifa miaka mingi kwa elimu hii hii ya shule za serikali za Tanzania. Na tumeheshimika sana.

Wewe unazungumzia wateule wa CCM kwa kigezo cha uchawa. Tanzania ina wasomi wa kweli wengi ndani na nje ya nchi. Nyinyi kwenye circles zenu za CCM mnazunguka na majina hayo hayo ya machawa mkifikiri ndio wasomi pekee walioko nchini.
Mmefanya kazi nchi za nje halafu majina yenu yako chini ya kapeti? Mbona hamjulikani? Mashirika gani hayo?
 
Unawafahamu wasomi wote wanaofanya kazi nje ya nchi?

Nitajie Watanzania unaowahafamu hata 5 ambao ni senior officials kwenye mashirika ya UN, AU, IRC, n.k.
 
Moderator hii ni hoja ya kisiasa msiigeuze ya lugha.

Suala la Elimu ya nchi hii kuwa ya kiwango cha juu ama cha chini ni la mjadala.

Lakini kiwango cha usomi wa wasomi wetu si mjadala unaotakiwa kuahirishwa.

Hivi wasomi wetu tunawapimaje, kwa nini wasomi wetu linapokuja suala la ushindani na wasomi wa nchi nyingine linakuja suala la udhaifu wa wasomi wetu kutokuwa na weledi wa matumizi ya lugha ya kiingereza?

Hivi Elimu yetu ni duni ama wasomi wetu ni weledi ila hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha?

Kama hawajui kiingereza kwa ufasaha imekuwaje walifaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu?

Yaani lugha inayotumiwa kujifunzia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita (miaka 6) na vyuoni (miaka 3 - 4 au miaka 7) wasomi wetu inakuwaje hawana weledi nayo?

Kuna sehemu CCM wameharibu Elimu yetu ila wanasingizia kiingereza.
Wewe umeona wapi watanzania wanafundisha kwa kiingereza? Watu wanafundishwa somo la English yenyewe kwa kiswahili😂😂😂😂
 
English medium unazijua huzijui ? Nenda kakutane na watoto wa msingi uone wanavyozunguza kingereza kilichonyooka

Kenya hapo lugha ya nyumbani kiswahili kama sisi lakini shule zao zote za Msingi ni English medium Kenya mbona kwao sio issue kingereza

Hata sisi lugha ya nyumbani kiswahili mtoto akitoka shule kama yule wa Kenya anakutana na kiswahili mbona wanamudu kingereza vizuri tu

Labda wewe hujafika Kenya lugha ya nyumbani kiswahili shule ndio kingereza na wako fit.Sababu muda mwingi wa siku watoto wanakuwa shule environment ya kingereza kitupu .Nyumbani wanakuwa na muda kidogo sana ndio maana wana master kingereza upesi

Tofauti na shule ya kayumba siku nzima shule ntoto anasoma kiswahili tu na nyumbani hapo unazalisha mtoto mswahili hasa kingereza kwake itakuwa mtihani mzito kukimudu.
Sio kweli unapotosha hicho kingereza cha English medium cha ajabu sana uzuri hizo shule nazifahamu
 
Ndugu yangu,huwezi kutia Neno hapa tujifunze??kwanini watoto wana struggle kuongea kilugha cha malkia??
 
Embu na wewe weka video ukiongea na kuzungumza Kizungu.
Mleta mada sio kiongozi hatutaki hiyo video yake unayoiomba, tunataka video za viongozi hasa ma ccm maana ndio wanaotuongoza...tuanzie na ule utopolo wa Jenista Mhagama kwenye uchaguzi mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika.
 
Acha ulimbukeni.kwani wachina wanaongea kiingereza? Warusi wanaongea kiingereza? Acha utumwa wa kifikra
 
Unawafahamu wasomi wote wanaofanya kazi nje ya nchi?

Nitajie Watanzania unaowahafamu hata 5 ambao ni senior officials kwenye mashirika ya UN, AU, IRC, n.k.
1. Asha Rose Migiro,- UN undersecretary general prof.
2. Anna Tibaijuka:-UN Habitat.
3. Salim Ahmed Salim....AU secretary general.
4. The late Mahiga .. permanent representative of Tanzania to the UN.
5. Sir George Kahama....
 
Hiki nacho ni kimombo? Mbona hukijui? Watanzania mna njaa, kila kitu hamuwezi.

Mpira, kuogelea, kuruka juu na chini, kucheza ngumi na kufanya muziki nako kumewashinda kimataifa kwasabb ya kimombo?

Olympic ya mwaka huu tulipeleka watu 3. Nchi nzima kwa michezo yote 40 ya Olympic tulipeleka watu 3??? Aibu naona mimi.
Lawama kwa Samia, ahahahah
 
Hoja sio kingereza ni mhimu au sio mhimu... Mleta mada anauliza inakuwaje miaka kumi ya kusoma kwa kutumia kingereza na bado mtu hawezi kuongea lugha aliyotumia kusoma... Inaacha maswali juu ya ubora wa elimu yetu... That's the point.
Nashukuru miongoni mwa wengi waliochangia wewe umeelewa hoja yangu.

Sijui ni wangapi wamewahi kusoma kitabu kinaitwa "Language Crisis in Tanzania. The myth of English Versus Education" kilichoandikwa na Zaine M. Roy-Campbell na Martha A.S. Qorro.

Au ni wangapi wamewahi kusoma vitabu vilivyochapishwa na Haki Elimu vya "Nyerere On Education" Juzuu ya kwanza na pili?

Jee ni udhaifu wetu wa kimantiki ndiyo unaotufanya tuwe na Elimu duni ama ni matumizi ya lugha ya kufundishia masomo kwenye shule zetu?

