Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,483
- 40,130
Leo tarehe 04 Agosti 2025 nchi nzima imeshuhudia zoezi la kura za uteuzi wa wagombea nafasi za Udiwani na Ubunge kuelekea uchaguzi mkuu hapo Oktoba 29.
CCM ilianza kuvunja Katiba ya Nchi baada ya kumteua Samia Suluhu kuwa mgombea pekee wa Urais hapo January ambapo kwa mujibu wa Ibara ya 38 ya Katiba ya JMT, zoezi hilo lilipaswa kufanyika baada ya Agosti 3 siku Bunge lilipovunjwa rasmi.
Katiba ya CCM imebadilishwa kuwaengua wanachama ktk hatua za awali za uteuzi wa wagombea badala yake watiania watasubiri teuzi kutoka Kamati za mikoa na Sekretarieti ya Taifa kufanya mchujo. Hivyo kuwanyima wanachama wagombea wanaowataka.
Tumeona namna ambavyo maeneo mengi nchini wanachama wakirejesha kadi zao na hata kuonesha hisia zao dhidi ya michakato ya uteuzi wa watiania kutoka vikao vya juu vya chama.
Leo tumeona kupitia picha mnato na jongefu vurugu zilizojitokeza wakati wa zoezi la upigaji kura za uteuzi.
Haya na mengine yanadhihirisha kuwa:-

- CCM ndiyo kinara wa uvunjwaji na ukiukwaji wa Katiba na Sheria za nchini
- CCM ndiyo adui namba moja wa demokrasia nchini. Kama inaweza kuwanyima wanachama wake kuteua wagombea, seuse haki za raia kuchagua viongozi wanaowataka?
- Mihimili ya Serikali yaani Utawala, Bunge na Mahakama vimejiunga kuinyonga Katiba ya nchi bila huruma
- Vyombo vya dola vinasimama na CCM kwenye kukiuka haki za raia.