Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,982
- 51,157
Kuna mtu aliniambia kuwa CCM bungeni imejaza watu wasiosoma, nikamtalia kabisa.Nikamwambia katika bunge Lililojaza wasomi na wasomi wabobevu ni hili la Sasa.
Baadhi ya watu hawajui ni kwa nini nchi imejaza wasomi lakini bado watu wanadhani hatuna wasomi. Tatizo ni kwa CCM kuwepo kwake madarakani, usomi hauna maana tena.
Watanzania wametoa maoni kuhusu mambo mbali mbali juu ya nchi yao lakini wamepuuzwa na watawala toka CCM.
Kwa muda mrefu Sana watanzania wamevumilia mambo mengi mabaya yanayotendwa na CCM hadi mioyo yao imepigwa ganzi.
Matokeo yake watanzania wamegeukia upande wa kufanya mizaha kwenye kila jambo. Kwenye mizaha watanzania ndiyo wanajihisi wapo salama.
Nchi iliyojaa wafanya mizaha, Iko siku mizaha hiyo itatumbuka usaha.