CCM limebaki kuwa kusanyiko la waramba asali. Asiyeramba asali anapiga yowe linalowashitua wenzie.Enzi za kale mfalme alipokuwa mwoga akaanza kuhisi kila mtu ni adui yake, kila mtu anataka kumpokonya madaraka, basi alikuwa anazungukwa na chawa wanaomwongopea na kumfanya ashughulikie wale wanaowaona ni hatari kwao hao machawa, mwisho hao machawa ndio wanaokuja kumpeleka shimoni.
Waache wafu wazikane. Nyerere alisemaga mpinzani wa kweli wa CCM atatoka ndani ya CCM yenyewe. Wosia huu ni lazima iko siku utatimiaSijaona wala kusikia kibaya chochote kutoka kwa Bashiru, kwasababu watawala walipoomba kura na kuchaguliwa walikuwa wanaomba kazi siyo kunyenyekewa na kuogopwa
MANENO tu ya BASHIRU wanachama wote Wanatetemeka Aibu kubwaCCM imechakaa sana, imekosa watu wenye nguvu za hoja, imejaa watu waoga wanaogopa hata watoto wadogo wanaopigana wakiwa wamevalishwa sare za CCM.
Walianza kuogopa wapinzani lakini sasa wanaogopana hata wenyewe kwa wenyewe. Wasipokuwa makini lazima kutatokea jambo lisilofaa.
sio bure ila wanajua kuwa wako madarakani kwa njia ambazo Mungu hana hamu nazo, na kila mwana CCM analifahamu hili. Ukweli huu ndio unaosababisha wana CCM kunyamazishana kwa njia mbalimbali zinazojumuisha kutishana, kuvuana uwanachama kwa muda tu, kushirikisha watoto wao kwenye serikali, kupewa kazi mbalimbali, nk ilimradi tu kunyamazishana, maana kila mwanaCCM anafahamu wanafanya nini ili kubaki madarakani. Ndio maana Bashiru aliyekuwa katibu Mkuu wao anataja mambo ya rushwa, t-shirts na kofia na nyimbo kama moja ya njia zinazotumika kubaki madarakani wakati wa uchaguzi.MANENO tu ya BASHIRU wanachama wote Wanatetemeka Aibu kubwa
✍️Waache wafu wazikane. Nyerere alisemaga mpinzani wa kweli wa CCM atatoka ndani ya CCM yenyewe. Wosia huu ni lazima iko siku utatimia
Binafsi siamini sana kwenye katiba mpya, bali ninaamini kwenye utayari wa wananchi kutaka na kusimamia ukweli na mabadiliko. Marekani wana katiba nzuri na iliyokomaa lakini Trump alidai ameibiwa kura vilevile. Shida iko pale wananchi watakapogundua kuwa kura zimeibwa huwa wanafanya nini. Kile wananchi wanachofanya baada ya kura kuibiwa ndicho kitu mwizi wa kura anachokiogopa. Wananchi wetu wana tabia ya kuwaachia akina Mbowe na wenzake waganga njaa zao waamue cha kusema na cha kufanya.Katiba mpya ndiyo kila kitu