Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
ILANI YA CCM INATOA SULUHU YA MASWALI, ACT NA CHADEMA ZINALALAMIKA
Na Elius Ndabila
Nimefanikiwa kuzisoma Ilani za vyama vitatu, yaani Ilani ya CCM, ACT Wazalendo na CHADEMA. Nikiwa ninazipitia Ilani hizi nimegundua utofauti mkubwa kwenye kujibu mahitaji ya Watanzania.
Ilani ya CCM kama chama chenyewe kilivyo kikubwa na kikongwe Afrika basi hata Ilani yake ni kubwa. Ilani ya CCM ina kurasa 308. Ilani ya CCM imeeleza namna serikali ilivyofanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano ya 2015/2020 na imeeleza jinsi wanavyopanga kufanya kazi nyingine kubwa mwaka 2020/2025 kama watapewa ridhaa tr 28.
Ilani ya CCM inatoa mwelekeo kama Taifa na kuonyesha namna walivyo jipanga kuendelea kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta mbalimbali za kimaendeleo hasa Elimu, Afya, Mawasiliano, Viwanda, Maji, Michezo n.k. Hata hivyo Ilani inaendelea kusisitiza juu ya kuendelea kusimamia Amani ya Taifa ambayo ni tunu.
Ilani ya CCM ya mwaka huu imeeleza wanategemea kufanya nini kwenye kila Wilaya kwa miaka yao mitano watakapopata ridhaa, zaidi kuendeleza kasi ya kuliletea Taifa Maendeleo.
Lakini ukisoma Ilani ya ACT Wazalendo ambayo ina kurasa 60 na Ilani ya CHADEMA ambayo pia ina kurasa 104 zimejaa kulalamika. Ilani hizi mbili ambazo Utadhani walikaa pamoja na kuziandika mengi yaliyoandikwa kwenye hizo kurasa chache ni:-
Wanalaani ukandamizaji wa demokrasia, wanalaani Uhuru wa vyombo vya habari, Wanalaani watu kubambikiwa kesi na kupelekwa jela, Wanalaani ununuzi wa ndege bila Ridhaa ya Watanzania, Wanaskitika Serikali kukopa fedha na kujenga miradi mikubwa kama SGR na Mradi wa Umeme, Wanalaani Bunge Kuto kuwa mubashara n.k
Baada ya malalamiko wanasema wao wataboresha Kilimo, Uhuru wa habari, kuwatoa watu magerezani, kupunguza madaraka ya Rais n.k Lakini ACT wao wanaongeza kwa kusema watu watakula Bata.
Ukisoma kwa umakini Ilani hizi utaona kuna vyama wanawatania Watanzania, hawako serious. Huwezi kuandika Ilani kwa kulalamika. Ilani inatakiwa kuonyesha matarajio yako ukipata zamani unategemea kufanya nini? Ilani ya upinzani inatakiwa kuonyesha wapi Ilani ya Chama Tawala ilifeli na wao watafanya nini?
Lakini kubwa zaidi Ilani ya Upinzani ilipaswa kuwa kubwa kuliko ya CCM kwa kuwa wao wapo nje na wanaona makosa mengi. Lakini kitendo cha kuwa na ilani ndogo inaonyesha fika CCM imefanya makosa machache hivyo bado tunastahili kuendelea kuongoza.