Kwakuwa hata SAA mbovu inasema kweli Mara 2 kwa siku. Ccm inaogopa kusema Mwenyekiti wao anaumwa hajisikii vizuri mpaka wasemewe na cdmKukata tamaa Ni dhambi mbaya sana. Lakini kujifariji kila siku bila Ukweli na jitihada Ni ubwege na uzandiki sana. Mkuu kama hiyo CCM yenu ingekuwa imekufa unadhani Kwanini unaandika uzi mrefu hivyo.
Kama hakuna upinzani ile marufuku ya vyama vya siasa kufanya siasa kwa miaka 5 ilikuwa ya nini? IQ zenu zimeyumba.CCM ife kwa upinzani gani Tz???
You must be sick
Jitu limeshakula ubwabwa wake maharage ya juzi ndo linaanzisha thread ya kitoombo
Tuaandika ili kutimiza ule usemi wa hata SAA iliyokufa kuna wakati inasema ukweli. Ccm bars imekufa kweli na kama huamini subiri Mwenyekiti kiti mpya kutoka ccm ya kuleee asimikwe rasmi.Kukata tamaa Ni dhambi mbaya sana. Lakini kujifariji kila siku bila Ukweli na jitihada Ni ubwege na uzandiki sana. Mkuu kama hiyo CCM yenu ingekuwa imekufa unadhani Kwanini unaandika uzi mrefu hivyo.
Awamu ya tano ilimalizia kuiua CCM iliyokuwa tayari imepigwa jembe la mgongoni na Edward Lowassa alipohamia Chadema.
CCM ya kweli haiwezi kuwa na viongozi aina ya Mh. Polepole na Mh. Bashiru kama watendaji wakuu na kuwafungia nje wenye CCM yao. CCM halisi haiwezi kuwadhalilisha watu kama Kinana, Yusufu Makamba, Nape na wengine kutokana na michango yao kwenye siasa za CCM.
Awamu ya Mh. Magufuli R.I.P haikuamini nguvu ya CCM bali jina lake tu. Walihitaji jina la CCM lakini sio nguvu ya CCM kwenye siasa zao.
Kuondoka kwa Rais Magufuli CCM pia inayo kazi ya kufanya ya kuirudisha CCM kwa wenyewe. Ndiyo maana hata mafanikio ya JPM yanakutana na changamoto kutoka ndani na nje ya CCM baada ya yeye kuondoka.
Bahati yao kubwa ni kumpata Rais Samia ambae sio mwanacha wa kundi hili na kundi lile la CCM Bars, vinginevyo tungeshuhudia makubwa kwwnye vikao vyao.
Imekufa anakosekana wa kusema imekufa.
Miaka 5 hakukuwa na CCM nchini, nchi ni na CCM ni kama vile vilipinduliwa, kulikuwa na kila dalili zote kuwa nchi iliongozwa kijeshi, vyombo vya dola vilionekana zaidi kuliko CCM. Hata vikao vya chama havikiwa vikao vya maamuzi bali vilikuwa vya kubariki maamuzi.CCM iliyokuwa kwenye threat ya kufa ilikuwa 2015, 2020 licha ya faulo still ilikuwa ni CCM yenye nguvu compare to 2015, tatizo washindani wa CCM wameelekeza nguvu nyingi kumnyooshea kidole hayati kuliko CCM yenyewe,then what dakika za mwisho mambo yakiwa magumu wataungana na non CCM kumshutumu hayati then wao watauaminisha umma wao ni wasafi boom wanachukua nchi tena. so nategemea sana kuiona CCM ikiendelea kutawala sababu ya inconsistently ya washindani wake
Waache wajiridhishe. Bunge zima limejaa Wabunge wa CCM halafu mtu anaropoka eti CCM imekufa. Vipi mile Chadema ambayo Mgombea Urais wake anaishi ughaibuni kwa "hawara" utasema kiko hai?Sielewi mtasema nini 2025 kwa kipigo cha mbwa Koko!
CCM ipo haijafa,ndio chama tawala,lakini inapungukiwa hoja zenye ushawishi kwa umma.
Lakini ujio wa SSH unaweza ukairudisha CCM kwenye misingi yake ya awali ya haki kwa wote na kuheshimiana,japo haitakuwa kazi rahisi kwa kundi lenye mlengo wa kushoto kuunga mkono SSH.
Huwezi kudharau kundi hilo kwani katika miaka mitano ya Magufuli limewezeshwa kiuchumi na limejizatiti sana katika ngazi zote za utawala,likishindwa litaenda underground kusubiri muda muafaka.
Lakini kitakachounganisha CCM na vyama vya upinzani ni haja ya kuwa na katiba mpya ikiwemo serikali ya Tanganyika. Huko nyuma G45 iilifanya hivyo na kuungwa mkono na bunge la Jamhuri kwa kuwa mtawala alitokea Zanzibar.
Nayo Zanzibar inasubiri mwanya huwo ijinasue kwenye makucha ya Muungano.Katika mazingira hayo tutegemee mabadiliko makubwa ya kisiasa na labda kiutawala.