Hoja hapa siyo Kiswahili ama Kiingereza bali inakuwaje mtu afundishwe Kwa miaka kumi Kwa kiingereza halafu asijue hicho kiingereza kilichotumika kufumfundishia maarifa inayodaiwa anayo?
 
1. Asha Rose Migiro,- UN undersecretary general prof.
2. Anna Tibaijuka:-UN Habitat.
3. Salim Ahmed Salim....AU secretary general.
4. The late Mahiga .. permanent representative of Tanzania to the UN.
5. Sir George Kahama....
Acha hizo political appointments. Tena za kale. Heri ungewataja Dr Ndugulile na late Dr M Malechela ambao ni professionals wa maeneo yao.

Hapa naongea hasa kuhusu maafisa/wataalamu waandamizi (wakuu wa idara na vitengo) walioajiriwa kiushindani (meritorious) kwa juhudi zao wenyewe bila back-up ya serikali.

Hao ni wengi tu. Hawavumi kwa kuwa hawako kwenye circles za kisiasa wala sio media personalities. Ni watu wa taaluma; watendaji.
 
Moderator hii ni hoja ya kisiasa msiigeuze ya lugha.

Suala la Elimu ya nchi hii kuwa ya kiwango cha juu ama cha chini ni la mjadala.

Lakini kiwango cha usomi wa wasomi wetu si mjadala unaotakiwa kuahirishwa.

Hivi wasomi wetu tunawapimaje, kwa nini wasomi wetu linapokuja suala la ushindani na wasomi wa nchi nyingine linakuja suala la udhaifu wa wasomi wetu kutokuwa na weledi wa matumizi ya lugha ya kiingereza?

Hivi Elimu yetu ni duni ama wasomi wetu ni weledi ila hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha?

Kama hawajui kiingereza kwa ufasaha imekuwaje walifaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu?

Yaani lugha inayotumiwa kujifunzia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita (miaka 6) na vyuoni (miaka 3 - 4 au miaka 7) wasomi wetu inakuwaje hawana weledi nayo?

Kuna sehemu CCM wameharibu Elimu yetu ila wanasingizia kiingereza.
Ukitaka kuua Taifa lolote lile hapa duniani, ua mifumo yake ya elimu kwanza. Ukiua mifumo yake ya elimu, then automatically Taifa hilo litakuwa limekufa.
 
Moderator hii ni hoja ya kisiasa msiigeuze ya lugha.

Suala la Elimu ya nchi hii kuwa ya kiwango cha juu ama cha chini ni la mjadala.

Lakini kiwango cha usomi wa wasomi wetu si mjadala unaotakiwa kuahirishwa.

Hivi wasomi wetu tunawapimaje, kwa nini wasomi wetu linapokuja suala la ushindani na wasomi wa nchi nyingine linakuja suala la udhaifu wa wasomi wetu kutokuwa na weledi wa matumizi ya lugha ya kiingereza?

Hivi Elimu yetu ni duni ama wasomi wetu ni weledi ila hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha?

Kama hawajui kiingereza kwa ufasaha imekuwaje walifaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu?

Yaani lugha inayotumiwa kujifunzia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita (miaka 6) na vyuoni (miaka 3 - 4 au miaka 7) wasomi wetu inakuwaje hawana weledi nayo?

Kuna sehemu CCM wameharibu Elimu yetu ila wanasingizia kiingereza.

High time now we start addressing some of these issues at individual level, group leven and eventually to the majority in puplic.

Kuna maneno ambayo hata ukisema vip hakuna anayesikia. Wakati mimi nasoma, nikiwa kidato cha pili, rafiki yangu alinipeleka library tukasome.

Yeye baba yake alikuwa Professor. Ila kile alichoanzisha, sijui hata nisemeje..all the difference started there. Kusoma na kujielimisha. Sio kusoma ili ufaulu wakati hujaelimika.
 
Ni seme katuika wakati mgumu nilioupitia kwenye kusoma ni Ile natoka shule ya msingi kayumba alafi naenda form 1 kukutana na kingereza,Ile kitu ni tatizo Yani unakariri vitu mpaka kichwa kinachoka.ivi Hawa wenye mamlka wao haoni hii shida?
 
Inanishangaza, unakuta mtu form six kapasua ila lugha ya malkia haipandi, alijielezazaje?
 
Moderator hii ni hoja ya kisiasa msiigeuze ya lugha.

Suala la Elimu ya nchi hii kuwa ya kiwango cha juu ama cha chini ni la mjadala.

Lakini kiwango cha usomi wa wasomi wetu si mjadala unaotakiwa kuahirishwa.

Hivi wasomi wetu tunawapimaje, kwa nini wasomi wetu linapokuja suala la ushindani na wasomi wa nchi nyingine linakuja suala la udhaifu wa wasomi wetu kutokuwa na weledi wa matumizi ya lugha ya kiingereza?

Hivi Elimu yetu ni duni ama wasomi wetu ni weledi ila hawajui lugha ya kiingereza kwa ufasaha?

Kama hawajui kiingereza kwa ufasaha imekuwaje walifaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu?

Yaani lugha inayotumiwa kujifunzia kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita (miaka 6) na vyuoni (miaka 3 - 4 au miaka 7) wasomi wetu inakuwaje hawana weledi nayo?

Kuna sehemu CCM wameharibu Elimu yetu ila wanasingizia kiingereza.
Kujua Kiingereza kunataka mazoezi ya kukitumia.

Tanzania watu wanaongea Kiingereza nje ya hizo shule?
 
Kuongea kingereza siyo usomi china , Japan, Russia hawaongei kingereza ila wanamchango mkubwa kwenye Technology servicescape
Je huoni kuwa elimu yao imejengwa katika lugha hizo?
Je elimu yetu imejengwa katika lugha zetu?
 
Back
Top Bottom