CCM imvue Uanachama na kumfukuza kabisa Chamani Askofu Gwajima haraka sana bila kuchelewa

Ukienda ugenini ni lazima ufuate na kuzingatia maadili ,miiko na utamaduni wao na siyo kujikurupukia zako.
Wazungu walikuja Africa wakatufundisha mambo Yao. Nasi Leo tunajivunia ustarabu wao. Zikiwemo dini, nguo, elimu, nyumba n.k.

Ngwajima anawafundisha CCM ustarabu, mzuri tu. Sio vibaya mkaiga na kusonga mbele. Itasaidia kuendelea kuaminika kwa wananchi. Sasa hivi bila Dola kushinda inakuwa kazi sana.
 
Lukas acha uzandiki acha Roho mbaya acha utekaji kuua kuwabambikia kesi za uongo chadema, ujue na wewe utakufa na kukutana na wale wote uliowaua , mipango yako yo kishetani uache mara moja mwache Gwajima atoe maoni yake kwani ni haki yake kikatiba na sheria
 
Kwa sasa ccm bila Polisiccm, mahakamaccm, magerezaccm, DPPccm ni Weupe sana
 
Naona sindano zimewaingia mpaka mmeanza kunena kwa lugha...
Eti siyo mwenzenu!! Ilikuwaje mkawa nae !?
 
Ndio maana mimi sisomi mtango wake pamoja na yule thaadi. Hawana wanaloeleza isipokuwa kuongea utumbo.
 
Si uwa mnaimba hapa kila siku kuwa ccm ni baba wa demokrasia?. Kelele Kidogo za Gwajima mnaanza kutoa makucha. Demokrasia ni uvumilivu wa kukubali kusikia usiyoyataka na ukabaki na amani.
 
Akili fupii sanaa ndio. Suluhisho lenu and hiyo tutaisikia ndio maazimio.ya kikao chenu cha keshokutwa
 
Si uwa mnaimba hapa kila siku kuwa ccm ni baba wa demokrasia?. Kelele Kidogo za Gwajima mnaanza kutoa makucha. Demokrasia ni uvumilivu wa kukubali kusikia usiyoyataka na ukabaki na amani.
Ujinga hauvumiliwi. Chama kinachoweza kuvumilia ujinga jinga hakiwezi kudumu.
 
Kwa sasa ccm bila Polisiccm, mahakamaccm, magerezaccm, DPPccm ni Weupe sana
Hata ije Tume ya uchaguzi kutoka Marekani bado CCM itashinda kwa kishindo kikuu kitakacho itetemesha Dunia nzima
 
Mbona wewe hujauwawa
 
Utabiri wa marehemu shekhe Yahya unaenda kutimia ya Zambia na Senegal yanaenda kutokea Tanzania na ndipo ccm itakuwa kama KANU ya kenya kwa kweli na vyote hivyo vitasababishwa na ccm kupokea ushauri wa watu kama Lukas
 
Ikifanya hivi, ccm itakuwa imeondoka kwenye misingi yake ya kutetea wanyonge na kupinga maovu.Gwajima pamoja na mapungufu yake yote kwa hili ameonyesha uzalendo kwa nchi na chama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…